Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
Kwa muda mrefu yamekuwepo madai kwamba Chama cha Mapinduzi na wanachama wake wamekua mstari wa mbele kupandikiza mbegu za ubaguzi na kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini, ukanda, ukabila au rangi. Lakini CCM imekuwa ikipinga tuhuma hizo kwa nguvu zote na kuzielekeza kwa vyama vya upinzani.
Lakini ni CCM haohao waliosema CUF ni chama cha waislamu mwaka 2000 baada ya kuona CUF imepata nguvu kubwa Tanzania bara. Kwahiyo wakasema ni chama cha kiislamu kwa hiyo wakristo wasikichague.
Mwaka 2005 CCM wakaanza propaganda kwamba CHADEMA ni chama cha kaskazini tena cha wachagga kwa hiyo wasio wachagga wasikichague. Propaganda hizo zimeendelea kuenezwa hadi sasa na wanachama na viongozi mbalimbali wa CCM.
Kwenye uchaguzi mkuu uliopita mtoto wa Rais mmoja mstaafu aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba nchi hii haiwezi kuongozwa na watu wa kaskazini. Huu ulikuwa ubaguzi mbaya sana. Nikajiuliza kwani yeye ni nani hadi afikie kusema hivyo? Nikajiuliza tena kwani watu wa kaskazini sio watanzania? sio binadamu? Mbona wanabaguliwa kwenye nchi yao wenyewe?
Kijana huyo hakuambiwa aombe radhi wala hakukemewa. Kwa kuwa CCM imeendelea kulea wanachama wake wanaofanya ubaguzi, bila kuwachukulia hatua yoyote basi wimbi la siasa za ubaguzi limeonekana ni kitu cha kawaida ndani ya chama hicho.
Jana rafiki yangu mmoja aitwae Justin Mushi ambaye ni mwanachama, kada na kiongozi wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) ameamua kuonesha waziwazi siasa za ubaguzi bila kujali athari zake kwa jamii.
Akichangia mjadala niliouanzisha kuhusu wakuu wa mikoa walioshindwa kwenye ubunge Justin alisema, nanukuu "Hilo la Aggrey Mwanri si sahihi, Mwanri hakukataliwa na wananchi kwa kuwa hana uwezo, alikataliwa kwa kuwa si Mmasai.... Na uchaguzi pale Siha ulitawaliwa na siasa za kikabila na kuchochewa zaidi na Nguvu ya Lowassa na uKaskazini."
Niliposoma maelezo haya nikadhani Justin amepitiwa, maana najua ni msomi mzuri wa sheria na anafahamu athari ya ubaguzi. Lakini katika hali ya kushangaza Justin akaendelea kusema:
"Mwanri ni Mchaga na jimbo la Siha limekaliwa na Wamasai sana, ambao walimchagua Dr.Mollel kwa ajili ya umasai wake.... Hilo mbishe au mkubali huo ndio uhalisia"
Nilipoona hivi nikajua huyu jamaa amedhamiria kufanya ubaguzi na hajapitiwa kama nilivyodhani. Kwa hiyo nikamshauri kuwa aache siasa za ubaguzi maana sio nzuri lakini akaendelea kushikilia msimamo wake kuwa Dr.Molell alichaguliwa Siha sio kwa sababu ya uwezo wake bali kwa sababu ya kabila lake.
UKWELI KUHUSU DR.MOLELL NA USHINDI WAKE SIHA,
Taarifa zinazoenezwa na Justin kwamba Dr.Molell alishinda kwa sababu tu ni Mmasai si za kweli na tunaomba umma wa watanzania uzipuuze. Dr.Godwin Mollel alichaguliwa kwa uwezo wake baada ya wananchi wa Siha kumpima na kuona kwamba anafaa kuwaongoza.
Kuna msemo wa wazungu kwamba ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri. Bahati mbaya Justin Mushi anasema uongo lakini hana kumbukumbu.
Kwa kuwa vijana wengi wa CCM ni waongo lakini empty minded, Justin alishindwa hata kutafuta taarifa kidogo za Siha ambazo zingempa nakisi ya ukweli wa mambo. Sasa ngoja nimsaidie some facts zinazopingana na taarifa yake.
#FACT_NUMBER1
Jimbo la Siha lina kata 17, vijiji 60 na vitongoji 159, linakadiriwa kuwa na idadi ya wakazi 150,000 ambao kati yao wenye sifa za kupiga kura ni 55,000. Wachagga wanakadiriwa kuwa 70% ya wakazi wote, Wamassai 20% na makabila mengine chini ya 10%.
Sasa kama kweli kura zilipigwa kikabila kama asemavyo Justin Mushi kwanini Mwanri hakushinda wakati kabila lake lina watu wengi zaidi? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!
#FACT_NUMBER2
Katika Kata 17 za jimbo la Siha, kata 12 zinakaliwa na Wachagga, kata 3 Wamassai na kata mbili mchanganyiko wa makabila mbalimbali.
