Kashfa ya makontena yamuibua Ridhiwan Kikwete!

Kashfa ya makontena yamuibua Ridhiwan Kikwete!

Unaweza kupumzika wakati unasumbuliwa
Kinachotakiwa ni mazingira mazuri ya kutoa ushahidi huo. Wale wafanyakazi wa TRA wana mengi ya kusema na ushahidi wanao. Haiwezekani makontena yakatoka bila amri. Niwakumbushe pia utaratibu wa maadili TRA unamtaka mtumishi kutekeleza amri ya mkubwa wake, sasa Masamaki angefanya nini kama kaamriwa hivyo. Haki itendeke na wote waliohusika wapelekwe mahakamani waombewe adhabu ya kifo na wasjifiche kwenye matamko wakati wafanyakazi wa TRA wasio na hatia wanasakamwa!
 
Naona wameanza kuruka na kukanyagana subiri wataalam waendelee kukata mizizi yenu yote mwshon mtabak na heka ya mananas na pensheni mlizani nchi haina wenyewe ngoja Mheshimiwa Rais kipenzi chetu John Pombe Joseph Magufuli na vijana wake wazalendo wawaonyeshe mamlaka ya Rais Mzalendo. ..Mkiskia kelele jueni jiwe limefka penyewe...asiwadanganye mtu bandarini..Airport..Boda/Customs na TRA ndio mizizi wa kila biashara sasa ikikatwa kwsha kazi
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI.
Ndugu zangu waandishi wa
habari, nimeamua kuwaita ili
kuzungumza nanyi kuhusu
baadhi ya mambo
yaliyokuwa yanasemwa
katika vyombo vya habari
kuhusu mimi.
Awali ya yote napenda
kusema kuwa habari hizo ni
UONGO mtupu, ni mambo
yanayozushwa na waandishi
wa habari hizo kwa nia ya
kuchafua jina langu kwa
sababu wanazozijua
wanaoandika. UKWELI ni
kwamba haya ni mambo
yenye kufanywa kwa nia na
dhamira mbaya dhidi yangu
na hata familia yangu.
Hivi karibuni, kwa mfano, lipo
gazeti moja liliandika na
kutoa picha yangu na mtu
mmoja waliyedai ni Mhe. Paul
Makonda eti akinifunga
kamba za viatu. Katika
maelezo yake mwandishi
akadai kuwa Mhe. Makonda
alipata uteuzi kuwa Mkuu wa
wilaya ya Kinondoni kwa
sababu hiyo. Huu ni uongo
usiokuwa na hata chembe ya
ukweli. Napenda watanzania
wajue kuwa hakuna wakati
wowote Baba yangu
alipokuwa Rais wa nchi yetu
alinihusisha kwa namna
yeyote ile katika uteuzi wa
mtu yeyote katika Serikali.
Hivyo basi kujaribu
kunihusisha na uteuzi wa
Mhe. Paul Makonda kuwa
Mkuu wa Wilaya wa
Kinondoni ni jambo
lisilokuwa na ukweli wowote.
Pili, Yule mtu anae onekana
katika ile picha siyo Mhe.
Paulo Makonda bali ni Bwana
Deogratius Kessy anayefanya
kazi katika kampuni ya
ushonaji na mavazi ya Bwana
Sheria Ngowi. Nilishona safari
suti kwenye kampuni hiyo.
Nilipokwenda kuchukua nguo
yangu na nilipovaa ili kuona
kama imeshonwa vizuri,
Bwana Sheria Ngowi alitaka
nivae viatu vya ngozi. Bahati
mbaya nilikuwa nimevaa
sandals hivyo akaamua
kunipa viatu vya dukani
kwake nivae. Wakati bwana
Deogratius Kessy akinisaidia
kuvaa viatu ndipo ile picha
ikapigwa nampiga picha wa
kampuni ya Bwana Sheria
Ngowi , inashangaza na
kusikitisha kuona picha hiyo
inatumiwa kupotosha ukweli
kwa kutoa maelezo ya
uongo. Ni dhahiri kwamba
mwandishi aliamua kufanya
hivyo kwa maksudi mazima
ya kutoa sifa mbaya kwangu
na kwa Mheshimiwa Paul
