Kashfa ya kigogo Ikulu yaibuka upya

Kashfa ya kigogo Ikulu yaibuka upya

Hawa Kina Shaban Kesi na Hadida Kesi si ndio Mapendeshee wanaowamwagia pesa wale vijana wa Akudo Impact wanaojiita marais kina Christian Bella na wenzake wanaojulikana kama Taasis Maseba Masela, Kanali Top Uncle Shemesha na wengineo?
 
Hii kitu mwanahalisi ambao wanaitwa wachochezi na kufungiwa waliandika kumbe muda ni mwalimu na hakimu mzuri katika kuujua ukweli hata hili la LWAKATARE tutajua tu sana!!!!!!!!!!!
 
Hii yote ni kwa sababu ya JK mwenyewe. Yeye anasafiri tu hajua hata safari ngapi kafanya ndio maana hawa jamaa wanaona hata wakipiga safari zake tatu yeye atakubali tu. TZ shamba la bibi.
 
PCCB inastahili kutokuwepo kabisa make kesi kubwa zimewashinda wamebaki kukomalia rushwa za elfu 10.
 
Watu wameshaanza kusifia vitu bila hata kuelewa habari yenyewe.

Someni habari vizuri muelewe, halafu ndio muanze kuchangia.

Msisifie watu wanaowachezea akili.

Inaonyesha ni jinsi gani mumechanganyikiwa hata kulala hamlari kutafuta pakutengeneza video zamabox
 
kwanini kila mtendaji anaogopa kumwajibisha huyu mkuu wa itifaki.hili ni suala la siku nyingi.nilitegemea Rais awe ameshachukua hatua kuhusiana na hili.Yaani hii serikali ya wamu ya nne kila jambo hata liwe kubwa vipi hawachukui hatua.
 
[/COLOR]
Red: Ndio panaondoa uzito wa hoja yoooooooote, Mh. Lowasa hana uchungu na nchi, yeye ndio mwenyekiti wa kikio cha mambo ya nje, hakuuliza ndani ya kikao, anauliza nje! kwanza Mh. Naibu Waziri kumjibu ni Bahati sana, mwingine asingemjibu, ila inaonekana lowasa anafanya siasa za uanaharakati.....Tanzanian Mbona wakati wati wa mijadala ya sera ya gasi Bungeni hakusema? leo anasema kuna haja ya kuwa na sera ya Gesi? waangalieni wanasiasa wetu
Nimeielewa vizuri point yako. Ndiyo maana hata kwenye hitimisho langu nimedonoa point kuhusiana na motives za Mh. Lowassa kuuliza ili waandishi wa habari wasikie na kudaka swali lake in order to embarrass someone.
Nikisema aliuliza kwa manufaa ya Watanzania nitakuwa nina exaggerate. Ninadhani aliuliza kwa manufaa yake kisiasa zaidi.

Sina uhakika kama wajumbe wa kamati yake kama wote ni wapya, lakini kulitakiwa waulifahamu swala zima na siyo kumtegea mwenyekiti wao wa kamati. Hizi ni pesa nyingi, kamati ilitakiwa kulipa kipauwo cha mbele kujua kinachoendelea.

I'm compelled to believe, kuna madudu mengi kwenye hicho kitengo zaidi ya hili.
 
Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.


Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.
Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.


Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.


Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.
Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.


Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.


Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.
“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.
Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo. Source-MWANANCHI.


My comment: Hapa inaonekana suala hili mkuu wa kaya analijua kinagaubega, ameshiriki hujuma hii!.
 
Bila kupelekwa mahakani kwa kughushi, jamani hii haki kweli au wanakinga ya kidiplomasia ndani ya nchi yao???
 
Eti hatma ya washenzi hao iko mikononi mwa rais, huu ujinga sijui utaisha lini jamani?
 
Lowassa alipouliza swali hilo ghafla hivyo, je hakujua matokeo yake> Au naye ameanza kuwa mwana harakati dhidi ya ufisadi? Aangaliye asiwe feki kama Anne Kilango katika eneo hilo.

Halafu na yeye mzee wa richmond kwanini hakuuliza hilo swali kwenye kikao rasmi akasubiri aje kuliuliza nje ya kikao, au ndo ule msemo wa ondoa kwanza boriti kwenye jicho lako ndo uone kibanzi kwenye jicho la mwenzako?? lakini tumeshawazoea ccm hakuna wa kumfunga paka kengele
 
kwanini kila mtendaji anaogopa kumwajibisha huyu mkuu wa itifaki.hili ni suala la siku nyingi.nilitegemea Rais awe ameshachukua hatua kuhusiana na hili.Yaani hii serikali ya wamu ya nne kila jambo hata liwe kubwa vipi hawachukui hatua.