Wachagga wapo zaidi kata za Kashashi, Ivaeny, Kirua, Levishi, Nasai, Sanya juu, Diriri, Makiwaru, Songu, Ngare-nairobi, Nduneti, na Miti mirefu.
Wamasai wanapatikana zaidi kata za Karansi, Gararagua na Donyomurwa. Kata ya Ormelili ina mchanganyiko wa Wachagga, Wamasai na Wameru, na Kata ya Orkolili ina wachagga na Wameru.
Kwa mlinganyo huo hapo juu unawezaje kusema Mwanri ameshindwa kwa sababu ni Mchagga? Wachagga wana kata 12 zenye wapiga kura 35,000 Wamassai wana kata 3 zenye wapiga kura 12,000 na kata mbili zilizobaki ni makabila mchanganyiko.
Unahitaji degree nyingi za ujinga ili uweze kuamini kwamba Aggrey Mwanri alishindwa kwa sababu si mmasai, while kabila lake ndio lenye idadi kubwa ya wapiga kura. Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!
#FACT_NUMBER3
Kata ya Ormelili ambayo wakazi wake ni mchanganyiko wa makabila mbalimbali (wachagga wakiongoza kwa idadi) diwani wake ni Mmassai Bw.Noel Mollel. Ikiwa kweli kura zilipigwa kikabila ilikuaje Wachagga wa Ormelili wakamchagua Ndugu Mollel ambaye si kabila lao? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!
#FACT_NUMBER4
Kata ya Karasi ambayo inakaliwa na Wamassai kwa zaidi ya 99% diwani wake ni Mchagga Mhe.Urassa. Ikiwa kweli kura zilipigwa kikabila ilikuaje Wamassai wa Karasi wakamchagua Ndugu Urassa ambyae si kabila lao? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!
#FACT_NUMBER5
Kata ya Donyomuro ambayo wakazi wake ni Wamassai wa zaidi ya asilimia 95% diwani wake ni Mchagga Mhe. Nsonu Ndossi. Ikiwa kweli kura zilipigwa kikabila ilikuaje Wamassai wa Donyomuro wakamchagua Ndugu Ndossi ambaye si kabila lao? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!
#FACT_NUMBER6
Ilikuaje Dr.Mollel ashinde Ubunge halafu Wamassai wenzie washindwe udiwani? Maana kwa mujibu wa Justin Wamassai ndio wengi jimbo la Siha. Lakini cha ajabu kuna madiwani wawili tu ambao ni Wamassai (Noel Mollel, kata ya Ormelili CCM, na Zacharia Lukumay, kata ya Gararagua CHADEMA).
Sasa mbona hao Wamassai waliompa kura Dr.Mollel na kumfanya ashinde ubunge, hawakutoa kura kwa madiwani wenzao wamasai ili washinde? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!
#FACT_NUMBER7
Kampeni Manger wa Dr.Mollel alikuwa kamanda Imma Saro (Mchagga). Ikiwa kweli Dr.Mollel alichaguliwa na wamasai wenzie ilikuaje awe na kampemni manager asiye mmasai? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!
#FACT_NUMBER8
Timu ya ushindi ya Dr.Mollel iliongozwa na Imma Saro (Mchagga), Solomoni Mmary (Mchagga), Witness Witness Riwa (Mchagga), Suzan Natai (Mchagga), na Baltazar Mmary (Mchagga). Ikiwa kweli Dr.Mollel alichaguliwa kwa sababu tu ni Mmassai mbona kwenye timu ya ushindi hatuoni Mmassai hata mmoja?
Inawezekanaje wachagga kumnadi Mmasai kama aliyosema Justin yana ukweli? Hawa Wachagga si wangeenda kumuunga mkono mchaga mwenzao Aggrey Mwanri? Ukiwa mwongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri.!
Kwa ujumla vijana jamii ya Justin Mushi wanafaa kukemewa na kupuuzwa kwa kiwango cha juu mno, maana wanataka kuligawa taifa kwa misingi ya ubaguzi. Leo ameanza na ukabila, kesho rangi, keshokutwa udini. Utasikia msimchague fulani kwa kuwa si wa dini yetu. Huu ni upuuzi wa kiwango cha Shahada ya juu ya Uzamivu (PhD). Ni aibu kwa kijana msomi kama huyu kuhubiri ukabila katika karne hii ya 21 na chama chake kisimkemee.
Waogopeni watu jamii ya Justin Mushi, na kiogopeni sana chama chake maana ni chama kinacholea ubaguzi. Ikiwa wanachama wa CCM ni watu wenye mawazo ya namna ya Justin Mushi tutegemee nini wakija kuwa viongozi wakubwa ndani ya chama chao? Kuchagua CCM ni kuchagua watu jamii ya Justin Mushi. Wababuzi, wadini, wakabila, waongo. Kataa CCM. Kataa Ubaguzi.
Tanzania ni yetu sote. Tushikamane kupinga ubaguzi wa aina yoyote.!
By Malisa GJ,