Katavi: Mke amkata Mume kwa panga kisha ajiua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mwanamke mkazi wa Kijiji cha Sibwesa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Wande Emmanuel (30), amemjeruhi mumewe, Dotto Enosi (35) kwa kumkata na panga kichwani kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia kitenge.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame Hamad, alisema tukio hilo lilitokea ljumaa, na chanzo ni ugomvi wa kifamilia unaohusiana na shughuli za kilimo.

Kamanda Hamad alisema mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kwa kutoshiriki katika shughuli za kilimo, hivyo kusababisha ugomvi.

Alisema kutokana na ugomvi huo Wande aliamua kumkata kwa mapanga mumewe na kumjeruhi baada ya kugundua kuwa anaweza kufariki na yeye kutuhumiwa kwa kesi ya mauaji.

Alisema baada ya kumjeruhi, Wande alizunguka nyuma ya nyumba yao na kujinyonga.

Kamanda Hamad alisema Dotto alipelekwa Hospitali ya Rufani mkoani Katavi kwa ajili ya matibabu, na sasa hali yake inaendelea vizuri.

FOYhVyYXoAE67PU.jpg

Chanzo: Nipashe
 
Yanaua na kutisha sana kwani siku zote mwanzo wake ni mzuri mno lakini mwisho wake mara nyingi ni kusikitika tu
 
Katavi kuna shida kubwa mahali fulani; sawa kabisa kama ilivyo kwa mkoa wa Geita.

Na Mungu apishie mbali tatizo hili lisije likawa halitokani na wazawa kwa sababu kuna kabila jingine pia na geni lililohamia huko; na ambalo ni la pili kwa ukubwa ndani ya mkoa huo, ukiondoa kabila lile la wazawa wenyewe wa mkoa huo
 
Nusu ya wanakijiji hapo Sibwesa ni hawamiaji Wasukuma, yaani wenyeji wa hapo Wabende wamefunikwa kila mahala, hata kwenye uongozi wa Kijiji.
 
Back
Top Bottom