Kataa au kubali lakini ukweli ndiyo huu!

Kataa au kubali lakini ukweli ndiyo huu!

scramble

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
1,593
Reaction score
257
huwa sipendi kuzungumzia udini lakini lisilobudi hutendwa. nchi yetu imekua na mfumo wa vyama vingi toka 1992. ni miaka 20 sasa tukiwa katika mfumo wa vyama vingi. kinacho nisonnesha ni ukweli kwamba baadhi ya vyama vinaelemea kwenye ukanda, ukabila na udini. hali hii haitotufikisha popote. hali hii itaifanya CCM iendelee kutawala milele.

nizungumzie uchaguzi wa 2010 huku nikiuoanisha na ule wa 2015. katika uchaguzi wa 2010, ccm waliibuka washindi wakifuatiwa na chadema na cuf wakashika nafasi ya tatu. nccr walishika nafasi ya nne. mgombea wa ccm alikua Muislamu. mgombea wa chdm alikua Mkristu. mgombea wa cuf alikua Muislamu na yule wa nccr alikua Muislamu pia.

meseji chafu zilizoegemea kwenye udini ziliwasihi Wakristu kutumia fursa ya kuwepo kwa wagombea wengi Waislamu. Walitanabahisha kuwa kura za Waislamu zitagawanyika kwa wagombea Waislamu. vile mgombea Mkristu ni mmoja (Slaa), basi ni neema kwa Wakristu.

Meseji chafu nyingine zilisambazwa na Waislamu wakiwaomba wana cuf kumpa jk kura ili kumzuia Slaa kuchukua nchi! baadhi ya wana cuf licha ya kuichukia ccm, walimpa jk kura! baadhi ya wana ccm licha ya kuipenda ccm, walimpa slaa kura kwa misingi ya udini!

kule kigoma waliamua kuipa nccr kura nyingi kwa sababu mgombea wa nccr alikua mtoto wao wa kigoma! walipata wabunge 4!


ukubali ukatae huu ndiyo ukweli kuhusu uchaguzi wa 2010.


2015 mambo yatakuaje?

uwezekano wa ccm kumpitisha mgombea Mkristu ni mkubwa. kwa mbali nahisi mama asharose migiro na dkt salim wanaweza kuchukua fomu japo siyo Wakristu. Iwapo ccm watampitisha mgombea Mkristu, maaskofu na mapadri waliompigia Slaa debe 2010, wote watakua nyuma ya mgombea wa ccc. ikumbukwe kuwa kuna mikatba minono kati ya makanisa na serikali ya ccm. japo baadhi ya maaskofu waliipigia debe chadema, 2015 watakua upande wa ccm kama mgombea atakua Mkristu.

kwa upande wa chdm, nahisi mgombea atakua Mkristu. Zitto ajue kuwa Mtei hawezi kumpa uenyekiti au kumruhusu abebe bendera ya chdm 2015. bila shaka mgombea wa chdm atakua Mkristu. iwapo kama wagombea wa ccm na chdm watakua Wakristo pana uwezekano mkubwa kura za Wakristu zitagawanyika kwa wagombea ho wawili.

kwa upande wa cuf, wanaweza hubahatika kupata kura za Waislamu wengi kwa kuwepo mgombea Muislamu anaepambana na wagombea Wakristu wawili (ccm na chdm). hali hii inaweza kukirudisha cuf kwenye nafasi ya pili.

kutokana na maradhi ya ukanda, ukabila na udini yanayovitafuna cuf na chdm, ukiongezea migogoro na unafiki vilivyopo chdm, ccm ina nafasi nzuri kushinda 2015. ujenzi wa barabara, visima na shule vitatumiwa na ccm mwaka 2015. licha ya umaskini mkubwa tuliyonao Watanzania, propaganda za ccm zitatufanya tusahau umaskini tuliyonao.


nimeamua kueleza ukweli. naomba wachangiaji wajenge hoja siyo kuongea kama wapo kijiweni.
 
Ulikuwa wapi kufanya uchambuzi wako wa kitoto toka 2010? Habari ya mujini. Ni gesi jombaaaa
 
Ulikuwa wapi kufanya uchambuzi wako wa kitoto toka 2010? Habari ya mujini. Ni gesi jombaaaa


soma vizuri. nafanya tathmini ya 2010 kuelekea 2015. kama umezoea mabishano ya vijiweni kaa kimya! naomba great thinkers peke yake ndiyo wachangie.
 
kWELI KAMAND WANANCHI WANATAKA HAKI YAO YA UKWELI NAWAUNGA MKONO KUHUSU GASI MTWARA NA LINDI KOMAENI
GASI IBAKI HAPO.
 
soma vizuri. nafanya tathmini ya 2010 kuelekea 2015. kama umezoea mabishano ya vijiweni kaa kimya! naomba great thinkers peke yake ndiyo wachangie.

huu ni utafiti au utabiri ... habari hii ni fresh from kijiweni
 
gechi tu apa. ccm nchale cdm nchale cuf nchale
 
Mimi napita tu! ninachojua mimi kwa namna yoyote ile kama CCM watashinda basi watashinda kwa wizi!Na kwa hali ilivyo ninaamini mfumo wa uchaguzi utabdirishwa ili washinde kwa hila
 
Baada ya kusoma nimegundua mleta mada amelenga nini.Naona unaota mchana.Huna kingine zaidi ya udini
 
huu ni uchambuzi wenye mtazamo binafsi. hata hvy nakubaliana nawe kuwa udini umetawala sana miongoni mwa watanzania wengi. Kuhusu Cuf kushika nafasi ya pili naona itakuwa ndoto. hadi sasa hakuna mtu hasa mwenye mvuto wa kiuongozi na mwenye kukubalika. Labda kama Prof Lipumba angelikuwa ndio anagombea kwa mara ya kwanza.
 
