Katavi: Waganga wa tiba asilia kujengewa hospitali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera amesema wana mpango wa kujenga Hospitali itakayotumiwa na ‘Waganga wa Tiba Asilia’ katika Mkoa huo ambapo ujenzi huo unatokana na fedha kutoka kwa Waganga wenyewe.

RC Homera amesema Hospitali hiyo itasaidia kuondoa ramli chonganishi katika Mkoa huo na kuwaondoa ‘Waganga wa Tiba Asilia’ kutoka vichochoroni na kuwa sehemu moja na kwamba Waganga hao watapeana zamu ya kutibu katika Hospitali hiyo.

 
Wastage of time and resources, anadhani watahamishia mizimu na dunguli hapo? Ana uhakika gani kuwa watafanya kazi? suala la kufanya kazi kwa zamu ni upuuzi, je wale wasiokuwepo zamu siku hiyo watakuwa wanafanya nini na watakuwa wapi kwa uangalizi wa nani kuwa hawafanyi ramli chonganishi kwa wakati ambao hawapo kwenye kituo chao?

I see this being another rubbish idea
 
Wastage of time and resources, anadhani watahamishia mizimu na dunguli hapo? Ana uhakika gani kuwa watafanya kazi? suala la kufanya kazi kwa zamu ni upuuzi, je wale wasiokuwepo zamu siku hiyo watakuwa wanafanya nini na watakuwa wapi kwa uangalizi wa nani kuwa hawafanyi ramli chonganishi kwa wakati ambao hawapo kwenye kituo chao?

I see this being another rubbish idea
Hivi Dr. Mwaka, Ndodi wamewahi tibu kwa mizimu ama walikuwa nayo kwa ofisi.
 
Mizimu haitofanya kazi hyo

Hivi kutumia dawa ya kienyeji kutibu vidonda vya tumbo, kisukari, typhoid inahitaji mizimu

Hospitali haitokuwa inatibu mambo ya ulozi ama kupigwa vipande ila wale walio pimwa hosp. za kawaida na kukutwa na magonjwa kama kisukari, typhoid isiyo koma, utia sugu, malengelenge.

Hawa ndo wamelengwa ( kwa uelewa wangu) ila nashangaa mnavyo waza mizimu. mawazo ya kichawi yamewatawala sana vijana

Watu wanatumia miti shamba kutibu maralia, UTI wewe wauliza mizimu itakuwepo
 
ivi kutumiq dawa ya kienyeji kutibu vidonda vya tumbo, kisukari, typhoid inahitaji mizimu

hosp. haitokuwa inatibu mambo ya ulozi ama kupigwa vipande ila wale walio pimwa hosp. za kawaida na kukutwa na magonjwa kama kisukari, typhoid isiyo koma, utia sugu, malengelenge.

hawa ndo wamelengwa ( kwa uelewa wangu) ila nashangaa mnavyo waza mizimu. mawazo ya kichawi yamewatawala sana vijana

watu wanatumia miti shamba kutibu maralia, u.t.i ww wauliza mizimu itakuwepo
Daaaah hapo nmekpata mkuu nlikua na mwawaO hasi kwa hyo koment yako umenifumbua vitu mkuu
 
Kwahiyo kila siku mganga ikifika zamu yake anabeba furushi lake la mizizi na matunguli ya kufanyia kazi kutoka nyumbani au watakuwa wanashare...?
 
Possibly kama walikuwa wanafanya ramli chonganishi alizosema RC
Mkuu ramli chonganishi ni matokea ya mgonjwa kutopima hivyo ramli inatumika kama kipimo cha kujua ugonjwa

Kama wagonjwa wangekuwa wamepimwa toka hosp. na kujua huyu anaumwa kichwa, kisukari ama tumbo basi angepewa dawa stahiki.

Kama watu tungeenda kwa waganga tukiwa tunajua tunamwa nn? bas kusingekuwa na ramli chonganishi
 
Kwahiyo kila siku mganga ikifika zamu yake anabeba furushi lake la mizizi na matunguli ya kufanyia kazi kutoka nyumbani au watakuwa wanashare...?
Kuna ripoti inasema 98% ya wa tz inaamini katika uchawi haya ya tunguri yanakuja vp?

Umewahi sikia tunguri ikatibu maralia, typhoid ama miguu kuwaka moto ama presha

Tunguri ni kwa ajil ya mambo ya giza pale watatibu watu walio pimwa na kukutwa na magonjwa yanayo fahamika ila dawa za hosp. zimeshindwa wapa nafuu

Hakuna mambo ya mizimu, tunguri wala chale pale
 
Duh! wagonjwa watakuwa wanaenda kutibiwa wamebeba kuku mweusi, mbuzi, asali nakadharika:D:D:D itabidi pawe na zizi la kuhifadhi mifugo
 
Hapo unaambiwa chukua hizi lita 5 za dawa unywe kwa siku mbili halafu zingine chemsha uogee na nyingine sukutua na zingine jipake
Yaani huwa nacheka nikiona wanavyotoa matibabu hawa jamaa
Dawa moja inatibu magonjwa 50
 
sasa kila mganga ana dawa zake na zinatofautiana raw material ingawa zinatibu ugonjwa mmoja.je kama mgonjwa kalazwa mganga wa shift anamuanzishia dozi yake na kusitisha ya yule aliyetoka zamu????
 
HILI NI JEMA SANA NA NADHANI KILA MKOA UWE NA JENGO LA TIBA ASILI ZA MITI SHAMBA.NA WATIBABU WOTE WAWE VERIFIED,KWANI HII HASWA NDIO ASILI YETU YA KIAFRIKA NA TIBA ZETU,TUSIDHARAU TIBA ZETU,KWANI HATA MWL.JKN ALIWAHI SEMA KARIBU 80% YA DAWA ZOTE HOSPITALI HUTOKANA NA MITISHAMBA.
HONGERENI SANA.
 
Back
Top Bottom