Kasisi (Padre) wangu wa leo sijui 'kavurugwa' na nini hadi akaamua kujikita zaidi 'kimahubiri' na hili eneo pekee

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
36,533
Points
2,000

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
36,533 2,000
Alisema,

1. Ukiona mtu anapenda kusalisali sana jua ana sifa zote za Unafiki na Uchawi uliotukuka.
2. Ukiona mtu anapenda kulitajataja jina la Mungu mara kwa mara jua ni Mnafiki na Mchawi
3. Ukiona mtu anapenda kujionyesha kuwa anasali sana jua ni Mnafiki na Mchawi
4. Ukiona mtu anajifanya Mnyenyekevu kuliko uhalisia jua ni Mnafiki na Mchawi
5. Ukiona mtu anazijua sana ratiba za ibada jua ni Mnafiki na Mchawi
6. Ukiona mtu analazimisha watu wajue kuwa anasali mno jua ni Mnafiki na Mchawi
7. Ukiona mtu anapenda sana kupiga picha Ibadani na analazimsha ziwe mtandaoni jua ni Mnafiki na Mchawi

Je, Waumini wenzagu mliohudhuria Maombi (Ibada) leo sehemu zenu mbalimbali nanyi Makasisi (Mapadri) wenu nanyi ‘walivurugwa‘ kama huyu wangu leo au ni yeye tu? Na mpaka sasa sijajua ni kwani somo lake alilenga sana suala zima la Unafiki na Uchawi.

Na hapa naomba niseme tu ukweli wangu kuwa mimi GENTAMYCINE nilishindwa kabisa kuimaliza hiyo ibada na badala yake nilianza kununa na kutoka kabisa ndani ya Nyumba ya Bwana kwani niliona kama vile amenilenga mimi moja kwa moja kwakuwa hizo tabia zote (7) tajwa hapo juu ninazo kwa 100%.

Jumapili ijayo nikienda ibadani nikimkuta huyu kasisi (Padre) wa leo siingii kanisani napitiliza zangu baa tu kugambeka.

Halafu hawa viongozi wa dini sijui huwa wanatembelewa na Roho Mtakatifu wa aina gani kwani ahubiri yao huwa wanayaandaa vyema na wakiyasema huwa yanakulenga na kuuma mno.
 

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Messages
580
Points
1,000

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined May 3, 2018
580 1,000
Mi wangu alizungumzia sn sifa za mtu muoga. Alisema:-

1. Ukiona mtu anatisha tisha sn wenzake ujue ni muoga
2. Ukiona mtu anatembea na walinzi wengi na kulindwa sn ujue ni muoga
3. Ukiona mtu hataki kushindana na wenzake ujue ni muoga
4. Ukiona mtu hasafiri nje ya nchi ujue ni muoga
 

stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Messages
18,777
Points
2,000

stroke

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2012
18,777 2,000
Tumtafute bwana na ufalme wake na mengine yote tutazidishiwa, ( Mathew 6 :33)

Hivyo katika kumtafuta bwana, yote hayo ni muhimu, Kujua ratiba zote za ibada na kuzifuatilia.
 

Lamisa Danish

Member
Joined
Nov 17, 2019
Messages
72
Points
150

Lamisa Danish

Member
Joined Nov 17, 2019
72 150
Ulifanya vizuri sana kutoka mana hata mm pia ningetoka mana huwa Sipangiwi kanisa la kusali,na ukijaribu kunipangia ndio unaharibu kabisaa..
Kazi ya kasisi ni kuniombea tu ili nisiwe na kiburi ktk utumishi wangu wa kumtumikia bwana..mambo ya kunisema sema awapo madhabahuni anakosea sana..
Hii kazi ya kumtumikia bwana ni ngumu kweli kweli wakati saa zingine najiuliza kwann niligombea huu utumishi ila kwa vile nilibeep tu ikang'ang'ania huko huko basi tena sina jinsi
 

Forum statistics

Threads 1,390,268
Members 528,139
Posts 34,047,897
Top