Ben-adam
JF-Expert Member
- Jun 2, 2023
- 1,126
- 2,517
Kati ya mwanaume na mwanamke, nani hupitia maisha ya tabu zaidi ndoa inapovunjika? tukitazama hali halisi ya maisha ya Watanzania, ukweli unauma: wanawake wengi wanakosa uhuru wa kiuchumi!
Mwanamke wa Kitanzania analelewa kuamini kuwa mwanaume ndiye "mkombozi wake" kifedha. Matokeo yake, wengi wanapofiwa, kuachwa au ndoa kuvunjika, maisha yao yanaanguka ghafla. Kwa nini?
Hawakuwa na mpango B wa kiuchumi, angalia mtaani jinsi single mothers wanavyoishi kwa tabu, (Wana depression haó) na utagundua wengi maisha yao yamebdilika baada ya ndia zao kuvunjika au sababu zinazofanana na hiyo
Mwanamke anapobaki peke yake bila rasilimali au kazi ya uhakika, ana hatari kubwa ya kuishi maisha magumu sana. Wanaume wengi huweza "kusimama tena" kwa sababu waliwekeza kwenye kazi, biashara, au vyanzo vyao vya kipato.
Hata ukiwapa mtaji wa milioni 10, ni wangapi wataitumia vizuri na kuifanya iwe chanzo endelevu cha kipato? Fanya utafiti. Pesa za wanawake wengi huishia kwenye matumizi ya haraka, sio uwekezaji wa muda mrefu, ni wangapi wenye project zao wenyewe?
Mwanamke asiye na uhuru wa kiuchumi akipatwa na changamoto (mfano kufukuzwa kazi au biashara kuanguka), mara nyingi huchagua mojawapo kati ya haya:
Kutafuta mwanaume/wanaume wengine kwa msaada wa kifedha (kujiuza) au
Kurudi kwa wazazi
Kuhangaika na maisha yasiyo na uhakika
💥Ukweli mchungu ni huu: Mwanamke wa Kitanzania anahitaji mwanaume ili aendelee kuishi vizuri
Si kwa sababu hawezi, bali kwa sababu mfumo unamfundisha kutegemea zaidi badala ya kujitegemea.
Lakini je, hii ni lawama kwa wanawake pekee? Hapana.
Mfumo wa malezi unawajenga hivi.
Wanaume wengi wanapenda wake waliowategemez.
Fursa kwa wanawake bado ni chache ukilinganisha na wanaume.
Suluhisho ni nini?
Wanawake wafundishwe uhuru wa kifedha kutoka wakiwa wadogo.
Misingi ya ndoa ibadilike, ndoa isiwe mkataba wa utegemezi bali ushirikiano wa maendeleo.
Wanawake wajifunze kuwekeza na kusimama wenyewe hata wakiwa ndani ya ndoa.
Tukubaliane, ndoa ikivunjika, mwanaume anapata shida kiakili na kihisia, lakini mwanamke anapata shida zaidi kiuchumi. Na ukiwa na shida ya pesa, maisha yanakuwa magumu mara mbili zaidi!
Je, unakubaliana? Tupe mawazo yako!