Kataa CCM, kataa ubaguzi, mpuuze Justin Mushi

Kataa CCM, kataa ubaguzi, mpuuze Justin Mushi

Kwa muda mrefu yamekuwepo madai kwamba Chama cha Mapinduzi na wanachama wake wamekua mstari wa mbele kupandikiza mbegu za ubaguzi na kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini, ukanda, ukabila au rangi. Lakini CCM imekuwa ikipinga tuhuma hizo kwa nguvu zote na kuzielekeza kwa vyama vya upinzani.

Lakini ni CCM haohao waliosema CUF ni chama cha waislamu mwaka 2000 baada ya kuona CUF imepata nguvu kubwa Tanzania bara. Kwahiyo wakasema ni chama cha kiislamu kwa hiyo wakristo wasikichague.

Mwaka 2005 CCM wakaanza propaganda kwamba CHADEMA ni chama cha kaskazini tena cha wachagga kwa hiyo wasio wachagga wasikichague. Propaganda hizo zimeendelea kuenezwa hadi sasa na wanachama na viongozi mbalimbali wa CCM.

Kwenye uchaguzi mkuu uliopita mtoto wa Rais mmoja mstaafu aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba nchi hii haiwezi kuongozwa na watu wa kaskazini. Huu ulikuwa ubaguzi mbaya sana. Nikajiuliza kwani yeye ni nani hadi afikie kusema hivyo? Nikajiuliza tena kwani watu wa kaskazini sio watanzania? sio binadamu? Mbona wanabaguliwa kwenye nchi yao wenyewe?

Kijana huyo hakuambiwa aombe radhi wala hakukemewa. Kwa kuwa CCM imeendelea kulea wanachama wake wanaofanya ubaguzi, bila kuwachukulia hatua yoyote basi wimbi la siasa za ubaguzi limeonekana ni kitu cha kawaida ndani ya chama hicho.

Jana rafiki yangu mmoja aitwae Justin Mushi ambaye ni mwanachama, kada na kiongozi wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) ameamua kuonesha waziwazi siasa za ubaguzi bila kujali athari zake kwa jamii.

Akichangia mjadala niliouanzisha kuhusu wakuu wa mikoa walioshindwa kwenye ubunge Justin alisema, nanukuu "Hilo la Aggrey Mwanri si sahihi, Mwanri hakukataliwa na wananchi kwa kuwa hana uwezo, alikataliwa kwa kuwa si Mmasai.... Na uchaguzi pale Siha ulitawaliwa na siasa za kikabila na kuchochewa zaidi na Nguvu ya Lowassa na uKaskazini."

Niliposoma maelezo haya nikadhani Justin amepitiwa, maana najua ni msomi mzuri wa sheria na anafahamu athari ya ubaguzi. Lakini katika hali ya kushangaza Justin akaendelea kusema:

"Mwanri ni Mchaga na jimbo la Siha limekaliwa na Wamasai sana, ambao walimchagua Dr.Mollel kwa ajili ya umasai wake.... Hilo mbishe au mkubali huo ndio uhalisia"

Nilipoona hivi nikajua huyu jamaa amedhamiria kufanya ubaguzi na hajapitiwa kama nilivyodhani. Kwa hiyo nikamshauri kuwa aache siasa za ubaguzi maana sio nzuri lakini akaendelea kushikilia msimamo wake kuwa Dr.Molell alichaguliwa Siha sio kwa sababu ya uwezo wake bali kwa sababu ya kabila lake.

UKWELI KUHUSU DR.MOLELL NA USHINDI WAKE SIHA,

Taarifa zinazoenezwa na Justin kwamba Dr.Molell alishinda kwa sababu tu ni Mmasai si za kweli na tunaomba umma wa watanzania uzipuuze. Dr.Godwin Mollel alichaguliwa kwa uwezo wake baada ya wananchi wa Siha kumpima na kuona kwamba anafaa kuwaongoza.

Kuna msemo wa wazungu kwamba ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri. Bahati mbaya Justin Mushi anasema uongo lakini hana kumbukumbu.

Kwa kuwa vijana wengi wa CCM ni waongo lakini empty minded, Justin alishindwa hata kutafuta taarifa kidogo za Siha ambazo zingempa nakisi ya ukweli wa mambo. Sasa ngoja nimsaidie some facts zinazopingana na taarifa yake.

