Kati ya haki na amani kipi ni muhimu zaidi na kipi hutangulia kingine?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
15,812
Reaction score
40,297
Naomba niwaulize hasa viongozi wa dini wa kiislamu na kikristo kati ya hayo mawili kipi huanza ili kingine kifwate.

Mfano.
Mtu anaiba kura ukikemea unaitwa mchochezi Yani mwizi wa kura anakuwa na haki kuliko yule anayefichua wizi.

Ndani ya jamii kuna utekaji na mauwaji ya raia holela anayekemea utekaji anakamatwa na kufanyiwa ufedhuli ila mtekaji na muuwaji wa raia analindwa.

Rasilimali za nchi zinaibiwa na kuporwa na mafisadi anayefichua mafisadi anakamatwa na kuwa na hatia au kuuwawa ila mafisadi yenyewe ndio Yana lindwa.

Mifumo yote ya uchaguzi ni uongo na kiini macho na imewaumiza wengi anayelilia mabadiliko ya haki anakamatwa na kutaka kunyongwa ila majizi ya uchaguzi yanatamba.

Mahakama zote zipo corrupt hazitoi haki tena ila zinasubiri maelekezo ya nini Cha kufanya katika mazingira kama haya je wapenda haki mabadiliko na maskini wanapoonewa na mifumo iliyohodhiwa na majizi na kulindwa na Dola waki react kujikomboa ni kosa?
 
Mahakama zote zipo corrupt hazitoi haki tena ila zinasubiri maelekezo ya nini Cha kufanya katika mazingira kama haya je wapenda haki mabadiliko na maskini wanapoonewa na mifumo iliyohodhiwa na majizi na kulindwa na Dola waki react kujikomboa ni kosa?
 
HAKI ni mama wa AMANI, kwa sababu ili kuwe na Amani lazima Haki iwepo,

Unapohubiri Amani alafu hamna haki hapo hakuna Amani Bali Kuna kimya Cha watu waliokata tamaa
 
HAKI
 
HAKI ni Tunda la amani, HAKI huinua Taifa.✍️📌
 
Wana ccm hutawaona wakikoment nyuzi kama hizi wao utawakuta wanahubiri amani tuuuu ila nyuma wameficha mapanga. Na hiyo amani wanayoihubiri ni ili wale Kwa utulivu bila kubugudhiwa shenz type.
 
Amani ni mtoto wa haki. Pakiwa na haki, amani inakuja yenyewe..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…