Kashfa ya Uzinzi: Lissu amsafisha Mbowe

Kashfa ya Uzinzi: Lissu amsafisha Mbowe

Status
Not open for further replies.
nawewe unajiita great thinker miongon mwa great thinkers? hivi great thinker unawaza mtu binafsi tena kwa mambo binafsi, badalala ya maswala nyeti ya kitaifa? ebu tujiulize, huo unaouita uzinzi wa mbowe, umesababishaje umasikin wa watanzania? umesababishaje elimu duni kwa watz? ndo unaomaliza tembo wetu na raslimali nyinginezo? ndo unasababisha garama za umeme kupanda kila uchao? jaman watanzania, tunaacha maswala ya msingi tunadeal na vitu ambavyo havitusaidii hata kidogo! tukianza kuangaliana haya maswala nani atasimama? wewe hapo hujawai kuzin? nakwambia tukianza kusema hakuna atakayepona, wachungaji, maaskofu mawazir wetu, rais, haponi mtu nakwambia! tuachane na mambo haya tuzungumze maendeleo yetu na vikwazo vyake!
 
Mbowe N Public Figure Hatakiw Kuwa Mzinzi Tena Aache. Amuulze Sakozii Ilkuaje
 
wewe ndio unajua mambo binafsi ni mwanvuli wa kumkinga bwana wenu clinton alipata kashfa ya kutembea na sekretari wake kulingana na hadhi yake aliponea chupuchupu ang'olewe kiongozi ni kioo aijalishi kafanya nini nje ya ofisi,kukatisha ziara ya mbunge kiwa ziara ya kazi na kumwita wajumuike kwa jambo binafsi ni sawa?
 
nchi haiwezi kwenda kwa wahuni je mbowe akiwa waziri mkuu atawagongaje

Kabla hujaoa Uzinzi ndio hutangulia
..
Sasa mkuu wa kaya kamega wangapi?
Acha watoto wa 2 aliowaacha Masasi..
Vpi Kapuya na kesi ya Kubaka? Mbona humnyooshei kidole? Vp issue ya Nape kule Geraffe hotel?
 

Ojuku Abraham na Jelard Lucas


KATIKA kile kinachoonekana kama kumsafisha Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe dhidi ya kashfa ya uzinzi inayomuandama.

Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tindu Lissu amesema suala hilo ni maisha binafsi ya mtu, ambayo hayawezi kuhusishwa na wadhifa wake kwa namna yoyote.


Akizungumza katika mahojiano maalum ndani ya chumba cha habari cha Global Publishers Ltd, Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam juzi, Lissu alisema kwa kadiri anavyofahamu, suala hilo ni binafsi linalopaswa kuachwa chumbani, kwa sababu kama litahusishwa na nafasi yake, ni sawa na kukubali kuwa mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini si lolote wala chochote.

“Maisha ya kimapenzi ya mzee Mandela yalikuwa ya ukakasi, kwa maana hiyo unataka tuseme kuwa kwa sababu hiyo, mzee huyu hakuwa kiongozi bora, unataka tuseme Bill Clinton wa Marekani hakuwa kiongozi bora kwa sababu tu alipata kashfa katika moja ya makorido ya Ikulu ya White House? Mimi nadhani haya mambo kama yapo au hayapo, hayahusiani na uwezo wa mtu kiuongozi, ni mambo ya chumbani yanayopaswa kuachwa huko,” alisema Lissu.


Lissu alikuwa akirejea baadhi ya sababu zilizosababisha mgogoro kati ya chama chake na Naibu Katibu Mkuu wao aliyetimuliwa, Zitto Kabwe, anayedaiwa kushiriki kuandaa waraka wenye nia ovu, ambao pamoja na mambo mengine, ulitaka kufanyika kwa mabadiliko ya viongozi wa juu, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, kwa kudaiwa kuwa na elimu ndogo pamoja na kukosa uaminifu katika ndoa yake.

Aidha, hivi karibuni wakati wa kikao kilichomalizika cha Bunge mjini Dodoma, Freeman Mbowe alidaiwa kuvuruga ziara ya mbunge mmoja mwanamke (wa viti maalum) wa chama chake aliyekuwa katika ziara ya kibunge nje ya nchi, na badala yake kumtaka kuungana sehemu alipokuwepo.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki, licha ya kukiri kuwepo kwa mgogoro unaokitikisa chama chao, lakini alisema hatimaye Chadema itashinda na kubakia imara na akasisitiza kuwa mwavuli wa mahakama alionao Zito ukiondoka, watamtimua.


Chanzo: LISSU AMSAFISHA MBOWE - Global Publishers


Hee! Kumbe si shituma bali ni kweli?
 
