Kashfa ya kigogo Ikulu yaibuka upya

Kashfa ya kigogo Ikulu yaibuka upya

Sasa kama vibaka wamo nyumba moja na raisi na wanaiba akiwepo sasa huku kwingine sijui kama kuna senti imebaki
 
Inakuwa kama Trilion 1 na mil mia moja hivi
Hapo ni kuanzia mwaka 2005 hadi 2012.
Halafu sasa hapo chini ni hotuba ya bajeti ya 2012/13 iliposomwa na waziri wa fedha bugeni,hiki kipengele kinahusiana na mikopo ya serikali kutoka huko anakozunguka...

Mikopo ya Nje yenye Masharti ya Kibiashara

32. Mheshimiwa Spika, mwaka 2011/12 Serikali ilikadiria kukopa kiasi cha Dola za Marekani milioni 822, sawa na shilingi bilioni 1,271.6 kama mikopo ya kibiashara. Katika kipindi cha Julai 2011 hadi Aprili 2012, Serikali ilisaini Mkataba wa mkopo wa kiasi cha Dola za Marekani milioni 310 na Benki ya Standard ya Afrika Kusini. Hadi kufikia Aprili 2012, jumla ya Dola za Marekani milioni 229 ambazo zilitumika kulipia madeni ya barabara ya mwaka 2010/11. Aidha, Serikali ilisaini Mkataba wa mkopo wa Euro milioni 61 na Benki ya HSBC. Mkopo huu umeelekezwa kugharamia ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa megawati 60 Nyakato Mwanza. Serikali pia imesaini mkataba wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 350 kutoka Benki ya Credit Suisse ya Uingereza ambapo Dola za Marekani milioni 200 zimepokelewa mwanzoni mwa Mwezi Juni 2012. Kiasi kilichobaki cha Dola za Marekani milioni 150 kitapatikana na kutumika mwaka 2012/13.
Jiulize kama rais akitulia nyumbani kujenga nchi kama tunahitaji kukopa kopa.Mi nadhani safari zake zilikuwa na misukumo binafsi kama utalii nk.
Tuna hasara kweli kweli.
 
Duh.... jamaa wezi anaondani kwake anashindwa kuwachukulia hatua, je walionje .si Ndio hawaguswi....?
 
Kama inahusisha Wizara ya mambo ya Nje, basi hilo ni Dongo kwa Bernard Membe.

Naona Lowassa na yeye anaanza kurusha Makombora kuelekea kwa Membe Moja kwa moja.

Hili pia linamuweka vibaya Waziri wa Mambo ya nchi za nje.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
RAHISI wetu kweli ni Vasco da Gama,,,ana safari nyingi hadi anabambikiwa?
 
watu wanaghushi document kutaka kuiba bilioni 3 wanahamishwa vitengo wakati mwalim anaiba shs.milioni 1 anafungwa miaka 10. kila siku Rais anaimba nchi kuongozwa kwa sheria wakati anaficha majambazi nyumbani kwake ikulu.
hawachukuliwi hatua kwasababu hiyo ngoma ilikuwa igawiwe pasu kwa pasu...
 
NO. Something is not right.
Utaratibu na sheria gani ya mtu/watu kutaka kughushi na kujipatia Tsh 3 billion halafu adhabu anayopata/wanayopata ni kushushwa cheo au kubadilishwa idara. THIS IS THE JEST OF FOOLS.

Halafu cha kushangaza, huyu jamaa, Mahadhi, sijui naibu Waziri. Haoni hata soni mbele ya kusanyiko la waandishi wa habari kusema maneno ya kitoto na kijinga kama haya.

TAKUKURU IS JUST A BATCH OF JOKE. Kwani wanapowapeleka watu mahakamani kwa rushwa za kishenzi shenzi huwa lazima waombe idhini kutoka kwa Rais?. Wanashindwa hata kuutetea uongo wao.

Vyombo vyetu vya habari navyo ni madudu tupu. Hakuna chombo cha habari chochote kilichofuatilia sakata hili kwa mwaka mzima mpaka linaletwa tena na Mh. Lowassa

Thanks Lowassa hata kama una motive nyingine kisiasa.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hao wana-michezo yao ya kisiasa tu wala sio hela za watanzania! Nae Mh. Lowasa leo wamuulize hela zetu za Richmod alichukuliwa hatua gani na chama? hawezi kuwa na jibu, basi nae kwa hili afunike kombe mwanaharamu apite!
 
