Kashfa ya ajira TANAPA

Yaani nchi hii kama huna wa kukushika mkono umekwisha! mm naka diploma kangu nilishaapply kazi mpaka sasa nimeamua niwe chinga tu! natamani kurudi shule, nikifikiria niache umachinga nirudi shule (full time)familia itakufa njaa. Nyegezi nao evening classes wamefunga! basi kasheshe.
 
tanzania bwana majibu yakiwahi kutoka tatizo . na yakichelewa kutoka tatizo.
 
Mkuu pole sana..subiria ya TASAF utaona moto wake..at least hao walifanya written ngoja tuone walioapply TASAF watasemaje..
 
Wizi mtupu. Kuna haja gani kuita watu 100 kwenye interview wakati unahitaji 1. I love UN agency!
 
Hahaaa!! "Unajuwa mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni" sasa tatizo ni lipi? Nikutoa majina mapema au tatizo haukuchaguliwa uanajuwa sme tyme tusitoe hoja kisia zaidi ila toa kitakwim/kitaluma. Sasa hebu tuonyeshe usibitisho wa hiyo kashfa ya ajira uliyo ipa TANAPA. Kama ndiyo hiyo uliyo toa hapo umekosea cz umeitoa kisia!! TAFUTA KAZI AU JIAJIR KUEPUSHA LAWAMA, YANGU NI HAYO TU.
 
Mimi sipendi generalise mambo lakini kama kweli walikuwa 800 kwa spidi ya supersonic waliyotumia it is most likely walikuwa na watu wao kwa hiyo they went through the motion kujustify the whole exercise
 
Wakati nipo chuo mzumbe
kuna classmates alikuwa anatutania

"Mkinipita kwenye gpa mimi nitawapita kwenye soko la ajira"

Alikuwa anasoma kivivu kweli tukajua atapata shida sana kwenye soko na
gpa yake ndogo, uliza alichotufanya baada ya kumaliza chuo alianzia kazi
tanesco hata majibu hayajatoka and then akaamia zake tra wakati wenye
gpa kubwa mpaka leo tunasua sua, yaan dogo anachagua kazi kama zake
alipata bot mwanza akasema hawez kuondoka dar akaamua kubaki tra...
Watoto wa kishua wana raha sana mjini hapa, kila kitu kinaenda kwa
mteremko wakati watabe wanasota
mkata kiu umenikumbusha mbali!
studio !studio!unanipata studio!
 
Jamani pepa wametoa NBAA na wamesahihisha NBAA msianze majungu

skuizi kuna NBAA au takataka tu, mana nao ndo walewale tu,yani mkuu kwa kifupi bongo skuizi ni madudu matupu, private watu walikuwa wanaona wako poa, kumbe naka skuizi wameingiwa na wandawezimu nao yale yale tu.
 
Je, ni rahisi kwa taasisi kubwa kama Tanapa kusahihisha written interview (yenye maswali 25) ya zaidi ya watu 800 kwa masaa ma 5 tu na kutoa matokeo kuwa watu 30 pekee ndo wamefaulu kuendelea na oral interview?!

ninasema hivyo kwa kuwa naona kama kuna rushwa na kujuana maana haingii akilini zaidi ya watu 800 pepa yao kusahihishwa kwa masaa ma 5 halafu eti matokeo yanawaruhusu 30 tu na wanaarifiwa the same day kuwa keshoye warudi for oral interview.

ni hivi:
tarehe 13 august kulikuwa a interview ya nafasi mbali mbali za kazi katika Tanapa.interview ilifanyikia msimbazi center saa 3 asubui mpaka saa 5 asubui.maswali 25 yalipitishwa kwa watahiniwa ili wayafanye.ilipofika saa 11 jioni majina ya watu 30 waliofaulu kuingia oral interview yakabandikwa.sio matokeo ya watahiniwa wote waliofaulu,bali ni majina tu na wala haionyeshi maksi zao.
nina wasi wasi matokeo na majina yalishapangwa kitambo na ile interview ilikuwa ni kutimiza wajibu tu..naomba vyombo vinavyohusika vilifuatilie suala hili ili kuondoa kujuana ndani ya taasisi hizi kubwa za serikali
St. Marrian Girls wamefanya interview watu 4,000. Mitihani mitatu ya Hesabu, Maarifa na Kiingereza, kila mtihani una maswali 50. Kila mtihani ni 1 hour, mitihani imeanza saa 3:00-6:00 mchana. Majibu yamepatikana saa 10:00 jioni the same day!.