Awe Nape Mbowe Kapuya Na Yule Mzee Wa Bariadi Hatutak Uzinz Waache 2kiwapa Nch Ndo Watakua Wanakwenda Kupmzka Na Mabint Washngton Na Pesa Za Wavuj Jasho Huu N Ujinga,
 
Jamani tafadhli sana kama tunajadili tabia ya viongozi kujihusisha na uzinzi basi viongozi WA chichiemu hatapona mtu, kuanzia balozi WA shina hadi taifa. kwa hiyo fungeni midomo
 
Anayemtetea mzinzi aliyetekeleza familia yake nami namuona ni mzinzi hivohivo.
 
Viongozi wa CHADEMA ni majanga tupu.

Kwa hiyo kumbe Mh. Mbowe ni mzinzi kwa maana nyingine, tuhuma hizi ni za kweli.

Sasa kama maswala ya Uzinzi ni private affairs. Vipi hili swala la kupewa millions pesa za Tanzania na wale wale kila mara alikuwa akipanda kwenye majukwaa alikuwa anawaita mafisadi.

Pesa za huyu kada wa CCM alizochukua nazo ni private affairs

View attachment 132573

Tunaomba tufahamu mipaka ya private affairs nchini

Kama ameweza kuijibu hoja ya uzinzi, kwa nini hakutaka kuijibu hoja ya "double agent" kwa maana kuwa, mchana ni mpiga vita mafisadi na usiku ni mpokea pesa za mafisadi

Kama unashabikia sana hii ona na hii ya Mfanyakazi wa IKULU Sehemu ambayo Marehemu baba wa Taifa(R.I.P) alisema ni mahara PATAKATIFU.

[h=1]WEMA ANYANG'ANYWA KILA KITU NA KIGOGO WA IKULU, KISA KURUDIANA NA DIAMOND[/h]
ZILE tambo, mbwembwe na majigambo ya Miss Tanzania 2006/07, aliye pia msanii wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu, zimefika mwisho kufuatia kunyang’anywa samani za ofisi yake ya Endless Fame Film Production na aliyekuwa mpenzi wake, Clement ‘kigogo wa ikulu’ na sasa amebaki mweupe, Amani limepakuliwa ikiwa imeiva.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo la aibu lilijiri hivi karibuni kwenye ofisi hiyo ya Wema iliyopo Mwananyamala-Komakoma jijini Dar.

KIGOGO WA IKULU AVAMIA NA MABAUNSA
Habari za uhakika zinadai kuwa, siku ya tukio, Clement akiwa ameongozana na watu waliosadikiwa kuwa ni mabaunsa, walivamia ofisi hiyo aliyomfungulia mlimbwende huyo na kukomba vitu vyote vya thamani alivyomnunulia wakati wa mapenzi motomoto (hakuna lenye mwanzo lisilo na ncha).

KUMBE ALIKODI CANTER
Kama njiwa apelekaye ujumbe muhimu wa huba, mtoa taarifa huyo alizidi kumwaga ‘upupu’ kuwa, siku hiyo Clement mbali na gari lake la kifahari, pia alitinga akiwa na gari aina ya Canter ambapo bila maswali wala maelezo achilia mbali ufafanuzi, alikusanya vifaa vyote na kuvirundika kwenye gari.


IDADI YA VITU VILIVYOBEBWA
Vifaa hivyo ni tarakishi (computer), kamera ya kurekodi sinema (video camera), vifaa vya kurekebisha hali ya hewa (air conditioner), vifaa vya kuhifadhia umeme wa ziada, uninterruptible power supply (ups) pamoja na vifaa vingine zikiwemo nyaya za umeme na kuiacha ofisi nyeupe kama uwanja wa mpira.

“Hali ni mbaya sana, jamaa (Clement) alichukua kila kitu ndani ya ofisi hiyo kuanzia kompyuta, kamera hata nyaya! Hivi tunavyoongea, ofisi haina kitu kabisa,” kilisema ‘kikulacho’ hicho.

CHANZO NI DIAMOND
Mpashaji huyo alizidi kuyapa utulivu masikio ya mwandishi wetu kuwa, chanzo cha kigogo huyo kufanya ‘umafia’ huo ni kitendo cha Wema kurejesha penzi lake kwa ‘mtemea maiki’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.

Taarifa hizo zilieleza kuwa, kitendo hicho kilichochea hasira za Clement, hasa pale Diamond alipohojiwa kuhusu kuingilia penzi hilo na kujibu hamwogopi mtu, “ndiyo maana Clement akaamua kumwaga ugali baada ya wawili hao (Wema na Diamond) kumwaga mboga,” kiliongeza chanzo.

HEBU MSIKILIZE WEMA
Ili kujua yapi ni maziwa na lipi ni tui juu ‘niuz’ hizo, mwandishi wetu alimtafuta Wema na kukutana naye laivu juzi ambapo alikiri kukumbwa na zahama hiyo huku akionesha mshangao wa wazi kwa kitendo alichofanyiwa na ‘zilipendwa’ wake huyo.


