Kashfa nzito: Malipo hewa kwa wabunge na ubadhilifu wa pesa bungeni waanikwa na CAG

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
Utoh(22).jpg
Anne%20Makinda(3).jpg

Kushoto (CAG), Ludovick Utouh Kulia Speaker Anne Makinda

Malipo hewa kwa wabunge yabainishwa

Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG), Ludovick Utouh, amebaini kulipwa kwa posho ya kujikimu Sh. 6,960,000 wabunge wakati hawakuwa mjini Dodoma.

Hayo yapo katika ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka jana, iliyowasilishwa katika mkutano wa saba wa Bunge. Pia alisema Sh. 20,915,126 zililipwa kwa wafanyakazi kinyume cha kanuni za Bunge na mwongozo wa utumishi.


Utouh alisema uongozi uliripoti kuwepo kwa madeni katika taarifa ya fedha ambayo ni Sh. 209, 010,235. Alisema madeni hayo ni kinyume cha mfumo wa bajeti ambayo unatumiwa na serikali.


Aidha, malipo yenye thamani ya Sh. 163,195,130.34 hayakuwa na nyaraka zinazostahili kama kanuni ya 94 (4) ya kanuni ya fedha za umma ya mwaka 2001. Pia ukaguzi huo umebaini posho za muda wa ziada wa kazi na posho nyingine zinazofikia Sh. 94,000,000 zililipwa kwa wafanyakazi wa Bunge.


Pia alisema madurufu ya safari (imprests) yenye thamani y a Sh. 65,803,144 hayakurudishwa kwa mwaka mzima kinyume na kanuni namba 103 (1) (7) ya kanuni ya fedha za umma ya mwaka 2001 ambayo inataka madurufu ya awali kurudishwa kabla ya kutoa mapya.
Aliongeza kuwa marejesho yanatakiwa kurejeshwa siku 14 tangu mfanyakazi aliporejea kutoka safari ambayo aliombea madurufu. Ripoti hiyo imeonyesha kuwa matumizi ya sh 170,858,030, vocha za malipo zilikosekana.Katika ripoti hiyo kunabainisha kuwa uongozi wa Bunge ulinunua mashine ya kuchapisha kwa gharama ya sh 370,019,894 lakini haikufanya kazi.

Hivyo, ilisababisha uongozi wa Bunge kukodisha mashine nyingine kwa malipo ya Sh. 190,480,496 kwa mwaka. Hali kadhalika uongozi wa Bunge, haukuweka kumbukumbu sahihi kama vile za orodha ya mali zisizohamishika hali inayosababisha mapungufu mbalimbali.
Alizitaja kuwa ni magari mawili yaliyosajiliwa kwa namba STK 8590 aina Toyota Land Cruiser Hardtop na STK 3039 Toyota LandCruisser hazikuwekwa katika orodha ya mali zisizohamishika. Magari hayo yalishushwa thamani ya mali kwa kuwekwa katika taarifa ya fedha.
 
Wabunge wangeanza kusafisha kasha za uvujaji mali ya umma unaofanywa katika bunge letu na moto huo unendelee taasisi nyingine za serikali. Haya yanayotokea bungeni yamenishtua. Na hakuna wabunge waliotoka povu kama ilivyotokea kwa taasisi nyingine za serikali.
 
Ooh Boy, yaleyale....!! If you scratch my back, i'll scratch yours.
Kwa mwendo huu ni nani atakuwa na moral authority ya kumnyooshea kidole mwenzake?
Kama hivi ndivyo, Bunge liwawajibishe watendaji wa Bunge kama muendelezao wa OPERESHENI UWAJIBIKAJI, kwani udhaifu huu unapaswa kubebwa na hao
 
1. Watajwe hao wabunge na wafanyakazi husika
2.Masurufu na si madurufu.
3.Kama mtu kapewa masurufu(imprest) na hajafanya marejesho(retirement/settlement), kwa nini inaonekana kwenye vitabu vya fedha kama madeni wakati mfumo ni kumkata yule mtumishi kwenye mshahara wake kiasi kile kile ailichopewa?Naomba kueleweshwa hapo.
 
Ooh Boy, yaleyale....!! If you scratch my back, i'll scratch yours.
Kwa mendo huu nani atakuwa na moral authority ya kumnyooshea kidole mwenzake?
Kama hivi ndivyo, Bunge liwawajibishe watendaji wa Bunge kama muendelezao wa OPERESHENI UWAJIBIKAJI, kwani udhaifu huu unapaswa kubebwa na hao

Ninachochangaa kwa nini wabunge hawakutoka povu katika madai haya kama ilivyotokea kwa taasisi nyingine? Maana yake wizarani wanagombea kupata uwaziri au?
 
Nilishangaa jana wabunge katika kipindi cha kuhitimisha bunge walikuwa wapole isivyo kawaida kumbe (CAG), Ludovick Utouh kawafunga goli la tikitaki.

Kama taarifa ya CAG ilikuwa pia na ripoti dhidi ya Wabunge hapa kuna maswali mengi sana! Yaani hata Zitto hajasema lolote juu ya hili? Hapa kazi ipo!
 