#FACT_NUMBER1
Jimbo la Siha lina kata 17, vijiji 60 na vitongoji 159, linakadiriwa kuwa na idadi ya wakazi 150,000 ambao kati yao wenye sifa za kupiga kura ni 55,000. Wachagga wanakadiriwa kuwa 70% ya wakazi wote, Wamassai 20% na makabila mengine chini ya 10%.

Sasa kama kweli kura zilipigwa kikabila kama asemavyo Justin Mushi kwanini Mwanri hakushinda wakati kabila lake lina watu wengi zaidi? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!

#FACT_NUMBER2
Katika Kata 17 za jimbo la Siha, kata 12 zinakaliwa na Wachagga, kata 3 Wamassai na kata mbili mchanganyiko wa makabila mbalimbali.

Wachagga wapo zaidi kata za Kashashi, Ivaeny, Kirua, Levishi, Nasai, Sanya juu, Diriri, Makiwaru, Songu, Ngare-nairobi, Nduneti, na Miti mirefu.

Wamasai wanapatikana zaidi kata za Karansi, Gararagua na Donyomurwa. Kata ya Ormelili ina mchanganyiko wa Wachagga, Wamasai na Wameru, na Kata ya Orkolili ina wachagga na Wameru.

Kwa mlinganyo huo hapo juu unawezaje kusema Mwanri ameshindwa kwa sababu ni Mchagga? Wachagga wana kata 12 zenye wapiga kura 35,000 Wamassai wana kata 3 zenye wapiga kura 12,000 na kata mbili zilizobaki ni makabila mchanganyiko.

Unahitaji degree nyingi za ujinga ili uweze kuamini kwamba Aggrey Mwanri alishindwa kwa sababu si mmasai, while kabila lake ndio lenye idadi kubwa ya wapiga kura. Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!

#FACT_NUMBER3
Kata ya Ormelili ambayo wakazi wake ni mchanganyiko wa makabila mbalimbali (wachagga wakiongoza kwa idadi) diwani wake ni Mmassai Bw.Noel Mollel. Ikiwa kweli kura zilipigwa kikabila ilikuaje Wachagga wa Ormelili wakamchagua Ndugu Mollel ambaye si kabila lao? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!

#FACT_NUMBER4
Kata ya Karasi ambayo inakaliwa na Wamassai kwa zaidi ya 99% diwani wake ni Mchagga Mhe.Urassa. Ikiwa kweli kura zilipigwa kikabila ilikuaje Wamassai wa Karasi wakamchagua Ndugu Urassa ambyae si kabila lao? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!

#FACT_NUMBER5
Kata ya Donyomuro ambayo wakazi wake ni Wamassai wa zaidi ya asilimia 95% diwani wake ni Mchagga Mhe. Nsonu Ndossi. Ikiwa kweli kura zilipigwa kikabila ilikuaje Wamassai wa Donyomuro wakamchagua Ndugu Ndossi ambaye si kabila lao? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!

#FACT_NUMBER6
Ilikuaje Dr.Mollel ashinde Ubunge halafu Wamassai wenzie washindwe udiwani? Maana kwa mujibu wa Justin Wamassai ndio wengi jimbo la Siha. Lakini cha ajabu kuna madiwani wawili tu ambao ni Wamassai (Noel Mollel, kata ya Ormelili CCM, na Zacharia Lukumay, kata ya Gararagua CHADEMA).

Sasa mbona hao Wamassai waliompa kura Dr.Mollel na kumfanya ashinde ubunge, hawakutoa kura kwa madiwani wenzao wamasai ili washinde? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!

#FACT_NUMBER7
Kampeni Manger wa Dr.Mollel alikuwa kamanda Imma Saro (Mchagga). Ikiwa kweli Dr.Mollel alichaguliwa na wamasai wenzie ilikuaje awe na kampemni manager asiye mmasai? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!

#FACT_NUMBER8
Timu ya ushindi ya Dr.Mollel iliongozwa na Imma Saro (Mchagga), Solomoni Mmary (Mchagga), Witness Witness Riwa (Mchagga), Suzan Natai (Mchagga), na Baltazar Mmary (Mchagga). Ikiwa kweli Dr.Mollel alichaguliwa kwa sababu tu ni Mmassai mbona kwenye timu ya ushindi hatuoni Mmassai hata mmoja?

Inawezekanaje wachagga kumnadi Mmasai kama aliyosema Justin yana ukweli? Hawa Wachagga si wangeenda kumuunga mkono mchaga mwenzao Aggrey Mwanri? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!