“Ni kweli kabisa Clement amefanya hivyo, lakini nashangaa na ni mara yangu ya kwanza kuona wapenzi wakiachana mwanaume anaamua kuchukua vitu vyote alivyowahi kumnunulia au kumpa.
“Huo ni ushamba na unyanyasaji, akumbuke kwamba alipokuwa na mimi alinitumia pia,” alisema Wema na kuongeza:

“Hata hivyo, namshukuru Mungu, vitu vyote alivyochukuwa Clement, baby (Diamond) kasema ataninunulia, wiki mbili hazitapita.”
Wema alikwenda mblele zaidi kwa kuonesha machungu yake kwa kigogo huyo pale aliposema: “Kwanza nasikia vitu vyenyewe alipofika nyumbani kavimwaga nje maana ndani hakuna nafasi.”


KAANZA MWAKA VIBAYA
Mwanzoni mwa mwaka huu, Wema alikumbwa na mkasa wa kunyang’anywa lile gari la kifahari alilodai ni lake, Audi Q7 baada ya kusemekana kuwa halikuwa lake.
Kumbe gari hilo alipewa na Clement ambaye naye alilikopa kwa thamani ya shilingi milioni 90 kutoka kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Shadrack Tweve.

Tweve, baada ya kuzungushwa sana kulipwa fedha hizo, alikimbilia Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo hakimu aliamuru gari hilo likamatwe na kurejeshewa mlalalamikaji huyo.

PENZI LA WEMA, KIGOGO WA IKULU
Uhakika ni kwamba, penzi kati ya Wema na kigogo huyo halipo tena na kwa sasa jamaa ana demu mwingine (jina tunalo) ambapo mapaparazi wetu wanaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuwanasa katika mazingira yoyote yale.

 
Kama unashabikia sana hii ona na hii ya Mfanyakazi wa IKULU Sehemu ambayo Marehemu baba wa Taifa(R.I.P) alisema ni mahara PATAKATIFU.


WEMA ANYANG'ANYWA KILA KITU NA KIGOGO WA IKULU, KISA KURUDIANA NA DIAMOND
Hufahamu hata unachokiongea achilia mbali kile unachotakiwa kukijengea hoja.

Ulichoandika hakina mantiki yoyote na hoja iliyopo hapa. Are you BAVICHA?.
 
Kwa sababu ni mkataba baina ya mume, mke na jamii waliyopo.
Ndoa is public, ni mkataba unaotakiwa uwe published in public records.
There's always a public interest in any marriage .... a wedding can be private.

Ni public kwa mtazamo wako lakini kwa wengine ni individual, na ndio maana wengine ukimzingua tu anakimbilia sehemu nyngine tena kwa haraka pasipo kulegea. Cha muhimu ni kujitambua una wajibu gani kwa jamii inayokuzunguka na unaitimizia nini kwa wakati muafaka.Kwa jamii iliyo kubwa ni kuona maslahi yao yanatimizwa ili waishi vyema na wala siyo maisha yake ya ndani na familia yake. Tujikite katika utendaji na Maslahi ya Taifa Kwanza!
 
Kabla hujaoa Uzinzi ndio hutangulia
..
Sasa mkuu wa kaya kamega wangapi?
Acha watoto wa 2 aliowaacha Masasi..
Vpi Kapuya na kesi ya Kubaka? Mbona humnyooshei kidole? Vp issue ya Nape kule Geraffe hotel?

mbowe si ameoa mbona anaendeleza uzinzi?au jasiri haachi asili
 
Mbona unamzungumzia Lilian as if wewe ndo Mtei au mama mzazi? Kama unataka kupigwa kabang na unaona nafasi yako imezibwa si ufunguke? Mambo ya chumbani wewe umeyaona vp? Achana na mambo ya sirini utaabika.

Ntakuunga mkono ukiweka nada inayohusu kupanda kwa bei ya umeme na kukatika hovyo kwa nishati hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi.
 
Mh.mkono anajua bei ya mnadani kwa zitto na mbowe,sema mbowe amefanikiwa kuwa na watetezi wengi mapoyoyo kama lisu,lema,nasari ,na msigwa,otherwise wote wamekuwa wakinunulika kwa hao wanaowaita mafisadi.(wananunuliwa kwa njaa zao,halafu wanasingizia kivuli cha ccm)
 
Mi nasubiri Zitto aoe halafu 'tumchapie'! Lengo ajifunze, yeye si alimchapia marehemu Mpakanjia kwa Amina Chifupa?
 
Last edited by a moderator:
Lissu hakutakiwa kutoa kauli yoyote kuhusiana na mahusiano ya Mwenyekiti wake, amekosea mara mia mbili
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom