Katavi: Ugonjwa wa Surua umeua Watoto 12 Wilaya ya Mlele

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Jumla ya watoto 12 wamefariki kwa ugonjwa wa Surua, katika wilaya ya Mlele tangu Desemba 2022, mkuu wa wilaya Majid Mwanga ameiambia BBC. Aliongeza kuwa watoto 847 wameambukizwa ugonjwa wa surua wilayani humo kati ya Desemba na Februari.

Wahudumu wa afya kufikia sasa wamewachanja watoto 16,480 na wanaendelea na zoezi hilo, Bw Mwanga alisema. Serikali imewataka watu katika eneo hilo kuachana na imani potofu-kama vile watoto wao walikufa baada ya kurogwa- na wapatiwe chanjo.

Miezi mitano iliyopita, Waziri wa Afya wa Tanzania aUmmy Mwalimu alitangaza kuzuka kwa ugonjwa wa surua katika mikoa saba. Alianza kampeni ya nchi nzima ya kutoa chanjo ya surua na rubela kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Watu wa rika zote wanaweza kupata surua, lakini huathiri zaidi watoto chini ya miaka mitano.

Surua kawaida huanza na dalili kama baridi, ikifuatiwa na upele siku chache baadaye. Watu wengine wanaweza pia kupata alama ndogo kwenye midomo yao.

1676977296239.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom