Kwa kweli aibu za pale balaa! hata mimi nilipita pale hivi karibuni nilipata kizunguzungu. Mizigo inafungiliwa kirahisi na inaonekana wafanyakazi wa uwanja wanaelewana na wa nyanja nyingine za ndani KIA nk. maana wanao-scan mizigo ulikotokea inakua kama wanawapigia wenzao simu huko Dar kuwaambia details za vitu walivyoviona kwenye mzigo wa mtu. Especially kama umeweka kitu kama perfume mpya ndani ya mzigo ni lazima ufunguliwe pindi ufikapo JKN.
Hizi comments za Julius hapo juu ni nzito sana, mpaka mwananchi aikatae nchi yake namna hiyo ni kwamba imeuma, imemchefua. Sasa jiulize mgeni aliyekuja kuwekeza shida laizopata kufanya biashara yake humo ndani, usumbufu wa TRA, serkali za mitaa, traffic, jeuri za wanasiasa halafu na uwanja wa ndege si ndio maana wanaamua hata kuiba yaani kupakua kwa hasira! Kwamba hii nchi ya majitu majinga namna hii hakuna haja ya kuionea huruma!
Niliacha kutumia ile sehemu ya VIP maana niliona kuna kila dalili ya kuambukizwa ugonjwa kule. That place is small, filthy and has no windows, haina mzunguko wa hewa safi . Infact iko kama a garage converted to a VIP room!