Kwa ujumla vijana jamii ya Justin Mushi wanafaa kukemewa na kupuuzwa kwa kiwango cha juu mno, maana wanataka kuligawa taifa kwa misingi ya ubaguzi. Leo ameanza na ukabila, kesho rangi, keshokutwa udini. Utasikia msimchague fulani kwa kuwa si wa dini yetu. Huu ni upuuzi wa kiwango cha Shahada ya juu ya Uzamivu (PhD). Ni aibu kwa kijana msomi kama huyu kuhubiri ukabila katika karne hii ya 21 na chama chake kisimkemee.

Waogopeni watu jamii ya Justin Mushi, na kiogopeni sana chama chake maana ni chama kinacholea ubaguzi. Ikiwa wanachama wa CCM ni watu wenye mawazo ya namna ya Justin Mushi tutegemee nini wakija kuwa viongozi wakubwa ndani ya chama chao? Kuchagua CCM ni kuchagua watu jamii ya Justin Mushi. Wababuzi, wadini, wakabila, waongo. Kataa CCM. Kataa Ubaguzi.

Tanzania ni yetu sote. Tushikamane kupinga ubaguzi wa aina yoyote.!

Malisa GJ.!


naunga mkono hoja.
 
Dah! Huyu jamaa (Malisa Godlisten) always hujenga hoja kwa facts tofauti na migulu baja ya pale mtaa wa Lumumba kama huyu mdogo wangu Justin Mushi ambaye huropoka bila hata kuwa na ushahidi.
 
Waogopeni watu jamii ya Justin Mushi, na kiogopeni sana chama chake maana ni chama kinacholea ubaguzi. Ikiwa wanachama wa CCM ni watu wenye mawazo ya namna ya Justin Mushi tutegemee nini wakija kuwa viongozi wakubwa ndani ya chama chao? Kuchagua CCM ni kuchagua watu jamii ya Justin Mushi. Wababuzi, wadini, wakabila, waongo. Kataa CCM. Kataa Ubaguzi.

Tanzania ni yetu sote. Tushikamane kupinga ubaguzi wa aina yoyote.!

By Malisa GJ,

Kwanza nikupongeze si kwa mtiririko mzuri bali kwa kubaisha upumbavu wa maCCM kutumia midomo kusema uvundo. Think Tank wao akina JK Nepi Marope wanajulikana kuwa ni failures huko mashuleni.

Hao akina Justin wamepandikizwa ujinga kuwa kauli zao zitaheshimika tu ili mradi zinanasibishwa na CCM.

Mimi ni mwalimu by profession, sociology na psychology yetu kwa sasa inategemea mtawala wa ikulu kama ni msanii watanzania wote tunakuwa wasanii, kama ni dikteta tutamsifu kuwa anatukomboa. Ni lile suala la ELIMU ELIMU ELIMU linatusumbua na linawasumbua hao makada wa CCM. Justin Mushi kumsifia kuwa anajielewa wala kujitambua unajivunjia heshima. Nakukumbusha serikali ya CCM imejaza maDR, maProf lakini elimu zao zimeleta tija gani? CCM toka JK wanaingiza MaDR Ikulu lakini pima hekima na busara ni bidhaa adhimu kwao.

Sioni kama maCCM na Upungufu wa Elimu vchwani mwao wana suluhisho la Tanzania iliyoendelea na kujiheshimu. Kuwepo kwao kunategemea Ubaguzi, fitina, wizi, neno sahihi ni UFISADI lakini ndiyo hivyo tena wana dola.
 
Mimi sio mchagga ila nimeishi sana Bomang'ombe (makao makuu ya wilaya ya Hai) na pia Moshi na naifahamu vizuri wilaya ya Siha ambayo kabla ya hapo ilikuwa wilaya moja ya Hai.

Asilimia kubwa ya maeneo uliyoyataja nayafahamu sana mkubwa. Huko sehemu za milimani usafiri wao mkubwa ni vigari fulani vya kifaransa aina Pijoti yana nguvu kwelikweli ya kupanda milima na kuvumilia barabara za mawe na mashimo!

Kwanza sehemu kubwa ya Siha inakaliwa na wachagga na makabila mengine kama hao wamasai na wameru na wengineo ni wachache sana.

