Kashfa nzito: Malipo hewa kwa wabunge na ubadhilifu wa pesa bungeni waanikwa na CAG

Ningependa kujua hio ni mashine ya aina gani.., na inanunuliwa kwa fedha kiasi hicho bila guarantee ?

Kweli hapa someone must be answerable.
Hilo sio kwa Tanzania kwenye shamba la bibi. Hivi sasa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iceland yuko Mahakamani kwa kosa la kutochukua tahadhari juu ya hali ya uchumi. Petu watu wanajikusanyia hawana woga. Nani anaubavu wa kuwashitaki. Labda tuwapeleke kwa OCampo.
 
Hizi pesa zimelipwa na ofisi ya Bunge kama masurufu. Masurufu baada ya kutumiwa huwa unaretire/settle kwa risiti. Kama wafanyakazi wa Bunge au hata wabunge wamepewa masurufu hayo ofisi ya Bunge ndiyo inatakiwa iwakumbushe ku'retire'/settle masurufu yao kutokana na risiti zinazoonyesha matumizi halali. Kama ofisi ya Bunge haijali kuona hizi pesa zinakuwa accounted for basi pengine ni wafanyakazi wenyewe. Tusiwalaumu wabunge kwamba wanahusika sidhani kama ni kweli.

Jana ilikuwa siku ya mwisho ya Bunge, CAG ametoa taarifa na hivyo huwezi kusema kitu ambacho hujakifanyia research. No research/No right to speak. Mnataka waseme hewa?
 
Utoh%2822%29.jpg
Anne%20Makinda%283%29.jpg

Kushoto (CAG), Ludovick Utouh Kulia Speaker Anne Makinda

Malipo hewa kwa wabunge yabainishwa

Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG), Ludovick Utouh, amebaini kulipwa kwa posho ya kujikimu Sh. 6,960,000 wabunge wakati hawakuwa mjini Dodoma.

Hayo yapo katika ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka jana, iliyowasilishwa katika mkutano wa saba wa Bunge. Pia alisema Sh. 20,915,126 zililipwa kwa wafanyakazi kinyume cha kanuni za Bunge na mwongozo wa utumishi.

Utouh alisema uongozi uliripoti kuwepo kwa madeni katika taarifa ya fedha ambayo ni Sh. 209, 010,235. Alisema madeni hayo ni kinyume cha mfumo wa bajeti ambayo unatumiwa na serikali.

Aidha, malipo yenye thamani ya Sh. 163,195,130.34 hayakuwa na nyaraka zinazostahili kama kanuni ya 94 (4) ya kanuni ya fedha za umma ya mwaka 2001. Pia ukaguzi huo umebaini posho za muda wa ziada wa kazi na posho nyingine zinazofikia Sh. 94,000,000 zililipwa kwa wafanyakazi wa Bunge.

Pia alisema madurufu ya safari (imprests) yenye thamani y a Sh. 65,803,144 hayakurudishwa kwa mwaka mzima kinyume na kanuni namba 103 (1) (7) ya kanuni ya fedha za umma ya mwaka 2001 ambayo inataka madurufu ya awali kurudishwa kabla ya kutoa mapya.
Aliongeza kuwa marejesho yanatakiwa kurejeshwa siku 14 tangu mfanyakazi aliporejea kutoka safari ambayo aliombea madurufu. Ripoti hiyo imeonyesha kuwa matumizi ya sh 170,858,030, vocha za malipo zilikosekana.Katika ripoti hiyo kunabainisha kuwa uongozi wa Bunge ulinunua mashine ya kuchapisha kwa gharama ya sh 370,019,894 lakini haikufanya kazi.

Hivyo, ilisababisha uongozi wa Bunge kukodisha mashine nyingine kwa malipo ya Sh. 190,480,496 kwa mwaka. Hali kadhalika uongozi wa Bunge, haukuweka kumbukumbu sahihi kama vile za orodha ya mali zisizohamishika hali inayosababisha mapungufu mbalimbali.
Alizitaja kuwa ni magari mawili yaliyosajiliwa kwa namba STK 8590 aina Toyota Land Cruiser Hardtop na STK 3039 Toyota LandCruisser hazikuwekwa katika orodha ya mali zisizohamishika. Magari hayo yalishushwa thamani ya mali kwa kuwekwa katika taarifa ya fedha.
Loooo!
Tutabakiwa nini baada ya utawala huu?
 
Utoh(22).jpg
Anne%20Makinda(3).jpg

toa kwanza boriti ndani ya jicho lako ndipo utoe kibanzi ndani ya jicho la mwenzio. aibu kwa bunge
 
Mkuu, ofisi ya bunge ndio iliyokaguliwa sio wabunge!!

kama wabunge hewa wamelipwa, then ofisi ya bunge ituambie ilikuwaje ikawalipa?

