Kati ya hawa WANNE nani ufanikiwa haraka kama Wote mkianza siku moja...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,735
1:Anamtegemea Mungu katika kazi zake zote 100%...
2:Anategemea waganga na madawa 100% katika shughuli zake za kujitafutia kipato...
3:Anachanganya Mungu 50% na waganga 50% katika shughuli zake za kutafuta...
4:Hategemei kati ya viwili vya mwazo, yeye anategemea juhudi, ubunifu na maarifa tu...

wakina nani mitaani kwet tukiacha zile stori za kwenye "GET RICH QUICK BOOKS"
 
Namba 4, Mungu na waganga hawajawahi kushinda nguvu ya ubunifu na kufanya kazi kwa maarifa...tazama waafrika wanomtegemea mungu na waganga hali yao ilivyo
lakini kuna story nyingi matajiri wengi afrika huwezi kuwatenganisha na waganga.
mimi naamini mchanganyiko wa 1 na 4
 
''Imani yako ndio itakayo kuponya'' namaanisha kila mtu atafanikiwa kwa kile anachoamini kitamsaidia, iwe Mungu, mganga, juhud etc, coz hakuna 4mula kwenye haya mambo, dats y wote mnaweza kumtegemea Mungu na huyu akafanikiwa huyu asifanikiwe, kiufup mafanikio hutokana na combination of various aspects na hicho ulichotaja ni kimojawapo tu.
 
Hata ukimtegemea MUNGU... Au mganga kama huna JUHUDI NA MAARIFA ktk KAZI ZAKO au biashara zako ni BURE....MUNGU yupo Lakin unapaswa ufanye JUHUDI ZA MAISHA.... kwani HATA HUKO MISIKITINI na MAKANISANI ni NYUMBA ZA MUNGU lakini HAWAACHI MILANGO WAZI....USIKU....omba MUNGU na UKILALA PIA FUNGA MLANGO.....usilale mlango wazi japokuwa UKIMTEGEMEA MUNGU..
 
Tena wanaweka na walinzi wenye bunduki nzito nzito kabisa na CCTV kamera kila mahala...

Hata ukimtegemea MUNGU... Au mganga kama huna JUHUDI NA MAARIFA ktk KAZI ZAKO au biashara zako ni BURE....MUNGU yupo Lakin unapaswa ufanye JUHUDI ZA MAISHA.... kwani HATA HUKO MISIKITINI na MAKANISANI ni NYUMBA ZA MUNGU lakini HAWAACHI MILANGO WAZI....USIKU....omba MUNGU na UKILALA PIA FUNGA MLANGO.....usilale mlango wazi japokuwa UKIMTEGEMEA MUNGU..
 
wewe lala kanisan msikitini uone kama Mungu atakushushia pesa. biblia yenyewe inasema asiyefanya kazi na asile hata kama ni bishop .
 
Duh, watu hawana tena hofu ya Mungu jamani. Mmeingiwa na pepo gani.

Katika mafanikio mtegemee Mungu 100%, fanya kazi kwa bidii na maarifa sana utafanikiwa.

Ukimtegemea Mungu atakuzidishia maarifa na kukupa kibali cha kukubalika katika sehemu mbalimbali katika biashara yako. Lakini mara nyingi biashara huambatana na uovu mwingi. Kama unamtegemea Mungu utaepuka maovu mengi kama ya dhuluma, rushwa, wizi n.k

Utakuwa na biashara safi na isiyo na uchafu wowote huku ukijua vyote vyatoka kwa Mungu.

Kama humtegemei Mungu ndo wale wanaopata hasara kidogo na kuishia kupata magonjwa ya moyo na hata wengine kujiua kabisa.

Asikudanganye mtu kumtegemea Mungu inalipa zaidi.
 
Ukitaka kufanikiwa na usipate presha yoyote wala usipoteze chochote, mtegemee Mungu asilimia 100. Kumtegmea Mungu ni pamoja na kumwomba ili:_ a) akupe maarifa ya kugundua fursa za kukufanikisha b) akukutanishe na watu watakaokusaidia katika safari yako ya mafanikio na kukwepesha na watakaokuharibia c) akupe afya njema na akulinde na wabaya wanaotaka kukuharibia.

Hata ukiwa na juhudi kiasi gani kama Mungu hajakusaidia kwenye kuchagua shughuli za kufanya, unaweza kuishia kupata hasara. Mungu anaweza kukuongoza ukafanya shughuli fulani kwa wakati ambao ndio wa mafanikio lakini watu wengine waliofanya shughuli hiyo hiyo wakaambulia hasara kubwa. Mfano:- Mwaka jana tuliona kwenye vyombo vya habari namna ambavyo watu waliolima nyanya walipata hasara kubwa sana. Miezi miiwili iliyopita watu waliokuwa wamevuna nyanya kama hizo hizo waliziuza kwa pesa nyingi sana.

Ukimtegemea Mungu anaweza akukutanishe na mtu atakayekupa ufahamu juu ya jambo ambalo ulikuwa hulijui lakini baada ya kulijua ukalifuatilia na kulifanya na kujikuta umejikomboa kimaisha.

Tena, kama Mungu hajakupa afya njema, utafuatiliaje shughuli zako ufanikiwe?
 
Back
Top Bottom