Watoto 12 wapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa surua Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
Watoto 12 wapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa surua Tanzania.jpg

Watoto 12 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na surua katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi kusini magharibi mwa Tanzania .

Kati ya kipindi cha mwezi wa 12 mwaka jana hadi kufikia mwezi wa pili mwaka huu watoto 847 wameambukizwa surua kwenye wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Mlele Majid Mwanga ameiambia BBC hadi sasa wamefanikiwa kutoa chanjo kwa watoto 16480 na wanaendelea na zoezi hilo .

Pamoja na kutoa elimu wakiwataka wananchi wa eneo hilo kuachana na imani potofu kuwa vifo hivyo vimetokana na imani za kishirikina na badala yake wasikilize na kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya pamoja na kuwapelekea watoto kupata chanjo .

Ugonjwa wa surua huathiri watu wa rika zote japokuwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ndio huathiriwa zaidi na dalili zake ni homa kali, udhaifu wa mwili pamoja na upele.

Miezi mitano iliyopita Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitangaza mlipiko wa ugonjwa wa surua nchini Tanzania na kuanza kampeni ya utoaji chanjo ya surua na rubela kwa watoto walio chini ya miaka mitano nchi nzima
www.bbc.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom