Kati ya Mbagala na Gongo la Mboto wapi kuna watu wengi?

Binafsi na naanza na Mosi kusema Gongo la mboto ina watu wengi kuliko Mbagala kwa sababu Gongo la mboto kuna treni la mwakyembe ambalo lililetwa naamin linabeba sio chini ya watu buku au zaidi kwa tripu moja na kwa siku linapiga tripu 3 asubuhi na tripu 3 jioni ila pamoja na hivyo bado daladala za kkoo na posta zinazoenda Gongo la mboto zanapiga kazi kama kawaida wakati mbagara majuzi Mwendokasi wamefanya majaribio madaladala wameeanza kulia kulia abiria hakuna.
Kwanza unaizungumzia Mbagala ipi?! Mbagala ya kwenye vitabu vya Serikali au Mbagala ya Asili ambayo kutokana na ukubwa wake ikalazimika kuvunjwa vunjwa?! Mbagala ya asili inahusisha Mbagala yenyewe, Kiburugwa, Charambe, Kilungule, na Kibonde Maji. Hapo population ni zaidi ya 200K. Ukisema uiingize na Chamazi hesabu unanusa 500K! Hiyo, ndo MBAGALA.

Kuna mtu kaitaja Tandika na Buza. Hizo hazihusiani kabisa na Mbagala, labda angeitaka Maji Matitu, kwa sababu na yenyewe ni Mbagala!

Kwa upande mwingine, unakosea sana kutumia kigezo cha watu kujazana kwenye daladala. Hebu kwanza tafakari: Je, unaamini Gongo la Mboto ina Machinga wengi kuliko Mbagala?! Je, unaamini Gongo la Mboto kuna sehemu yenye pilikapilka nyingi za kibiashara kama ilivyo pale Rangi Tatu?! Je, ni maeneo mangapi Gongo la Mboto yapo busy sawa na pale Zakhem?!

Maeneo yote ya Mbagala niliyokutajia yana Machinga wengi sana. Na kutokana na kukua kwa Mbagala, Machinga wengi hawana sababu ya kupanda magari kwenda mjini kufanya biashara kwa sababu biashara zao zinaishia kule kule Mbagala! Ukiacha Rangi3 as a business center, mbele kidogo unaikuta Zakheim, napo kuna wafanyabiashara kibao ambao hawalazimiki kupanda gali kufika hapo. Ukitoa wa Rangi3 na Zakhem kuna kundi lingine kubwa sana linalofanyia biashara zao Tandika. Nadhani unafahamu ukubwa wa Tandika as business center. Hawa wa Tandika nao hata wakipanda daladala, hawapandi BRT wala zinazoenda mjini. Ukitoa kundi la Wachuuzi wanaoenda Tandika, kundi lingine kubwa linaenda Buguruni, Machinga Complex, na Mchikichini. Hawa nao wanapanda daladala lakini sio ziendazo mjini wala BRT.

Ukiondoa kundi hilo, unakutana na kundi lingine kubwa sana sana. Hawa hawapandi daladala ya aina yoyote kwa sababu biashara zao ni za kutembeza. Naandika sentensi hii takribani saa moja kasoro jioni. Ukifika pande za kuanzia Mtongani kuelekea Mbagala mida kama hii, utakutana na kundi kubwa sana la watu wanaotembea kuelekea Mbagala na wengi miongoni mwao ni Wachuuzi ambao ukitaka kupima uwingi wao kwa kuangalia wanapopanda daladala lazima uibuke na wrong data! Wachuuzi pekee watakaopanda sana BRT na Daladala za K/koo ni wale wanaofanyia biashara zao K/koo na wenyewe ni wengi sana!!
 
Mzee ebu kuwa serious hivi unaijua 500k vizuri yahn mbagara iwe na watu 200k aisee umeenistua sana naamini huzijui namba vizuri.

Nijuavyo mimi mbagara mwisho pale ndio kuna changanyiken ya watu ambayo pia kumbuka kuna watu kibao wanatoka goms wanaenda huko mbagara kupiga mishe ........

Chunguza gari za goms kwenda mbagara mara nyingi
asubuh zinajaa zikitoka gomsi kwenda mbagara na jioni zinajaa sana zikitoka mbagara kwenda gomsi hii maana yake ni kuwa katika hilo nyomi la mbagara kuna nyomi la watu wanaotoka gomsi na kwenda mbagara na kurudi kwa maana rahisi wanafanya mishe zao mbagara ila wanaishi Goms.

Fact ya daladala huwezi kuipotezea maana ndio indicator ya kujua wapi kuna watu wengi kuna sehemu mida ya jioni gari bwelele ila kuna maeneo gari kupata ni mapambano mfano pale station gari za mbagara zinakuja hata sio za kugambania sana.

Gongo la mboto hapa jua inaanzia airport,banana,mombasa,kituo kipya,gomsi,pugu,chanika,homboza,zingiziwa hiyo yote ni miji inakuwa na ina ruti zake za kwenda mjin.

Hapa inabidi apatikane mtu wa sensa na takwimu ndio atamaliza utata.
 
Ukikaa hapo karume afu ukatazama dalala namna zinavyo gombewa utasema mbagala inawatu wa kutosha kuliko G/mboto, ukizicheki dalala za mbagala-mbezi takribani muda wote zinabeba watu wengi asubuhi,mchana,jioni

Kwa kigezo hiki inaonesha mbagala inawatu wakutosha
 
Goms ina watu aiseee
Nimezaliwa rugambwa - madafu, nimesoma juhudi ukonga, maisha nimetafutia goms na mke mtarajiwa nimempatia goms[emoji1787]
Kwanza kuna treni mbili, inayopiga safari za majini yani kariakoo (zamani posta).

Nyingine ya TAZARA inayoanzia tazara mpaka pugu. Hizi treni zote zinajaza kwa trip tatu tatu (saa 1600, 1800, 200)hrs.

Daladala ziko nyomi mwanzo mwisho, bodaboda ziko full, maguta na virikuu zote full.

Bado sisi wapiga jogging mdogo mdogo (hatuna nauli) kutoka karume tuko wengi barabarani.
 
We hamna wewe Balaa la Mbagala haulijui wewe.
Siku nimekuja kujua mbagala ina watu wengi baada ya kushika top 3 kwa shule za msingi zenye watoto wengi.
1-mbande primary ina wanafunzi 9800
2-chamazi ina wanafunzi 8500
3-mbagala rangi tatu ina wanafunzi 8300.
NB:madarasa yote kuanzia std 1-std 7 wanafunzi mpaka walimu wanaingia kwa shift.
Hata ukiangalia muundo wa shule zenyewe sio za kitoto utasema kambi za jeshi
 
Back
Top Bottom