GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,553
- 108,889
Alisema,
Je, Waumini wenzagu mliohudhuria Maombi (Ibada) leo sehemu zenu mbalimbali nanyi Makasisi (Mapadri) wenu nanyi ‘walivurugwa‘ kama huyu wangu leo au ni yeye tu? Na mpaka sasa sijajua ni kwani somo lake alilenga sana suala zima la Unafiki na Uchawi.
Na hapa naomba niseme tu ukweli wangu kuwa mimi GENTAMYCINE nilishindwa kabisa kuimaliza hiyo ibada na badala yake nilianza kununa na kutoka kabisa ndani ya Nyumba ya Bwana kwani niliona kama vile amenilenga mimi moja kwa moja kwakuwa hizo tabia zote (7) tajwa hapo juu ninazo kwa 100%.
Jumapili ijayo nikienda ibadani nikimkuta huyu kasisi (Padre) wa leo siingii kanisani napitiliza zangu baa tu kugambeka.
Halafu hawa viongozi wa dini sijui huwa wanatembelewa na Roho Mtakatifu wa aina gani kwani ahubiri yao huwa wanayaandaa vyema na wakiyasema huwa yanakulenga na kuuma mno.
1. Ukiona mtu anapenda kusalisali sana jua ana sifa zote za Unafiki na Uchawi uliotukuka.
2. Ukiona mtu anapenda kulitajataja jina la Mungu mara kwa mara jua ni Mnafiki na Mchawi
3. Ukiona mtu anapenda kujionyesha kuwa anasali sana jua ni Mnafiki na Mchawi
4. Ukiona mtu anajifanya Mnyenyekevu kuliko uhalisia jua ni Mnafiki na Mchawi
5. Ukiona mtu anazijua sana ratiba za ibada jua ni Mnafiki na Mchawi
6. Ukiona mtu analazimisha watu wajue kuwa anasali mno jua ni Mnafiki na Mchawi
7. Ukiona mtu anapenda sana kupiga picha Ibadani na analazimsha ziwe mtandaoni jua ni Mnafiki na Mchawi