Kati ya ndoa na ujenzi nianze na kipi?

Kati ya ndoa na ujenzi nianze na kipi?

Wanabodi habari za Muda huu.

Naomba kwa wale wenye uzoefu na walionitangulia ktk haya mambo naomba tufahamishane ni kipi muhimu kuanza nacho kati ya Ndoa au Ujenzi wa Nyumba?

Tushauriane tafadhali...
Yani wewe unataka uolee kwenyu nyumba za wenzako??
Jenga kijana..
 
Ndoa haikuzuiii kuendeleza mipango na malengo uliyojiwekea

Ukiitazama ndoa kwa mitazamo ya kidunia utaona ndoa kama kifungo cha jela

Ukiitizama ndoa katika jicho la kiroho utagundua ndoa ni vazi jema lenye kumkaa vyema kijana na binti

Faida nyingine ndoa huipa changamoto akili ya muoaji na muolewaji......muhim omba upate mke mwema
 
Mkuu, Nenda sambamba... usianze na jengo!! gawa na ubalance bajeti yako!!
Mke uwenae na jengo uanze poelpole (kiwanja na msingi) huku maisha yakisonga mbele.....
kila la kheri
Nashukuru sana. Kiwanja nimeshapata. Sasa safari ya Ujenzi naifahamu sio ya kitoto. Upande mwingine mchumba ninae mwaka wa Pili Sasa. Yeye ananishauri kwanza nijenge ili tukitoka fungate tuingie kwetu. Yupo sahihi sana. Shida ipo kwangu. Umri unaenda halafu hatuyajui ya Kesho. Natamani nipate mtoto. Na ili nipate mtoto inabidi kwanza nimuoe kwanza ili Mtoto azaliwe ndani ya ndoa. Mchumba hajakataa ila haonyeshi kuridhia kumuoa bila kuwa tumejenga.
 
Nani kakwambia? Kipi kati ya Ndoa(Mke) na Nyumba unaweza kutoa talaka na kuachana nacho?. Anza na kile ambacho huwezi kukitolea taraka kwanza. NYUMBA NDO KILA KITU.
Sasa nitaishi mwenyewe? Halafu kwanini nioe huku nawaza talaka?
 
Vyote muhimu unategemea aina ya mchumba
1. Kama ni mchumba bi shoo anza na ujenzi kwani hawezi kuwa msaada hata ktk ujenzi wenyewe
2. Kama mchumba ni mchakarikaji anza na ndoa kwani atakusaidia hata kusimamia ujenzi wenyewe.
Mchumba namkubali. Kimsingi ndio alieniamsha usingizini.
 
Jenga mkuu kuoa unaongeza familia kuongeza familia ni kuongeza matumizi fikiria mkuu kama unauwezo Wa kufanya kitu hasa ujenzi Fanya sasa gharama za maisha zinapanda kila siku
Kazi kweli kweli. Vyote vinaumuhimu sana. Suala nianze na kipi. Opportunity Cost. What will I be losing nikianza na kimoja wapo? Kipato changu ni cha wastani. Sio kikubwa. Sio kidogo.
 
Wanabodi habari za Muda huu.

Naomba kwa wale wenye uzoefu na walionitangulia ktk haya mambo naomba tufahamishane ni kipi muhimu kuanza nacho kati ya Ndoa au Ujenzi wa Nyumba?

Tushauriane tafadhali...
Ndugu nakuomba uanze na ujenz mapenz yapo tu na hakikisha hicho kiwanja kina jina lako. Wanawake huwa washenzy sana unaweza kumfanyia kila kitu ila baadae akakukusaliti. Jenga, kwanza kisha ndio mchukue huyo mwenzio sbb ukimuoa kila kitu kitakuwa juu yako na gharama ya kuendesha maisha itakuwa juu, utashangaa unapata mtoto1,& 2 na pia upande wa mkeo wataanza kukupiga vizinga utajenga lini. Halafu kila siku gharama zinaongezeka hv unafikiri utajenga lini? Na utakapoanza kuchacha huyo mwanamke anaweza kukukimbia.
Usikimbilie kutumbukiza dudu yako tu kwa ke mkuu. Tafakari kwanza maisha yako leo utapuuzia hiyo nafas ya kujenga lkn baadae itajuta, pesa inaweza kuwa ngumu na vifaa vya ujenz vikawa gharama sana mara 2 ya ss
 
Daah!! Sawa Mkuu japo ndio unazidi kuniogopesha. Ukubwa taabu kweli kweli.
 
Ndoa haikuzuiii kuendeleza mipango na malengo uliyojiwekea

Ukiitazama ndoa kwa mitazamo ya kidunia utaona ndoa kama kifungo cha jela

Ukiitizama ndoa katika jicho la kiroho utagundua ndoa ni vazi jema lenye kumkaa vyema kijana na binti

Faida nyingine ndoa huipa changamoto akili ya muoaji na muolewaji......muhim omba upate mke mwema
Asante sana. Asante kwa huu ushauri wako mzuri.
 
Inategemea uko kijijini au mjini? Na uwezo wa familia unakotoka ukoje? Kama uko kijijini kujenga ni rahisi some how maana 8mil waweza kujenga nyumba yenye hadhi na huko tena yaweza kuwa nzuri tu. Kwa mjini ili ujenge yahitaji kwanza uwe na kiwanja na minimum cost kwa nyumba ya kawaida ni kama 40 mil.
Sasa wewe endelea kusubiri mpaka ujenge ndio uoe! Utazeeka ukiwa na msingi tu. Oa kwa kwanza ndio uwaze kujenga, hata myumba ya kupanga ina heshima yake maana si wote wenye uwezo wa kupanga. Angalia na age yako, kama bado una miaka 20 waweza kuanza na ujenzi, ila kama una approach 30yrs hilo la kujenga liende sambamba na ndoa
 
Back
Top Bottom