Kashfa nyingine kituo cha mabasi ubungo;mzabuni mpya kuwapeleka mahakamani jiji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa nyingine kituo cha mabasi ubungo;mzabuni mpya kuwapeleka mahakamani jiji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 27, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Katika kikao kilichokaa majuzi cha madiwani wa jiji la dar..waliongelea swala la kituo cha mabasi cha ubungo
  katika hilo waliongelewa sheria ya kupandisha kodi kwa wanaoongia ndan ya uwanja huo kama kibwagizo cha mzabuni alieshinda zabuni ya kusimamia uwanja huo..kwanza niulize jamani huyu mzabuni analipa ngapi kwanza huko serikalini isije ikawa mkataba ni ule ule wa mtoto wa kingunge wamebadilisha jina watu tumekaa kimya

  katika mahojiano madiwan hao walienda kuonana na baadhi wahusika wa shguli za kituo hicho ambao wamesema wazi
  kituo kinaitaji kufanyiwa marekebisho na uboreshaji na sio kuongeza tu hela wakati hizo mnazopata mmeshindwa kurekebisha baadhi ya vitu.. Baada ya kuongea hayo meya alikaa na madiwani na kukubaliana kusitisha hoja ya kutumia sheria yampya ya kuongeza viwango vya viingilio

  pamoja na hayo meya alipokea malalamiko kutokakwa mzabuni alieshinda zabuni ya kusimamia uwanja wa mabasi waubungo kwa kudai mkurugenzi wa jiji anapingana na mkataba kwa kuidhinisha baadhi ya watu tena wakiwa na barua zake waweze kuingia bure uwanjani nahivyo kwenda kinyume na mkataba wao...meya alishauri mgogoro huo uende kikao cha kamati ya fedha na uongozi na mzabuni aitwe na asikilizwe pamoja na vikao vyao

  mzabuni huyo ametoa notisi ya mwezi mmoja kwenda mahakamani kulishtaki jiji kwa kuvunja mkataba wake ikiwemo kuingiza watu kwa vimemo kinyume na mkataba...

  Anayway sidhani kulikuwa na haja ya kufikisha swala hili kamati ya fedha wakati meya mwenye akili zako timamu umeshika mkataba ukiwa na lugha mbili za kiingereza na kiswahili na zinasema nini ....na unajua kusoma
  hapa ndipo hoja ya lowasss ya maamuzi magumu inapotakiwa mkurugenzi wa jiji awezi kuwafanya madiwani wajinga na wapumbavu kiasi hicho kutoa memo ovyo watu waingie bure hata kama ajapata 10% ya hako kamktaba
   
Loading...