Makonda. Hivi ndivyo uhuru
wa habari unavyostahili
kutumika ?
Siku za nyuma gazeti lingine
liliandika eti kuwa nilihojiwa
kuhusu sakata la makontena
bandarini. Napenda
kuwaambia ndugu waandishi
wa habari kuwa sijawahi
kuhojiwa na mtu yeyote,
chombo chochote au kamati
yeyote kuhusu madai hayo.
Ni uongo usiokuwa na ukweli
wowote. Ni mambo ya
kugushi na uzushi kabisa,
Ninayasema maneno haya
kwa kujiamini na kama
mwandishi ana uthibitisho
wa madai yake autoe
hadharani watu wauone.
Aidha, nasema kama yupo
mtu aliyenihoji ajitokeze
kukanusha ninayoyasema,
Namtaka aseme wazi.
Nawahakikishia kuwa mtu
huyo hayupo na wala
hatakuwepo.
Ndugu waandishi na
watanzania wenzangu,
inaelekea kuna mtu au genge
la watu mahali Fulani ambao
wameamua na kudhamiria
kuchafua jina langu na la
familia yangu kwa kutumia
vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii. Tangu
Serikali ya awamu ya tano
ianze jitihada za kuwabana
watu wanaokwepa kulipa
kodi za Serikali bandarini
wapo watu wamekuwa
wakifanya jitihada za
kunihusisha na watu Fulani
wanaotuhumiwa kuhusika na
ukwepaji huo. Wapo baadhi
ya watu wamekuwa wakidai
eti baadhi ya makontena
hayo ni yangu. Na, wapo
waliodai eti kuwa nimekuwa
nawasaidia baadhi ya
wafanyabiashara hao
kukwepa kodi kwa kutoa
maagizo kwa maofisa wa
forodha wasiwatoze kodi
inayostahili kulipwa.
Napenda kuwafahamisha
kuwa sijawahi kuagiza bidhaa
zozote kutoka nje hivyo
sijawahi kuwa na kontena
lolote ambalo nililowahi
kutakiwa kulipia ushuru
nikakwepa. Aidha, sijawahi
kumuombea msamaha wa
kutokulipa au hata
kupunguziwa kodi
mfanyabiashara yeyote au
mtu yeyote aliyeingiza
kontena nchini kutoka nchi za
nje. Kama mtu ana ushahidi
autoe hadharani mimi niuone
na dunia iuone.
Nawahakikishia ushahidi huo
haupo na wala hautokuwepo.
Labda uwe wa kugushi na
wakifanya hivyo
wataumbuka.
Napenda pia kutumia nafasi
hii kusema kuwa sina na wala
sijawahi kumiliki lori au basi
wakati wowote katika maisha
yangu. Aidha, sina hisa au
ubia na mtu yeyote au
kampuni yeyote ya malori au
mabasi. Nayasema haya kwa
sababu wapo wabaya wangu
wanaoeneza maneno ya
kunihusisha na kumiliki
malori na mabasi. Pia
kunihusisha na baadhi ya
makampuni yanayomiliki na
kuendesha biashara ya malori
na mabasi.
Ndugu wanahabari, napenda
kusema kwa kurudia na
kusisitiza kuwa sina lori wala
basi hata moja na sina ubia
na wafanyabiashara ama
makampuni yoyote
yanayofanya shughuli hizo.
kama yupo mtu yeyote ana
ushahidi wa kuhusika
kwangu auweke hadharani
watu wauone. Napenda
ieleweke kuwa kama
ningekuwa na ubia wa
namna hiyo nisingekuwa na
sababu ya kuficha. Niogope
kitu gani ? Ukweli ni kwamba
sizuiliwi kufanya biashara
kama nikipenda kufanya
hivyo , Hata kwa nafasi yangu
ya sasa ya uongozi yaani
mbunge bado sina kizuizi.
Mbona Bungeni wapo
wafanyabiashara wakubwa
kwa wadogo. Isingekuwa
ajabu kwangu kufanya
biashara hivi sasa mimi
pamoja na kuwa mbunge ni
mwanasheria wa
kujitegemea na nimeiweka
katika TAMKO langu la mali na
mad
 