Kwa taarifa tu kwa wasiofahamu ni kwamba, ardhi ktk mikoa ya kaskazini hususani Arusha na Kilimanjaro ni ishu na bidhaa adimu. Kila eneo ni la ukoo flani. Ni ngumu sana mtu utoke huku usukumani eti uende Kilimanjaro ukapate ardhi ya kuchungia ng'ombe zako!!

Ndiyo maana nashangaa kidogo hata hao wamasai kidogo walioko huko ambao asili yao ni ufugaji walipenyaje mkoa huo hata kupata ardhi!

Hongera kwa kutoa somo zuri kwa mtiririko murua unaoeleweka. Ni wazi kuwa hata kama mtu haijui Siha, kwa namna ulivyoshuka atakuelewa vizuri sana!!
 
majuzi ZNZ CUF waliitwa 'Hizbo' tena kwa mabango yakipita mbele ya jukwaa kuu na makofi na kushangiliwa sana! Hao ndio ccm ndugu, unatakiwa uwe na 'mshipa' wa kishetani tu ili uweze kuwakubali! Wao ndio wanaoeneza siasa chuki, uhasama, udini, ukabila na ubaya wote! Ikumbukwe hii ni kazi ya shetani sasa tunapoona inafanywa na binadamu tena wenye kuongoza ni HATARI MNO MNO!
 
sio sahihi kulilia uongozi kwa kutegemea ukabila, mfano mzuri ni lema ambaye amechaguliwa hata na wamasai wa pale mjini arusha, tuseme kwamba lema kachaguliwa na wachaga wa pale mjini wenye maduka na biashara nyingine...
 
Hizo zinazoitwa "facts" ni uongo mtupu. Hakuna uhalisia wowote ni uzushi wa kimaandishi tu.

Unajiita Ikulu kwetu,, Tutegemee nini kutoka kichwani mwako,.
Kama mtu unaeishi madongo kuinama halafu unajiita 'IKULU KWETU' sidhani kama uko sawa.
 
Malisa upo sahihi kabisa,wakaz wengi wa siha ni watu wanaopenda kutenda na wagumu kubadilika wanapoamua,Mwanri alikwishaharibu na hata 2010 alishinda kwasababu CHADEMA walikuwa na mgombea dhaifu eng Tuni,ninakumbuka hata Dr Mollel alipokuwa CCM bado alimsumbua jamaa kwenye kura za maoni.Jamaa alikuwa na ahad zisizotekelezeka na mbwembwe nyingi mfano alitumia udhaifu wa mtanguliz wake Makidara Mosi wa kutokutekeleza ahad na yeye akatumbukia kwenye mkumbo huo huo matokeo yake wananchi waliomchagua 2000 waliamin atawakomboa ikawa kinyume.Kwa kifupi aliikuta siha ni ngome ya CCM na ameifuta CCM Siha indicator nzuri ni kata ya ngarenairobi ambayo ilikuwa ngome yao kuu
 
Ukweli ni kwamba upepo mchafu wa cdm/ukawa ulioikumba kanda ya kaskazini ndo uliomwangusha jembe Mwanri. Hata JPM, Sendeka, Chambiri na wengineo walipigwa chini maeneo hayo. Upepo umepita, wanakaskazini ndo wanazinduka walikumbwa na upepo mchafu. Too late, wasubiri 2020 wajisahihishe. No way.
Sasa hapa ndio umeandika nini? Irrelevant to the topic kabisa.
 
Kama Magu atakuwa mtu wa haki katika uongozi wake, wabunge wa CCM watapungua sana uchaguzi ujao.
 
Sasa hapa ndio umeandika nini? Irrelevant to the topic kabisa.
Ngoja, nikutafunie. Nakubaliana na mada. Mwanri kaangushwa Siha si kwa sababu za ubaguzi bali upepo wa cdm/ukawa uliosababishwa na EL kujiunga cdm. Upepo huo mchafu ndo uliomwangusha Sendeka na wengine. Utakuwa umenielewa sasa.
 
Ngoja, nikutafunie. Nakubaliana na mada. Mwanri kaangushwa Siha si kwa sababu za ubaguzi bali upepo wa cdm/ukawa uliosababishwa na EL kujiunga cdm. Upepo huo mchafu ndo uliomwangusha Sendeka na wengine. Utakuwa umenielewa sasa.
Sawa nimekuelewa ila hebu niambie ni maendeleo yapi kwa mfano aliyoyafanya Mwanri kwa wananchi wa Siha yatakayowashawishi wamchague tena?
 
Back
Top Bottom