Hivyo inategemea wasahihishaji ni wangapi, headline ni too definite as if kuna kashfa kweli, kumbe ni just a desparate job seeker, amekosa vigezo, sasa anakuja kulia lia humu jf ili kupata sympathisers baada ya kukosa kazi TANAPA!.

Headlines za namna hii, ndizo zinazopunguza credibility ya jukwaa letu, unapoita issue ni kashfa, lazima uje na udhibitisho wa kuwepo kwa kashfa ya ukweli na sio kashfa ya hisia just kisa, umekosa kuwa short listed!.

Kwa kukusaidia tuu, lengo la writen interview za kazi, ni elimination process kupunguza waombaji wasio na sifa na vigezo, hivyo hata handwriting tuu inatosha kukueliminate bila hata kusoma ulichoandika!.

Namalizia kwa kukupa pole kukosa kazi TANAPA, ushauri wa bure, endelea kuomba kazi sehemu mbalimbali sio lazima mpaka TANAPA!.
 
Pale ni kwa watu wa tanga tu nenda ukatafiti 80% ni tanga.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Swala hapo si muda gani umetumika kusahisha hiyo interview yenu, ni je unauhakika ulifanya vizuri na jina lako halikurudi kwa wale walioshinda?
Pili kwa ujumla interview nyingi hapa kwetu hata zisimamiwe na nani ni magumashi tu!, kuna baadhi hata unaweza kuta hawakuwepo kabisa katika kutahiniwa ndio unaambiwa wameshinda. Kazi ipo!
 
Tanapa imeoza na inanuka hata kama wakijisafisha kila siku kwenye TV.

Siku nyingine usitumie nguvu kuomba Tanapa hawafai kabisa.
 
Je, ni rahisi kwa taasisi kubwa kama Tanapa kusahihisha written interview (yenye maswali 25) ya zaidi ya watu 800 kwa masaa ma 5 tu na kutoa matokeo kuwa watu 30 pekee ndo wamefaulu kuendelea na oral interview?!

ninasema hivyo kwa kuwa naona kama kuna rushwa na kujuana maana haingii akilini zaidi ya watu 800 pepa yao kusahihishwa kwa masaa ma 5 halafu eti matokeo yanawaruhusu 30 tu na wanaarifiwa the same day kuwa keshoye warudi for oral interview.

ni hivi:
tarehe 13 august kulikuwa a interview ya nafasi mbali mbali za kazi katika Tanapa.interview ilifanyikia msimbazi center saa 3 asubui mpaka saa 5 asubui.maswali 25 yalipitishwa kwa watahiniwa ili wayafanye.ilipofika saa 11 jioni majina ya watu 30 waliofaulu kuingia oral interview yakabandikwa.sio matokeo ya watahiniwa wote waliofaulu,bali ni majina tu na wala haionyeshi maksi zao.
nina wasi wasi matokeo na majina yalishapangwa kitambo na ile interview ilikuwa ni kutimiza wajibu tu..naomba vyombo vinavyohusika vilifuatilie suala hili ili kuondoa kujuana ndani ya taasisi hizi kubwa za serikali
mdau naomba nikusahihishe kidogo watu walioitwa kwenye interview walikuwa 1020. waliohudhuria walikuwa chini ya mia saba(700). pia walisahihisha paper zote mpaka saa moja. matokeo yalitoka kama 7:20pm. then majina ya watu 30 yalibandikwa. kutobandika majina yote ni sababu za kimazingira na uchumi.
 
mimi ndo nilishajikatia zangu tamaa kuomba kazi sehemu kama izi. acha tu akiba yangu iwe nzuri kilimo kwanza wanikopeshe trekta la suma nikae zangu kijijini niendeleze mashamba ya babu
 
Nchi hii magumashi kuanzia level ya juu mpaka level ya mtaa. Pole ndugu kwa kujiandaa na intavyuu, pengine majibu yako yanafungia maandazi mtaani....cha msingi usikate tamaa tafuta namna ya Ku-swim upstream namaanisha ku-beat the system
 
Dah ,hivi ni vita kama huna mtu kazi yako wwe ni uwalimu tu ndio umebaki bila kupendeleana lakini sehemu nyingine taabu tupu mujiajili tu wenyewe nduguzangu if u like or not hiyo ndio option iliyobaki
 
Back
Top Bottom