Kati ya penzi la mzee au penzi la kijana lipi limanoga zaidi?

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
12,605
2,000
Jana nilikuwa airport napata huduma, katika kusubiria huduma kukawa na malumbano Kati ya binti mmoja na Mzee mmoja

Mzee: akawa anamtania Huyo binti kuwa amuoe wawe wapenzi, atampatia Mapenzi ya Raha, kupetipeti aachane na vijana, vijana NI stress, amkubali atamlea binti kama Yai, tena Mimi NI MTU wa Tanga

Binti: woi, we Mzee ujana ule na Nani, uzee umalizie na Mimi? Usiniletee gundu la maisha, Kwanza mume WA mtu Mimi simtaki

Mzee: Mimi naruhusiwa kuoa wake wengi, kwahiyo usiwe na wasiwasi

Binti: Mzee naomba nikuombe Radhi kabla ya haya nayotaka kusema, mimi siwezi oleww na mzee wala kuteleza na Mzee. Bora niolewe na Kijana mwenzangu tupambane na maisha na akili yangu ichangamke kuliko kupetiwapetiwa Kila siku na Mzee niwe kama kamasi, nimefungiwa ndani kama paka la kiarabu naishia kuwa zuzu

Mzee: vijana wanasumbua binti nikubali Mimi Mzee sikusumbui na hautofanya kazi, wanawake NI mapambo sio kuchakarika kama vichaa

Binti: Bora nisumbuliwe na Kijana akili isimame kuliko Mzee kunifanya ndondocha WA kukaa ndani kisa Raha, KAZI nitafanya sana ndio furaha yangu

Nikuulize mdau WA JF, je Kati ya penzi la Mzee na Kijana lini linanoga zaidi? Hili ni swali la wote wanaume na wanawake
 

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
40,051
2,000
Ngoja waje wanawake maana kwa upande wetu inafahamika kuoa mwanamke aliyekuzidi umri ni kwa wachache wanajifanya kujitoa akili na kuona ni sawa!
Nikuulize mdau WA JF, je Kati ya penzi la Mzee na Kijana lini linanoga zaidi?!
hili ni swali la wote wanaume na wanawake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom