Kashfa ya Escrow: Mnikulu Shabani Gurumo atimuliwa Ikulu

Kashfa ya Escrow: Mnikulu Shabani Gurumo atimuliwa Ikulu

Walau amechukua hatua kirichobaki tupaze sauti zetu ili haki itendeke na ionekane ikitendeka kwa kuenda mahakamani
 
imebaki miezi minne ndugu yake aachie ikulu...kapewa mda wa kwenda kutumia za escrow,bwana mkubwa ata-mjoin baadae visiwa vya caribbean
 
Wah!!kutimuliwa kazi/kustaafishwa ukiwa namamilioni ya escrow acha hayo mengine nyuma ya public eye, unalipwa haki zako..ni jambo la kujivunia katika nchi yenye weak and corrupt system kama ya kwetu...no wonder watajuivunia kwa hilo na wananchi tutawapigia makofi...
 
Ikulu imechafuka sana, madhara ya kufanya kazi kwa mazoea.Kama aliyoyasema Tundu Lisu dhidi ya Gurumo ni kweli, basi hamna msafi pale Ikulu.
 
Kwani hapo Magogoni alikuwa peke yake? Yule mama nanilino naye vipi? Na mkubwa wao aliyetetea anaachwaje?
 
1 Wakorintho 6

8 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
9 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
Samahani kwa uelewa zaidi naomba nipe tofauti ya wafiraji na walawiti - Nini tofauti ya Kufira na kulawiti?
 
Ndiyo mambo anayokataza Mwigulu. Hapa hatutakiwi kuambia karuhusiwa kwenda kutanua. Tuambiwe anefikishwa mahakamani
Mbona mnafikiri watanzania wote ni fuata mkumbo jamani? Mwingulu huyu anayewatumikia hao mafisadi na yeye fisadi halafu unatudanganya eti ndio mambo anayokataza? Usilete uhayawani wako hapa tafadhali!
 
Samahani kwa uelewa zaidi naomba nipe tofauti ya wafiraji na walawiti - Nini tofauti ya Kufira na kulawiti?

Iwe kwa wanawake au kwa wanaume, yote ni haramu na hatouona "ufalme wa Mungu" anaefanya hayo.
 
Back
Top Bottom