Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,251
- 44,586
Mazingaombwe ni sanaa; ni fani ya sanaa. Mazingaombwe pia hutumia ujuzi wa sayansi kufanikisha lengo lake - kufanya watu waamini kisichokuwepo kipo na ambacho kipo hakipo. Sanaa hii hujulikana kama 'wepesi wa mikono' yaani 'sleight of the hand'. Inaaminika kisayansi kuwa macho ya mwanadamu hayana uwezo wa kuona mambo mengi kwa wakati mmoja na hivyo mtu anaweza kabisa kupotosha macho kwa kuyafanya yaelekee kwingine - misdirection.
Zamani niliwahi kuchezesha mazingaombwe ya awali kabisa na hivyo naandika kutokana na ujuzi wangu. Itoshe tu kusema kuwa wapo watu wanaoamini mazingaombwe kabisa tena wengine wanaamini kuwa kuna kutumia 'ndumba' au 'uchawi' fulani. Ukweli ni kuwa mazingaombwe ni sanaa inayoandana na mazoezi ya muda mrefu, vifaa na mbwembwe - wanamazingaombwe wote duniani ni lazima wawe watu wa mbwembwe nyingine kwani hivyo ndivyo wanavyofanya ile 'misdirection'.
Watawala wa Tanzania wanapenda sana mazingaombwe. Wanapenda kuwaonesha Watanzania mazingaombwe mbalimbali kiasi wapo wenye kufurahia na kuamini kabisa. Wengine hawachoki kushuhudia mazingaombwe; tena wengine huyalilia kabisa! "tuoneshe tuoneshe" wanasema. Na wakifanyiwa mazingaombwe hawachelewi kusema 'duh ile ilikuwa bab kubwa'!
Kwa vile najua mazingaombwe sijali sana kama ni mazuri au la. Lakini linapokuja suala la utu na maisha ya watu; sipendi kabisa mazingaombwe. Kwani maisha ya watu huwezi kuyarudisha. Mazingaombwe ya kawaida mtu ataonekana anakatwa vipande na baadaye anaunganishwa tena; kwenye mazingaombwe ya wanasiasa madhara ya michezo yao wakati mwingine ni ya kudumu kwa vizazi!
Sipendi watawala wanaopenda mazingaombwe; wanaochezesha mazingaombwe na ambao hawakosi 'tricks' mpya. Na sipendi raia waonekane wanafurahia mazingaombwe kana kwamba ni kitu halisi.
Tetesi za mazingaombwe zimesikika; na tunaweza kushuhudia bonge la trick. Si lolote, ni sehemu ya mazingaombwe yale yale kama tuliyoyaona nyuma. Yanaweza kuambatana na maneno mengi ya kutupumbaza (misdirection).
Watatoka hawa; wataingia hawa!
Kashkash lete...!!
Sema ndumba, sema nangae!
MMM