TAMKO langu la mali na
madeni la viongozi kwa
mujibu wa sheria ya maadili
ya viongozi.
Nimewavumilia sana lakini
sasa nimechoka, nimeona leo
nivunje ukimya. Nimeona
niseme kidogo kwani bila ya
kufanya hivyo nitaliacha
genge la watu wenye nia
mbaya na mimi waonekane
wanasema kweli. Wahenga
wanasema msema pweke
hushinda! Nikiendelea kukaa
kimya uongo wao utageuka
kuwa ukweli dhidi yangu.
Naambiwa hapa nchini siku
hizi kila jengo jipya
linalojengwa linasemekana ni
la Ridhiwani, kituo kipya cha
petrol ni cha Ridhiwan.
Nimeanza kuona athari za
uongo huo, Siku moja kuna
mtu alikuja kuniomba
nimpangishe katika lile jengo
la PSPF pale stesheni.
Nilipomuuliza
nitampangishaje akasema
mbona watu wamemwambia
ni jengo langu!? Siku nyingine
nikakutana na jamaa mmoja
mwenye asili ya kiasia akiwa
anahema. Akasema
ananiomba sana niache
kutaka kupora kampuni
yake,nikamuuliza kampuni
gani hiyo? Na kwanini
anasema hivyo? Akanijibu,
anasikia wakisema kampuni
yake ni ya ridhiwani wakati
kampuni hiyo hata yeye
kairithi kwa baba yake na
yeye alirithi kwa baba yake
zaidi ya miaka hamsini
iliyopita, Nikamwambia kuwa
habari hiyo si kweli, sina
mpango huo na wala sina
sababu ya kufanya hivyo.
Hayo ni maneno
yanayoenezwa na wabaya
wangu walioamua
kunipakazia kwa sababu
wazijuazo wao. Tukaachana
,sijui kama ameamini kama
sina mpango wa kumpora
kampuni yake. Siku moja
Mzee wangu mmoja wa
kwetu kijijini alinilalamikia
kuwa nina roho mbaya kwa
vile sitaki kumpa kazi
mwanae kwenye kampuni
yangu ya malori wakati yeye
ni dereva mzuri,
Nilipomueleza Yule mzee
kuwa sina lori hata moja
akashangaa na kusema
mbona watu wanasema nina
malori mengi. Ndugu zangu
mnaiona fitina kubwa
inavyotengenezwa katika
jamii kuhusu maneno haya,
Wapo wanaoniona mimi
FISADI, Wapo wanaoniana
mimi nina Roho mbaya,
Wapo wanao niona mie
nataka kupora mali zao.
Baada ya Baba kustaafu
maneno yamekuwa mengi
na yanazidi kupata kasi. kila
kukicha wanazua jambo
jipya. Nimeoa niyaseme haya
ili watu wajue ukweli wa
upande wangu.
Naomba nimalize kama
nilivyoanza kwamba
yanasemwa mengi lakini ni
maneno ya uzandiki, uzushi
na ni uongo mtupu usiokuwa
na chembe ya ukweli. Wale
wanaosema, kuandika, na
kueneza maneno hayo
wanajua kuwa wanasema
UONGO, ila wanafanya hivyo
kwa vile wana nia mbaya
dhidi yangu na familia yangu
, Naomba watanzania
muyapuuze maneno hayo,
naomba watanzania
wenzangu muupuuze uongo
huo.
siko hivyo, sina mali hizo na
wala sifanyi hayo wanayodai
nafanya na wala sina mpango
wa kuyafanya.

Imetolewa na:-
Ridhiwan J. Kikwete
Mbunge wa Jimbo la Chalinze.
 
