Katambi azindua Kamati ya kuratibu uhamaji nguvu kazi

Katambi azindua Kamati ya kuratibu uhamaji nguvu kazi

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
726
Reaction score
953
KAMATI YA KURATIBU UHAMAJI NGUVUKAZI YAZINDULIWA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi amezindua Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu itakayoratibu Mradi wa Uhamaji Nguvukazi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika.

Mhe. Katambi amebainisha kuwa Mradi huo una umuhimu mkubwa katika kuhakikisha kuwa masuala ya uhamaji nguvukazi yanazingatia usalama, heshima, na ustawi wa wahamiaji.

Akizindua Kamati hiyo leo tarehe 26 Jijini Dar es Salam amefafanua kuwa Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu (National Technical Advisory Committee), jukumu lake kuu ni kuhakikisha kuwa mradi unatekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuongeza tija kwenye masuala ya uhamaji nguvukazi hapa nchini.

Mradi huo utasaidia katika kuwezesha vijana wanaoenda kufanya kazi nje ya nchi kupata kazi zinazozingatia viwango vya kazi za staha.

Mhe. Katambi amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itaendelea kushirikiana kwa karibu na Shirika la Uhamaji wa Kimataifa (IOM) katika kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi.

"Ushirikiano wetu utaendelea kuwa thabiti ili kuhakikisha kuwa malengo ya mradi yanatimizwa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya wananchi wetu"
IMG-20240727-WA0014.jpg
IMG-20240727-WA0015.jpg
IMG-20240727-WA0017.jpg
IMG-20240727-WA0018.jpg
IMG-20240727-WA0016.jpg
IMG-20240727-WA0013.jpg
IMG-20240727-WA0012.jpg
IMG-20240727-WA0010.jpg
IMG-20240727-WA0011.jpg
IMG-20240727-WA0009.jpg
IMG-20240727-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom