KashKash Lete!! - Mazingaombwe ya Watawala Hayeshi Vituko...

KashKash Lete!! - Mazingaombwe ya Watawala Hayeshi Vituko...

avatar yako inajieleza ...
I wish ungekua una upeo Japo kidogo wa kutofautisha werepete na straight talks

Anyway, we need watu wa bandwagon kama wewe kutukumbusha idadi ya wapumbavu tulionao
 
Kuna wakati natamani kufunuwa vichwa vya Watz kungalia kama ubongo wetu nao ni mweusi kama rangi zetu...mambo yetu tofautu na dunia nyingine...
 
Gagnija..hivi Tanzania kuna nupumgufu wa ripoti? Mwishonwa siku tunaweza kujikuta tuna jumba la makumbusho ya ripoti mbalimbali
unasema kuhusu ripoti,njoo kwenye sera ,kuna jamaa UDSM anafanya phd kwenye thesis yake ni policimania syndrome .yaani tanzania ni nchi ya sera,kuna hadi sera ya nyuki wenzetu kenya wakitaka kuandaa sera wanampigia simu balozi wao hapa nchini na yeye anapiga simu wizara husika wanampatia hiyo sera husika wanachofanya wanakopi na kupesti na kuedit kwenye tanzania wanaweka kenya wansave then wanaprint,sera zote zipo hapa nchini soon tutasikia kuna sera ya kukoment mada JF,sera ya kujisaidia ,sera ya kukohoa ,sera ya kutembea nk
 
ili mazingaombwe yatuepuke lazima tuwe serious katika tunacho kitaraji yaani mabadiliko.

leo nimeona watu wa UKAWA na CCM wakipongezana kwenye mchezo wa mtani JEMBE haya ni mazingaombwe.

si kweli kwamba watu wengi wanaipenda CCM ila UKAWA kwa ujumla wao hawako tayari kuchukua dola.

mtu makini anajua jinsi ya kucheza turufu yake, anajua makundi yote na mahitaji yao

Kenya kuna kundi dogo lakini ni muhimu sana linapokuja swala la kura za maamuzi.

Wajanja wanalitumia na kupata ushindi, je bado kwetu si ni mazingaombwe bado?
tukumbuke TURUFU iliyompa KIKWETE ushindi ni ipi UKAWA mpo hapo?
 
well.. how about that?
Kama zezeta niliamini yalompata Sitta basi; kumbe ndiyo mazingaombwe yalikuwa yanakolezwa, sijui tumechanga nini hadi kichwa kikaungana tena na kiwiliwili...jamani! tunachoshindwa kujiuliza ni je hicho kichwa ni kile kile? Je kiwiliwili nacho ni kile kile? Nakumbuka kichwa cha Sitta kilivyokipakata kiwiliwili cha Mwakyembe hadi hospitalini India! Je leo yawezekana kichwa cha Mwakyembe kimechukua kiwiliwili cha Sitta? Tatizo moja la mazingaombwe, kama alivyosema Mzee Mwanakijiji, ni kwamba unachokiona si lazima kiwe kinachotendeka. Leo nitalala ndani ya kabati kangu la nguo kwani sijui mtikisiko (tetemeko?) litakuwa kubwa na lenye athari kiasi gani...kweli ujanja kupata na katu si kuwahi...!
 
Last edited by a moderator:
Pittsburgh_Magician_David_Lawrence.jpg


Mazingaombwe ni sanaa; ni fani ya sanaa. Mazingaombwe pia hutumia ujuzi wa sayansi kufanikisha lengo lake - kufanya watu waamini kisichokuwepo kipo na ambacho kipo hakipo. Sanaa hii hujulikana kama 'wepesi wa mikono' yaani 'sleight of the hand'. Inaaminika kisayansi kuwa macho ya mwanadamu hayana uwezo wa kuona mambo mengi kwa wakati mmoja na hivyo mtu anaweza kabisa kupotosha macho kwa kuyafanya yaelekee kwingine - misdirection.

Zamani niliwahi kuchezesha mazingaombwe ya awali kabisa na hivyo naandika kutokana na ujuzi wangu. Itoshe tu kusema kuwa wapo watu wanaoamini mazingaombwe kabisa tena wengine wanaamini kuwa kuna kutumia 'ndumba' au 'uchawi' fulani. Ukweli ni kuwa mazingaombwe ni sanaa inayoandana na mazoezi ya muda mrefu, vifaa na mbwembwe - wanamazingaombwe wote duniani ni lazima wawe watu wa mbwembwe nyingine kwani hivyo ndivyo wanavyofanya ile 'misdirection'.

Watawala wa Tanzania wanapenda sana mazingaombwe. Wanapenda kuwaonesha Watanzania mazingaombwe mbalimbali kiasi wapo wenye kufurahia na kuamini kabisa. Wengine hawachoki kushuhudia mazingaombwe; tena wengine huyalilia kabisa! "tuoneshe tuoneshe" wanasema. Na wakifanyiwa mazingaombwe hawachelewi kusema 'duh ile ilikuwa bab kubwa'!

Kwa vile najua mazingaombwe sijali sana kama ni mazuri au la. Lakini linapokuja suala la utu na maisha ya watu; sipendi kabisa mazingaombwe. Kwani maisha ya watu huwezi kuyarudisha. Mazingaombwe ya kawaida mtu ataonekana anakatwa vipande na baadaye anaunganishwa tena; kwenye mazingaombwe ya wanasiasa madhara ya michezo yao wakati mwingine ni ya kudumu kwa vizazi!

Sipendi watawala wanaopenda mazingaombwe; wanaochezesha mazingaombwe na ambao hawakosi 'tricks' mpya. Na sipendi raia waonekane wanafurahia mazingaombwe kana kwamba ni kitu halisi.

Tetesi za mazingaombwe zimesikika; na tunaweza kushuhudia bonge la trick. Si lolote, ni sehemu ya mazingaombwe yale yale kama tuliyoyaona nyuma. Yanaweza kuambatana na maneno mengi ya kutupumbaza (misdirection).

Watatoka hawa; wataingia hawa!

Kashkash lete...!!
Sema ndumba, sema nangae!

MMM
Kile unchodhania umekiona wanataka tuamini hatukukiona na kile ambacho macho yetu yameshuhudia wanatuambia "si kweli".
 
Back
Top Bottom