Kassim Majaliwa: Atamaliza, tutamuongezea miaka mitano mingine kwa utamaduni wa chama cha Mapinduzi

Mzee mbona Ana HARAKA ? KWANINI TUSISUBIRI AMALIZE na Pia Tusubiri UTARATIBU wa VIKAO vya CHAMA?
Chama kimeshamaliza 2025 upande wa Rais, bado wabunge na madiwani!! Muda huu chama kipo kwenye hesabu ya 2030!! Sasa wale wengine wao kutwa mahakamani na kutukana mitandaoni, wakipigwa 2025 na 2030 wanasema wameibiwa kura, wakati maandalizi ni 0!!
 
Majaliwa anataka Kutuambia Iwe isiwe lazima Samia awe Rais Wa Nchi Kwa Miaka 10 ijayo?

===========

Kassim Majaliwa: Nataka kuwahakikishia tena, Serikali yenu iko makini na maam yetu kwenye eneo hili anaendelea kutenda haki. Leo miezi sita tu, ana miaka mitano tutamjumlishia miaka mitano mingine, bado ana nafasi ya kufanya sana. Hii miaka mitano anayokwanda nayo, sasa hivi bado tunafahamishana fahamishana tu lazima kila mtu ajue filosofi ya mama ni nini!

Atamaliza, tutamuongezea miaka mitano mingine kwa utamaduni wa chama cha Mapinduzi, Mama Samia lazima apate kipindi chake kama marais waliotangulia.

View attachment 1954361
Ndo akazane kumpamba mama sasa
 
Huyu mwalimu hesabu zinampiga chenga, Samia hata akipata awamu mbili bado atakuwa rais kwa miaka 9 na miezi kadhaa.

Na kwa mwenendo wake huu wa kurudisha majambazi na wanamtandao wapiga dili serikalini, niwawashangaa 'wazalendo' wetu uchwara kama wataruhusu aendelee past 2025.
Wewe ndie mzalendo uchwala. Mama bado yupo sana mpaka 2030.

Tatizo la raisi Samia ni nini? Unampangiaje watu wakufanya nae kazi. Hebu kwendeni huko na hizo chuki zenu na unafiki wenu.
 
Naona Bwa. Kassim anataka kuwa waziri mkuu wa kwanza duniani kuwa madarakani kwa miaka 15...
 
Back
Top Bottom