Kashfa ya Ufisadi Bandari ya Dar


Lakini Game kwani hayo ni maneno ya Mwanakijiji au ni maneno ya mnukuliwa (chanzo)? Au sijaelewa vizuri hiyo nukuu uliyoiwekea rangi nyekundu?
 
Kama huna la kusema kaa kimya....naona leo lazima utakuwa umekesha!! Mayn, yaani unafanyia ndalilo.....😀

Akheri mimi nakesha nyumbani kuliko wewe unayekesha kufunga vidonda vya walevi....ndio umetoka shift yako nini?
 
Akheri mimi nakesha nyumbani kuliko wewe unayekesha kufunga vidonda vya walevi....ndio umetoka shift yako nini?

Nyani Ngabu;

Hakika mnasikitisha sana, watu wazima kama ninyi kukashifiana hapa jamvini si vema, sisi wenzenu tunataka kujua kinachoendelea pale bandarini ninyi mnaleta mzaha, be carefull na yale mnayoyabandika hapa,

Nyani Ngabu; siku zote huwa naona kama michango yako imekwenda shule sasa pale unapoanza kutoa lugha chafu, mnaifanya forum hii ionekane kama likijiwe la wahuni furani.
 

Niwie radhi ndugu IsayaMwita.
 
Makontena kujaa pale bandarini ni ulaji wa hali ya juu wakuu wanajua na CCM wanapata mgao. Makontena yanayojaza yard ya bandari mengi ni yale ya transit ambayo huwezi kwenda kuyaweka kwenye yard ya nje ya bandari( amabayo hayakustahili kushushwa pale). Ila kwa kuwa haka kamchezo kanachezwa na wenye kampuni za meli, TICS na CCM ndo maana kameota mizizi. Dar Port sio transit port!!
Kwa kuwa kuna mizigo mingi ya ya kwenda ulaya, hasa madini toka DRC na Kahawa ya Burundi, meli zenye makontena ambayo yanakenda port zaidi ya Dar wanapunguza gharama kwa kuyashusha hapo Bandarini ili yaje yapakiwe na meli zingine yafikishwe kule yanakokwenda, then wao wanapakia mzigo ya kutoka DRC, Burundi na baadhi yetu sisi, kama Pamba, mbao, magogo nk. hivyo wanatengeneza kaela ka kueleweka kwa kuwa wanarudi na mzigo. Sasa hayo makontena kwa kuwa yanakuwa yanasubiri meli za kuyafikisha kule yanakokwenda, hayawezi kuondolewa pale yard Bandarini mpaka pale yatakapopata meli. Wakati huohuo wenye kampuni za meli wanakuwa wako tayari kulipa charge za kuyaweka pale hayo makontena na hii pesa wanayokula bila wasiawasi kwa kuwa haiko ndani ya mkataba.
Sasa meli zinazokuja zinakosa nafasi kwa kuwa kunakuwa hakuna mahali pa kuyapakulia, kwa lugha ingine yard inakuwa imejaa makontena ya transit.
 
Lawama inabidi pia ziende serikalini, kwa sababu hao waliotajwa hapo juu, mbali na udhaifu wao lakini pia nafikiri hawana hela za kununua cranes, hawana uwezo wa kujenga magati mengine, hawana uwezo wa kufuta mkataba wa TICTS, maamuzi mengi sana yamelazimishwa tu kutoka wizarani kwa manufaa binafsi ya mawaziri na watendaji wao, akina Mgawe mimi sometimes naona wanabeba lawama kwa sababu tu ni uso wa shirika, ni sawasawa na kumfokea fundi wa umeme wa TANESCO kwa umeme kukatika katika. Tutakuwa tunapeleka hasira zetu sehemu isiyostahili.
 
Lakini Game kwani hayo ni maneno ya Mwanakijiji au ni maneno ya mnukuliwa (chanzo)? Au sijaelewa vizuri hiyo nukuu uliyoiwekea rangi nyekundu?

NN - mimi hayo matatizo ya bandari sikuyajua kabla ya wiki mbili zilizopita. Sikuhitaji kwenda bandari ya Dar kujua matatizo hayo.

Hadi hivi sasa vyanzo vya ndani kabisa vinasema Dr. Dau ni front runner wa kwenda Bandari.
 
MKJJ .......Dr. Dau anakitaka hicho cheo au watu wanampendekeza...? !!!

Mwanakijj viulizwe vyanzo vyako kuwa kwani hakuna MTz mwingine anaeweza pewa nafasi hio akaimudu?...ktk List ya Viongozi wanaofaa ulionao hakuna anae wafaa ktk nafasi hio?

Ninaochohofia wana JF tunapoelekea ni kuwa wapambe wa baadhi ya Viongozi either kwa kujua au kutokujua.
 
Kati ya watanzania milioni 40 yaani Dau peke yake ndiye anayeweza kutatua THA?

acheni uhuni hapa.

mbona mnapenda kuleta issues zisizo husiana? why not anza na BODI NZIMA ya THA?