Sasa kama mkuu wa kaya na yeye alikuwepo kwenye mgao unategemea nini?? manake sioni kwanini ashindwe kumwajibisha mtu ambaye amemteua yeye mwenyewe na imethibitishwa pasipo shaka kuwa amelihujumu taifa. Hapo kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia. ndo maana hata wale maofisa wa itifaki pamoja na kuthibitika bila shaka yeyote kuwa wameshiriki kwenye mpango wote hawajapewa adhabu yoyote, manake kushushwa cheo au kuhamishwa kitengo wakati umetia mfukoni kitita cha nguvu namna ile sio adhabu hiyo. Kwahiyo hapo jamaa wamegwaya kuwawajibisha hao wahalifu coz mkulu inawezekana naye kafaidika na hiyo mihela. TANZANIA ITAJEGNGWA NA WENYE MOYO NA ITALIWA NA WENYE CHOYO
 
Nimekuelewa mkuu.Vasco da Gama aliingia katika utawala kwa lengo moja tu la kuchuma.na amefanikiwa kwenye hili.sijui kama kuna Rais amefuja pesa za nchi hii kama huyu jamaa
Sasa kama mkuu wa kaya na yeye alikuwepo kwenye mgao unategemea nini?? manake sioni kwanini ashindwe kumwajibisha mtu ambaye amemteua yeye mwenyewe na imethibitishwa pasipo shaka kuwa amelihujumu taifa. Hapo kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia. ndo maana hata wale maofisa wa itifaki pamoja na kuthibitika bila shaka yeyote kuwa wameshiriki kwenye mpango wote hawajapewa adhabu yoyote, manake kushushwa cheo au kuhamishwa kitengo wakati umetia mfukoni kitita cha nguvu namna ile sio adhabu hiyo. Kwahiyo hapo jamaa wamegwaya kuwawajibisha hao wahalifu coz mkulu inawezekana naye kafaidika na hiyo mihela. TANZANIA ITAJEGNGWA NA WENYE MOYO NA ITALIWA NA WENYE CHOYO
 
Nchi hii ukiiba ukiwa mkubwa au kushirikiana na wakubwa adhabu ndo kama hizo kuhamishwa vitengo na kushushwa vyeo wakati ushahidi upo wazi..! Afu anatoka mtu huko aliko atuaminishe eti kuna utawala wa sheria..?! Upi huo na wapi?
 
mh kumbe ule wimbo wa jamaa anaerap unaweza ukawa kweli
 
Hapa naishangaa serikali na TAKUKURU kwamba hapakuwa na ushahidi wa kwamba walitaka kuiba!! Kwani kuna sababu nyingine iliyotolewa zaidi ya hii ya safari hewa ya Rais?! Au kwavile hawakuwahi kuzitia mikononi na ndio maana imeonekana hakuna ushahidi hata kufikia hatua ya kushusha vyeo wahusika kama njia ya adhabu!!! Hawa walichofanya ni wizi sawa na wizi mwingine wowote ule, iwe walifanikiwa au hawakufanikiwa. NI kama jambazi anayevunja nyumba lakini kabla hajaiba, polisi wakatokea na kuwakamata! Hata kama hakuna walichoiba, bado kesi yao itabaki pale pale kwamba ni armed robbery.
 
Mama yangu we jamaa wanaandaa safari feki ya rais ili wapige hela, nimeamini hatuna rais aisee....!!! Waliofanya huo mchongo wa 3b wanafahamika lakini hawajachukuliwa hatua yeyote wanaishia tu kubadilishwa vyeo??? Watu wanalamba 3billion kwa kuandaa safari feki ya Mh Rais halafu bado tu wanaangaliwa??? kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Mimi nilitegemea eti ile tu kugundua kuwa jamaa walikuwa wanapiga mchongo wa kuandaa safari feki ya Rais ilikuwa inatosha kuwatimua kazi na kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake, badala yake jamaa wanaendelea kula bata kama kawaida.
Waziri anasema:
“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.


Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

“Ila maofisa hawa walitumia mwanya huo kuihadaa Wizara ya Fedha kwa kuandaa hoja ya safari feki ili kupata fedha hizo,” aliongeza Mahadhi
Na bado hao maafisa wako nao mpaka leo...!
 
Yani mkweree anasafiri mpaka watu wanchanganyikiwa maana hawajuhi hata kama yupo au kasafiri na naamini hakuna record ya safari zake.
Ila tumejifunza kitu kuwa safari moja si chini ya 3 Bil. Sasa piga hesabu safari zaidi ya 370 x 3 Bil. = 1,110 Bil. Na hii na hamini ni kima cha chini tu.
 
kwa hiyo wanataka kutuambia Mh rahisi amekalia ripoti ya TAKUKURU?

au ndo kama kawaida ulikuwa upepo tu umeshapita


Hiyo haitakuwa ripoti ya kwanza kuikalia mbona hata ya JAIRO kaikanyaga kabisa mpaka aondoke nae madarakani!!
 
Lowassa ni Jembe, alijua fika anachokifanya maana deal hiyo ilikuwa inamhusisha pia mkuu wa kaya! Jamaa ni Strategist mzuri, siku zote huwa anatembea na little dirt briefcase, Lyatonga huwa anasema ukimwaga ugali yeye anamwaga mboga...CCM wanalindana kwa ufisadi wao! hakuna msafi bali wanazidiana kwa kunuka...

Inawezekana kabisa katika dili hili la bilioni 3, bwana maendeleo nae alikuwa na mgao wake; kwani haiwezekani kabisa kuwa huu mpamgo ulisukwa hivi hivi tu kama huko nyuma hawakuwahi kuchukua kwa staili hii!!
 
Back
Top Bottom