Hapa kwetu kila siku ni kufichua kashfa nzito, nini kifanyike ndo sasa hv ilitakiwa iwe ishu ya kuijadili. Hizi kashfa nzito tutaendelea tu kuziona na kuzianika as long as hatuna means ya kupambana nazo. Mimi nadhani badala ya umahiri wetu kuuelekeza kwenye kufichua kashfa nzito, umahiri huo sasa ujikite kwenye kucraft strategies za kupambana na ubadhirifu sustainably. Otherwise, wanaosababisha hizo kashfa nzito wataendelea kutuona mambwa koko na kutuita wavimba macho.
 
Kama taarifa ya CAG ilikuwa pia na ripoti dhidi ya Wabunge hapa kuna maswali mengi sana! Yaani hata Zitto hajasema lolote juu ya hili? Hapa kazi ipo!
Mkuu, ukiangalia vizuri ni kwamba malipo hewa kwa wabunge ni 6.9 million tu......ni kiasi kidogo compared na upotevu wa fedha katika wizara nyingine.

However, kinachonisikitisha ni hii hapa

Katika ripoti hiyo kunabainisha kuwa uongozi wa Bunge ulinunua mashine ya kuchapisha kwa gharama ya sh 370,019,894 lakini haikufanya kazi.

Hivyo, ilisababisha uongozi wa Bunge kukodisha mashine nyingine kwa malipo ya Sh. 190,480,496 kwa mwaka.
 
Kama taarifa ya CAG ilikuwa pia na ripoti dhidi ya Wabunge hapa kuna maswali mengi sana! Yaani hata Zitto hajasema lolote juu ya hili? Hapa kazi ipo!
Mkuu, ofisi ya bunge ndio iliyokaguliwa sio wabunge!!

kama wabunge hewa wamelipwa, then ofisi ya bunge ituambie ilikuwaje ikawalipa?

SIMPLE.
 
Kule bungeni nako kuna madokta na maprofessor...wote ndo wale wale...wezi na wadokoaji pale inapowezekana...lakini sio kama mawaziri....mhhh
 
DUH! WABUNGE WAMEZIBWA MIDOMO! na nawaambia subirini mtaambiwa Mbowe, Zitto wamo humo! dah! kweli HATUTAFIKA kama wananchi wakiandamana maji ya washa washa na mabou ya machozi na wabunge nao wanazimwa kama hivi! KAZI IPO Tanzania!
 
.
Katika ripoti hiyo kunabainisha kuwa uongozi wa Bunge ulinunua mashine ya kuchapisha kwa gharama ya sh 370,019,894 lakini haikufanya kazi.

Hivyo, ilisababisha uongozi wa Bunge kukodisha mashine nyingine kwa malipo ya Sh. 190,480,496 kwa mwaka.
Ningependa kujua hio ni mashine ya aina gani.., na inanunuliwa kwa fedha kiasi hicho bila guarantee ?

Kweli hapa someone must be answerable.
 
Inauma, huu ni ujanja wa CCM kupoteza mada na msisimko wa kuwahitaji Mawaziri fisadi wajiuzuru.
1. Kwa nini CAG hakutaja kashfa hii mpema anakuja kutaja wakati huu Taifa linawakodolea Mawaziri macho?
2. Kama ni ukweli kuhusu ufujaji wa fedha umefanywa na wabunge; ina maanisha CAG anafahamu kashfa nyingi ambazo hazitaji na huu ni ukiukaji wa kisheria kwa kuwa ni matumizi mabovu ya madaraka?
3. Kama si kupoteza ramani kuu ya Mawaziri kujiuzuru; kwa nini Spika Makinda alitoa kauri za kuwaridhisha mawaziri?
4. Kwa nini Rais na Waziri Mkuu hawana haraka ya kuwawajibisha hawa mawaziri fisadi?
 
Last edited by a moderator:
Kama taarifa ya CAG ilikuwa pia na ripoti dhidi ya Wabunge hapa kuna maswali mengi sana! Yaani hata Zitto hajasema lolote juu ya hili? Hapa kazi ipo!
Jamani, kila kitu Zitto.
Hapa tu nimepata karibu ya bilioni moja (929,903,559).
Kwa mtaji huu, TZ kwishney.
 
I do not remember when was the last time I have come across something which made me happy!

Everyday ni yale yale tu...

Nihamie jukwaa la mapenzi:A S shade::A S shade::shut-mouth::A S angry:
 
Hapa lazima tujikoroge. Hivi pesa za waheshimiwa sihuwa zinaingizwa kwenye akaunti zao mmesahau mkakati wa cdm kuzikataa posho leo mnataka kuwamix na wezi wakubwa walioko serkalini? Posho hazigawiwi kama pdm huingizwa kwenye akaunti moja kwa moja. Hivo suala la kuwa majina yawekwe ni janja ya magamba kuwapaka matope wabunge. Uzi uko palex2 mafisadi washughulikiwe.
 
Back
Top Bottom