Kashfa ya kigogo Ikulu yaibuka upya

Kashfa ya kigogo Ikulu yaibuka upya

Mh..! Yawezekena pengine kuna watu walijaribu kukwapua kwa njia hiyo na wakafanikiwa na ndio maana nao walipopata chance wakajaribu. By the way billion 3 kwa safari za raisi.? Ni safari ngapi hizo na za siku ngapi zinazogharimu fedha zote hizo.? Additionaly, wizi mwingine hauna hata akili na inadhihirisha how our leaders are not smart at all katika moves zao. Wewe uibe fedha nyingi kiasi hicho.? Inamaana hamna anayefanya auditing ya safari kuhakikisha kama safari ilifanyika ama laa.? Na vipi kuhushu chenji za safari huwa hazirudishwi.? Ni mengi ya kujiuliza lakini acha niishie hapo.
 
...nchi ya ajabu hii....wezi wakubwa wa mali za umma ambao ndio wanarudiasha nyuma maendeleo wanajulikana lakini hawachukuliwi hatua.....lakini wezi wadogo wanakamatwa..na hata kuteswa...Hizi njama za kukwapua bil.3 zilijulikana....je njama kama hizi na hatimaye wizi ni ngapi zinapita bila kugunduliwa???.....kama wanaojulikana hawakamatwi na kufungwa....Nchi ya wendawazimu hii....namkumbuka na kumlilia sana marehemu Sokoine...maana angekuwepo huu ujambazi mweupe usingekuwepo tz....Nchi ya manyang'au na mafisi hii......
 
Kwa haraka haraka safari za rais zipo kwenye ratiba maalum kwa kipindi cha mwaka wote mzima sasa hawa raia waliweza kuwahadaa vipi hazina inamaana hazina inatoa fedha bila ya kuwa na ratiba ya rais wa nchi?

Pili kama ripoti ipo kwa JK basi hakuna utekelezaji atasema ni upepo tu utapita basi swala linahishia hapo.

Tatu kumshusha mtu cheo na kumwamisha idara wakati ni mwizi huu ni utani katika uongozi na kulinda raslimali za taifa
 
Hivi kumbe ikulu ukiiba adhabu yake ni kushuswa cheo na kuhamishwa idara!
 
Tunaiba Pesa za WALIPA KODI... TUNAKOPA PESA HATUNA

Nafikiri wakati wa kulalama umekwisha naomba tuchukue hatu. Naamini kuna watu wengi mbadala wa hawa waliopo sasa serikalini. Niwaombe waTanzania wenzangu chondechonde tujiandikishe kwa wingi na tukapige kura kwa wingi tuweke serikali mpya madarakan wakati ukifika. naomba tuhamasishane popote tulipo Serikali Hii ya sasa umri wake umekwisha. Tutakufa kwa njaa na mateso.
tUSIKATISHWE TAMAA NA PROPAGANDA NDOGO ZA KIJINGA ETI cHADEMA NI MAGAIDI.
 
jamaa ameona inawezekana kuiba kwenye bajeti ya safari za JK kwa sababu anasafiri mara nyingi mno kuliko hata waziri wa mambo ya nje.
Safari moja inagharimu pesa yote iyo jamani??
 
duuuuuu kama alighushi 3 BILLION tena kwa safari kanjanja ina maana safariza ukweli huwa zinakula hadi 5 bln...mtumeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Ah!!! Mwizi anashushwa cheo au anahamishwa kitengo Duh!! hii ni Tanzania tuu.

KITAIFA
Na Patricia Kimelemeta, Mwananchi

Posted Jumanne,Marchi19 2013 saa 21:35 PM

KWA UFUPI

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.

Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.

Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.

Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.

Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.

“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.

Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

“Ila maofisa hawa walitumia mwanya huo kuihadaa Wizara ya Fedha kwa kuandaa hoja ya safari feki ili kupata fedha hizo,” aliongeza Mahadhi.

Maofisa wengine ni pamoja na ofisa katika Idara ya Itifaki, Shamim Khalfa, Kaimu Mhasibu Mkuu, Kasim Laizer, Mhasibu, Deltha Mafie na karani wa fedha) aitwaye, Shabani Kesi.

tanzania yenyewe ni maajabu saba ya ulimwengu!
 
KITAIFA
Na Patricia Kimelemeta, Mwananchi

Posted Jumanne,Marchi19 2013 saa 21:35 PM

KWA UFUPI

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.

Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.

Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.

Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.

Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.

¡°Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,¡± aliongeza Mahadhi.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.

Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

¡°Ila maofisa hawa walitumia mwanya huo kuihadaa Wizara ya Fedha kwa kuandaa hoja ya safari feki ili kupata fedha hizo,¡± aliongeza Mahadhi.

Maofisa wengine ni pamoja na ofisa katika Idara ya Itifaki, Shamim Khalfa, Kaimu Mhasibu Mkuu, Kasim Laizer, Mhasibu, Deltha Mafie na karani wa fedha) aitwaye, Shabani Kesi.

yani karibia idadi kubwa ya maafisa wote walio husika ni takbir na asalaam alyekhum.
Kwa mfano huu mdogo tu napata picha kujua Ikulu imejaa watu wa aina gani humo ndani. Mtoke hapo muandamane na kuweka makongamano kuwa hampewi fursa ya uongozi, wakati mnabebwa na mpaka mbeleko za chuma lakini wapi??
Jamani wakati mwingine muwe na chembe hata ya huruma kwenye nyoyo zenu kuhusu kodi zetu sisi wavuja jasho mitaani.
 
RAHISI wetu kweli ni Vasco da Gama,,,ana safari nyingi hadi anabambikiwa?

Sijui Sasa HIVI; FBI kuja BONGO? Kutambua SERIKALI MPYA ya KENYA? Alikuwa anapendwa WEST sasa HIVI BOOT CAMP
 
Back
Top Bottom