SIMPLE.

Kila ofisi ya serikali na umma ni ufujaji tu wa fedha za wavuja jasho
 
Inauma, huu ni ujanja wa CCM kupoteza mada na msisimko wa kuwahitaji Mawaziri fisadi wajiuzuru.
1. Kwa nini CAG hakutaja kashfa hii mpema anakuja kutaja wakati huu Taifa linawakodolea Mawaziri macho?
2. Kama ni ukweli kuhusu ufujaji wa fedha umefanywa na wabunge; ina maanisha CAG anafahamu kashfa nyingi ambazo hazitaji na huu ni ukiukaji wa kisheria kwa kuwa ni matumizi mabovu ya madaraka?
3. Kama si kupoteza ramani kuu ya Mawaziri kujiuzuru; kwa nini Spika Makinda alitoa kauri za kuwaridhisha mawaziri?
4. Kwa nini Rais na Waziri Mkuu hawana haraka ya kuwawajibisha hawa mawaziri fisadi?

Ripoti ya CAG ina kurasa zaidi ya 300 so sio kwamba kaja hii ni mtu kupitia na kunyofoa sehemu ya taarifa!
 
Anayetakiwa kuwajibisha mawaziri ndo huyo anayetakiwa ktwajibisha watendaji wa bunge. Aache kukwepa wajibu, awajibishe wote maana ripoti ya CAG anayo.
 
mbowe,mnyika na zotto nao walipokea?????????????

Nilivyoelewa ni kwamba ripoti imebainisha malipo hewa kwa wabunge, maana yake hakuna mbunge aliyepokea hela ila rekodi zinaonyesha wamelipwe. Ni mwizi alichukua hela zote na kuandika zimechukuliwa na wabunge.
 
Mi sina tatizo na hili la kusema kuwa bunge nalo linahusika na ufisadi huo, na kama ikithibitika nao wachukuliwe hatua, Ila nadhani hili linaibuliwa kwa kuwaambia wakubwa hao wa mjengoni kuwa hata wao wamo kwenye kunyonya wananchi, na ni kama waibuaji wanataka wabunge wafunge midomo hivi... Ni ile esemi kuwa kwa kuwa wao wamemwaga mboga basi nasi tumwage ugali...
 
Mkuu, ofisi ya bunge ndio iliyokaguliwa sio wabunge!!

kama wabunge hewa wamelipwa, then ofisi ya bunge ituambie ilikuwaje ikawalipa?

SIMPLE.

Kweli Mkuu, uko sahihi! Hata hivyo kama wabunge wamepokea malipo hewa nao wanahusika PERSONALLY!! Kwa hiyo hawawezi kukwepa liability!
 
Mkuu, ukiangalia vizuri ni kwamba malipo hewa kwa wabunge ni 6.9 million tu......ni kiasi kidogo compared na upotevu wa fedha katika wizara nyingine.

However, kinachonisikitisha ni hii hapa

Mkuu uovu ni uovu tu, angalau Wabunge wangesema hata hicho kidogo, ningewaelewa, maana kwa upande wa Serikali walikuwa wanapigilia msumari hata kwa uuzaji wa twiga!! Hivi thamani ya twiga mmoja inaweza kufikia milioni sita?
 
Anna Makinda Semamba na Katibu wa bunge wanabeba lawama kwa vile ndio watendaji wakuu na waidhinishaji wa matumizi ya Bunge. Hapa ngoma nzito
 
ndio spika akafunika kombe la mawaziri akijua nae anahusika na kapu lake
 
Haya Bimkubwa usione aibu Chapa lapa kwa hii kashfa. Kumbe na wewe ulikuwa unakula kwa urefu wa kamba yako! Tutabaki na naibu spika
 
inauma, huu ni ujanja wa ccm kupoteza mada na msisimko wa kuwahitaji mawaziri fisadi wajiuzuru.
1. Kwa nini cag hakutaja kashfa hii mpema anakuja kutaja wakati huu taifa linawakodolea mawaziri macho?
2. Kama ni ukweli kuhusu ufujaji wa fedha umefanywa na wabunge; ina maanisha cag anafahamu kashfa nyingi ambazo hazitaji na huu ni ukiukaji wa kisheria kwa kuwa ni matumizi mabovu ya madaraka?
3. Kama si kupoteza ramani kuu ya mawaziri kujiuzuru; kwa nini spika makinda alitoa kauri za kuwaridhisha mawaziri?
4. Kwa nini rais na waziri mkuu hawana haraka ya kuwawajibisha hawa mawaziri fisadi?

werevu tu ndo wanaijua mitego ya ccm........chama cha kinfiki
 
Back
Top Bottom