Halafu mbona chama kikuu cha upinzani kama CHADEMA na DR SLAA,ZITTO et al wako kimya kuhusu huu ufisadi au kwa sababu hii haiwapi sifa wanazozitaka?
 
GT huo ndo uwezo wa muungwana katika kupanga safu ya wasaidizi wake. kwa kweli hyu dk kawambwa simwelewi kabisaaaaaaa. jk anambeba kwa kuwa sijui ni ndugu au ndo mtandao ila jamaa umanager HAWEZI. halafu amempatia wizara muhimu na yenye masilahi makubwa kwa taifa kama reli, bandari, ndege, barabara nk.

nasikia magufuli mkulu alikuwa anamwonea donge sanaa wakati wa ben alivyokuwa anapawezea na kumwagiwa sifa na boss wake. adhabu alompa nikumpeleka kwenye VITOWEO ambako gafla jamaa amepatia kuna uhai kwa sasa.

jamani mapato ya bandari tuuu kwa faida tuliyo nayo kijiografia kazi ikafanyika kwa asilimia 75 yaani ufanisi itachangia ya 50 pasent ya pato la taifa. dar, tanga na mtwara zikifanya kazi kwa ufanisi huo.

huyu kawambwa ataweka uswahili hapooooooooooooo na mambo yatakuwa hivyoooooo basi twaendeleaaa kuumia.

ni dk wa namna gani hata decision level yake inakuwa chini namna hiyoooooooooooooooooooo. huenda nisisomee phd kama ndo hivyoooooooooo
 
Labda Dau anapendekezwa kwa sababu aliishafanya kazi THA miaka ya nyuma. Raphael Mollel anahusika vipi na hii ishu?
 
Nadhani bosI wa TRA angefaa zaidi kule THA na JK is seriuosly considering kumbadilisha on a flipside ni kweli Mataka naye anaitaka sana hiyo post
 
Nadhani bosI wa TRA angefaa zaidi kule THA na JK is seriuosly considering kumbadilisha on a flipside ni kweli Mataka naye anaitaka sana hiyo post

GT, unafikiri Dr. Dau hawezi kuimudu na kuirudisha katika nidhamu Bandari?
 
GT, unafikiri Dr. Dau hawezi kuimudu na kuirudisha katika nidhamu Bandari?


kwani tatizo la bandari ni nidhamu ya Meneja na bodi au?


pili Dau unayemzungumzia ni yupi,yule yule aliyekuwa ukisema kashindwa kazi NSSF? sasa kama alishafeli NSSF (kutokana na maelezo yako siku za nyuma)iweje apelekwe Bandari ambako tayari alishapita?

Pili kwa sababu tatizo la bandari kwa ukubwa linatokana na TRA huoni kama kuna mabadiliko ya kufanya basi yafanywe TRA?
 
CHADEMA mbona wamekuwa kimya sana kwenye hili sakata la bandari au hili halina political capital?
 
CHADEMA mbona wamekuwa kimya sana kwenye hili sakata la bandari au hili halina political capital?
Kuna TLP,CUF,NCCR Mageuzi etc,etc...Why just CHADEMA!!?May be wakawa hawana facts za kutosha kuhusu hili suala,je ungependa wajitwishe hivyohivyo??
 
Kuna TLP,CUF,NCCR Mageuzi etc,etc...Why just CHADEMA!!?May be wakawa hawana facts za kutosha kuhusu hili suala,je ungependa wajitwishe hivyohivyo??

CHADEMA kwa sabau ndicho cham pekee amabo kina credibility na uwezao wa kuongelea mambo yenye maslahi ya taifa...surely huwezi kukilinganisha na CUF,NCCR,TLP na wengineo

Hilo la kutokuwa na facts zishani kama linanguvu kwa sababu wanaye shadow minister wa hiyo wizara ya SHUKURU KAWAMBWA na hili suala la bandari ya Dar kuwa na huduma hafifu halikuanza kuongelewa leo wala jana na sidhani kama kila kitu lazima akiseme Dr Slaa

Unless CHADEMA hili hawana interest nalo na kama ikiwa wao hawaoni umuhimu nalo then tumekwisha maana sidhani kama Lipumba na maalim Sefu wana nia ya kuzungumzia mambo kama haya zaidi ya kutaka wapewe ruzuku wagombee tena urais mwakani
 

Katika suala la NSSF na vifo Tabora ulitetea uwezo mkubwa wa Dr. Dau kiutendaji. Nakupa wewe benefit of the doubt kwa sababu hata Rais inaonekana anaamini hivyo. Sasa kwa kadiri unavyomjua na kutokana na ukweli kwamba alishakuwa Bandari, unafikiri ni mtu ambaye anaweza kuleta uongozi unaohitajika sana (hii ni pamoja na kupata bodi mpya of course)?

Kama huoni yeye ana uwezo wa kuinua Bandari na kuwa ni bora aendelee kubakia NSSF unafikiri ni nani mwingine ambaye unaweza kumpendekeza kushika nafasi hiyo hasa kutokana na matatizo ya Bandari uliyoyaonesha? Ungempendekeza nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…