NO. Something is not right.
Utaratibu na sheria gani ya mtu/watu kutaka kughushi na kujipatia Tsh 3 billion halafu adhabu anayopata/wanayopata ni kushushwa cheo au kubadilishwa idara. THIS IS THE JEST OF FOOLS.

Halafu cha kushangaza, huyu jamaa, Mahadhi, sijui naibu Waziri. Haoni hata soni mbele ya kusanyiko la waandishi wa habari kusema maneno ya kitoto na kijinga kama haya.

TAKUKURU IS JUST A BATCH OF JOKE. Kwani wanapowapeleka watu mahakamani kwa rushwa za kishenzi shenzi huwa lazima waombe idhini kutoka kwa Rais?. Wanashindwa hata kuutetea uongo wao.

Vyombo vyetu vya habari navyo ni madudu tupu. Hakuna chombo cha habari chochote kilichofuatilia sakata hili kwa mwaka mzima mpaka linaletwa tena na Mh. Lowassa

Thanks Lowassa hata kama una motive nyingine kisiasa.

Red: Ndio panaondoa uzito wa hoja yoooooooote, Mh. Lowasa hana uchungu na nchi, yeye ndio mwenyekiti wa kikio cha mambo ya nje, hakuuliza ndani ya kikao, anauliza nje! kwanza Mh. Naibu Waziri kumjibu ni Bahati sana, mwingine asingemjibu, ila inaonekana lowasa anafanya siasa za uanaharakati.....Tanzanian Mbona wakati wati wa mijadala ya sera ya gasi Bungeni hakusema? leo anasema kuna haja ya kuwa na sera ya Gesi? waangalieni wanasiasa wetu
 
Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.

Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.

Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.

Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.

Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.

"Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo," aliongeza Mahadhi.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.

Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

"Ila maofisa hawa walitumia mwanya huo kuihadaa Wizara ya Fedha kwa kuandaa hoja ya safari feki ili kupata fedha hizo," aliongeza Mahadhi.

Maofisa wengine ni pamoja na ofisa katika Idara ya Itifaki, Shamim Khalfa, Kaimu Mhasibu Mkuu, Kasim Laizer, Mhasibu, Deltha Mafie na karani wa fedha) aitwaye, Shabani Kesi.

Hata hili halieleweki, wewe naona akili zako kuna mtu anazo kakushikia, mwambie akurudishie unadhalilika huku.

Soma vizuri habari uelewe kinachosemwa. Unaweza kujifanya una akili nyingi kumbe wewe ndio hujaelewa!!!
 
KITAIFA
Na Patricia Kimelemeta, Mwananchi

Posted Jumanne,Marchi19 2013 saa 21:35 PM

KWA UFUPI

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.

Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.

Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.

Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.

Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.

“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.

Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

“Ila maofisa hawa walitumia mwanya huo kuihadaa Wizara ya Fedha kwa kuandaa hoja ya safari feki ili kupata fedha hizo,” aliongeza Mahadhi.

Maofisa wengine ni pamoja na ofisa katika Idara ya Itifaki, Shamim Khalfa, Kaimu Mhasibu Mkuu, Kasim Laizer, Mhasibu, Deltha Mafie na karani wa fedha) aitwaye, Shabani Kesi.

Kwanza mbona nchi hii ni full uislamu kila idara? Lakini pili, wangekuwa ni akina abeli, joshua, john, au yohana ungeone magari ya washawasha ya polisi na ving'ora yanavyopishana kuwafikisha mahakamani na kuwakuza kazi. Lakini kwakuwa ni wao watupu hatma anaachiwa rais
 
kweli sikio la kufa halisikii dawa, mtu anafoji ili aibe ela nyingi kiasi hicho, eti anashushwa cheo na kuhamishwa idara.
Hakuna usawa nchi hii angekuwa mwalimu kaiba laki 5 angefungwa miaka kumi. Mambo ya nchi hii yanakera hata kuyasikia ipo siku watu wataanza jitoa muhanga kama wapalestina
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini imesema haijapata ushahidi wa kuweza kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ukwapuaji wa fedha za safari za Rais.

Hivyo basi wamependekeza wachukuliwe hatua za kinidhamu ili waweze kuyamaliza tu..sijui ni kwa nini kumekosekana ushahidi kweli wa kesi kama hii na fedha ndio zishaondoka mda huu.Mambo haya mpaka lini jamani!!

Source
: Tanzania Daima
 
si mchezo na mimi naamini hiyo sio mara ya kwanza hako kamchezo wanakafanyaga mara kwa mara
 
So,kwa njama hiyo adhabu stahiki ni kubadilishwa kitengo?? Tanzania kweli shamba la bibi.
 
Back
Top Bottom