Mhhhh!!!! Sidhani Kama Kwa Maelezo Hayo Tu, WATANZANIA Watakuwa Wametosheka Nayo!! NADHANI Ilikuwa Bora Angeweka Hadharani Mali Zake Anazomiliki, Kama Alivyowasilisha Ktk Hiyo Tume Ya Maadili!!! Lkn Kuishia KUKANUSHA Tu!!!! Mhhhh!!
 
Kelele za mlango zimeanza kumnyima usingizi mwenye nyumba lol.
 
Naona Jipu limeguswa kidogo!!!Na yule aliyesema tunawaonea wivu wao watakuwa matajiri Mpaka mwisho wa dunia sijui alikuwa wa familia yake!!!
Pole Ridhwani Kutesa kwa zamu.hii ni ya familia ya Magu na kambi yake poleni sana.
 
VP kampuni yake ya lugumi interprises? inalipa kodi stahiki katika jengo LA ATC house posts mpya?

Lake oil inalipa kodi stahiki? au itakuwa imeanza kulipa kodi baada ya magufuli kuingia ikulu...!!!

Malori yake yameanza kulipa kodi?

Magufuli mulika na biashara za Job Ndugai anatuhumiwa kumuua ofisa wa TRA Aliyekwenda kudai kodi ya serikali mwaka Fulani...na yeye amulikwe.


Mulika na malori ya Ngereja , MTU mmoja ana malori zaidi ya 100 anayalipia kodi stahiki?

Enhee !keki ya taifa kwelibado ipo kweli?au wameimaliza yote tulambe sahani tupu!
 
Tusubiri nadhani kubenea atatoa ushaidi au kuomba radhi ila namshauri mh aende mahakamani ili haki itendeke
 
Aya ndio aliyoandika kwenye TL yake leo. Mwenye ukweli kuhusu tuhuma za Ridhiwani ajitokeze ili tujue ukweli haswa ni upi.

Anaanza hivi

CXEQ7yuW8AEZubq.jpg


Juu ya hoja Makonda kupata U-DC

CXEVMV9UkAA863E.jpg


Juu ya hoja ya KUKWEPA KODI

CXEVMU5UkAE1WtD.jpg


Nini kilitokea Ofisini kwa Sheria Ngowi

CXEVMXJU0AAi-Zz.jpg


Juu ya UMILIKI NA UENDESHAJI WA MAKAMPUNI YA MALORI NA MABASI

CXEVbrfWEAAu_p1.jpg


Madhara ya maneno yanayosemwa

CXEVMnLUoAAbNnL.jpg


Juu ya habari kwamba ameitwa KUHOJIWA juu ya upotevu wa makontena

CXEWC4mWwAAblxS.jpg
 
Hizi hadithi hazina faida yeye atulie tuu, Magufuli atamfikia tu!
 
mheshimiwa Riz akutukanaye hakuchagulii tusi,zidisha maombi mungu atakusaidia na wabaya wako wote ipo cku wataaibika
 
Aya ndio aliyoandika kwenye TL yake leo. Mwenye ukweli kuhusu tuhuma za Ridhiwani ajitokeze ili tujue ukweli haswa ni upi.

Anaanza hivi

CXEQ7yuW8AEZubq.jpg


Juu ya hoja Makonda kupata U-DC

CXEVMV9UkAA863E.jpg


Juu ya hoja ya KUKWEPA KODI

CXEVMU5UkAE1WtD.jpg


Nini kilitokea Ofisini kwa Sheria Ngowi

CXEVMXJU0AAi-Zz.jpg


Juu ya UMILIKI NA UENDESHAJI WA MAKAMPUNI YA MALORI NA MABASI

CXEVbrfWEAAu_p1.jpg


Madhara ya maneno yanayosemwa

CXEVMnLUoAAbNnL.jpg


Juu ya habari kwamba ameitwa KUHOJIWA juu ya upotevu wa makontena

CXEWC4mWwAAblxS.jpg

Ni nani anayeweza kutoka hadharani na kukubali hayo?
 
Hata ningekuwa mimi ningekataa na kuandika bango lefu zaidi ya hili lake
 
Back
Top Bottom