Mimi napita tu! ninachojua mimi kwa namna yoyote ile kama CCM watashinda basi watashinda kwa wizi!Na kwa hali ilivyo ninaamini mfumo wa uchaguzi utabdirishwa ili washinde kwa hila

Hii ndio kawaida yao. Ni vyema wasifanye hivyo 2015. chamsingi tume ya uchaguzi izidishe uwazi na kuboresha misingi mizuri ya uchaguzi tofauti na hapo nikuivuruga nchi
 
Wengi watapinga, ila ukweli usiopingika kuwa tangu chama chetu kilipo ahidi mahakama ya kadhi kwenye ilani ya uchaguzi, swala la udini lilianza. Hatuna namna ya kurudisha nyuma mkanda huu, ila tunajua chama chetu ndicho kimetuua. Tuliendelea kuuhadaa umma kuwa yule mkuu wa wilaya kwenye uchaguzi mdogo, alivuliwa hijab wakati kwake ni mfuga nguruwe, hapo chama chetu kilikuza udini. Swala la wakuu wa mikoa kuwaweka wachungaji wa madhehebu mengine mahabusu eti kwa kosa la kuchinja, linazidi kuchochea udini. Mkuu hatuna jinsi, ngoma ya udini iko uwanjani, lazima tuicheze. 2015 kila mtu achague mgombea wa dini yake, mambo yakikataana, basi damu imwagike.
 
watafanya (watavuruga) na wengi wataona ni mabadiriko ya kawaida tu ila wenye akiri watajua ndio bye bye, subiri utaona utashuhudia hapo mapema 2014 kama sio mwisho wa 2013 picha itakavyokuwa
Hii ndio kawaida yao. Ni vyema wasifanye hivyo 2015. chamsingi tume ya uchaguzi izidishe uwazi na kuboresha misingi mizuri ya uchaguzi tofauti na hapo nikuivuruga nchi
 
soma vizuri. nafanya tathmini ya 2010 kuelekea 2015. kama umezoea mabishano ya vijiweni kaa kimya! naomba great thinkers peke yake ndiyo wachangie.

Kama great thinker ulitakiwa utambue kuwa mesegi zingine zilikuwa ni propaganda za CCM kuharibia vyama pinzani waonekane ni wadini ,mfano ni kitendo cha Tambwe Hiza kukiri kuwa CCM ni mfadhili wa masalia wa CDM ambao tumewaona wkisema wamekimbia udini na ukanda.Pia umegusia juujuu sana kiasi kwamba ukweli umeuacha kwa kutawaliwa na hisia binafsi.
 
Mara Mtei, oh Zitto. wewe kama si masalia basi ni wale wanaofadhili masalia kutoka Magamba party, huna hoja, shut up.
 
We jamaa katafute kazi ya kufanya, usije na propaganda za Ma-CCM ukatuaharibia siku.


kwa taarifa yako mimi siyo mwanachama wa ccm. nahitaji chama mbadala lkn vilivyopo vinanitia mashaka kwa kuelemea kweye udini ukanda na ukabila. soma vizuri thread yangu ili uielewe
 
Mara Mtei, oh Zitto, wewe kama si masalia ni wale waofadhili masalia kutoka Magamba party, huna hoja shut up.


inaelekea unajaribu kuziba jua kwa kiganja cha mkono. kuhusu uchaguzi wa 2010 ukweli ni huo niliyouandika. udini ulitawala sana. labda kama ulikua bado shule ya msingi hapo unaweza kuwa hukuyaona ninayo yasema
 
Scramble, JK ndiye aliyeasisi ubaguzi wa aina zote, kuanzia kwa S.A.S na wakati kampeni akitumia baadhi ya masheikh.
 
Ulikuwa wapi kufanya uchambuzi wako wa kitoto toka 2010? Habari ya mujini. Ni gesi jombaaaa

usiwe kama mlevi kama habari ya mjini gesi kale hiyo gesi, huyu jamaa ameamua kufunguka na kuacha uchama pembeni me binafsi naipenda chadema japo sina gani ya chadema naipenda Cuf Japo sina kadi ya Cuf lakini kinachonisikitisha me na huwa nafkria nakuona kuwa CCM itaendelea kushinda ni hiki alichokisema huyu jamaa, kiukweli kuiangalia Chadema bila hata darubini Unaona Ni chama kinachosimamia Udini(Ukristo) Ukanda Na Ukabila Nakipenda Chadema sikisemei mabaya bali nasema ukweli uliopo na hii ni mbaya sana CUF nao ivo vio ndo kinachowafanya wasishinde Unajua Watanzania Tunawaona wajinga lakin n watu wanaopima sana unaweza ukaona wanakushangilia sana lakini mwisho wa siku kura wanampa mwingne kama alivyoshangiliwa Wababa kwenye Epiq den kura hawajampgia ni vizuri Chadema iondoe taswira ya Udin/ukabila/ukanda na kiwe chama ambacho kipo kipo hakina muonekano wa hayo mambo, Na si kusema kwamba CCM ndo wanayasema haya no bali namna klvyo Chadema na Cuf CCm wanacho hicho kitu cha Udini lakin Wanakificha tena mpaka ukipekua sana lakini wa macho huoni mpaka utumie darubini.


Tusiweke ushabiki mbele tutumie akili zetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom