Kataa kua mjinga

Kataa kua mjinga

Mnandi Jr

Member
Joined
May 30, 2026
Posts
62
Reaction score
91
Nawasalimu wote. Habari ya wakati huu?!. Moja kwa moja kwenye mada.

Ujinga sio tusi, bali ni hali anayoweza kuwa nayo mtu yeyote, wakati wowote.

Ukiambiwa wewe ni mjinga usilaumu kua umetukanwa bali jitafakari.

Mohamed Dewji (Mo) aliwahi kusema "unaweza kua mjinga kwa kufikiri ujinga." kwahiyo basi kwakua sio muda wote utafikiri mambo chanya (fact), unaweza kujikuta umekua mjinga kwa wakati fulani.

Mwanazuoni mmoja aliwahi kumtafsiri mjinga kwamba "ni yule anaejua ukweli, anauzungumza ukweli, lakini anadumu kuishi kwenye uongo.

Nafikiri kwa tafsiri hizi umeanza kujua ni kiasi gani umewahi kua mjinga.

Unajua ujinga utakufanya udharaulike! Ukisikia kwamba wazungu wanatuzarau ni kwababu ya ujinga. Ukisikia kwamba afrika ina utajiri wa raslimali lakini watu wake ni masikini ni kwasababu ya ujinga.

Ni ujinga ndio unafanya watawala wa afrika kuiba na kuficha pesa nyingi nje ya nchi, alafu wanakwenda huko kuomba mikopo na misaada.

Kwenye mkutano wa G20 wa mwaka 2019 rais wa marekani Donard Trump alinukuliwa akisema "Unapofika wakati wa kujadili maswala ya afrika mimi hua natoka nje. Sina muda wa kupoteza kufikiri watu ambao wao wenyewe hawajifikirii!".
Yote haya ni kwasababu ya ujinga.

Sijamaanisha kwamba waafrika ndio wajinga na wengine ni werevu, hasha! Kila mtu hua mjinga kwa wakati wake..

Kiufupi ni kwamba kuna adui mbaya unayeishi naye ingawa unampuuza ni ujinga. Kama unahisi wewe sio mjinga basi jitahidi kuuepuka..

Ujinga utakufanya upuuze uwezo wako ubaki kutegemea uwezo wa wengine.

Ujinga utakufanya usiamini fikra zako, usijiamini wewe, badala yake uishi kwa kushabikia fikra na utendaji wa wengine.

Ujinga utakujaza hofu au kiburi au jeuri na hatimaye utapoteza kabisa.

Ukikubali kua mjinga, ipo siku utawashukuru watu watakaokupa vile ambavyo tayari ni vyako..

Amani iwe juu yenu..
 
1000208159.jpg

Tupunguze kua serious maisha ni haya haya.
 
Back
Top Bottom