Kashfa mpya jeshi la polisi

mmbangifingi

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2011
Posts
2,839
Reaction score
567
Jeshi la Polisi Tanzania kupitia simu iliyotumwa kwa Makamanda Mikoa yote Tanzania bara limewataka askari wote wanaotumia vyeti vya kughushi wajiondoe wenyewe kwa kuacha kazi ama kuomba kustaafu kwa hiari la sivyo ikifika August 2014 watakamatwa na kufunguliwa mashtaka. What a shame!!!mtu aliyekula mishahara ya serikali kwa miaka yote kwa kudanganya unampa muda wa kujiondoa badala ya kumkamata na kumfungulia mashtaka sambamba na kurejesha mishahara yote aliyolipwa kipindi chote? Wanamuiga JK na tamko lake dhidi ya wezi wa EPA?

My take: Tanzania sasa tunapoteza mwelekeo mazima. Baada ya kashfa ya kuruta 200 kubainika na vyeti bandia CCP nilitarajia wote


wanaohusika na Kitengo cha ajira kuwa wameshawajibishwa na majalada ya uchunguzi kufunguliwa dhidi yao.
 

Attachments

  • IMG-20140603-WA0018.jpg
    41.9 KB · Views: 5,953
Kile kikundi cha mbwa mwitu sasa kitaingiza wataalamu rasmi...yetu macho
 
Hivi hii inji ya tanganyika ni nani aliyeturoga? Haya ni matunda ya serikali 'sikivu' ya CCM.
 
Walivyowengi si jeshi litavunjika.

Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!! Polisi kuna kubebana kwa kijinga sana. angalia hata utoaji wa mikataba kwa wanaostaafu,,Kova anastaafu eti anapewa mkataba,,kwa kipi? hakuna wengine kujaza nafasi hiyo? Kibabu cha Anti drug unit hakibanduki sababu ya uswahiba tu,,kama ni madawa trend ya kuingizwa nchini inazidi kukua. shame!!!!
 
Wakamateni na hao wanaowauzia vyeti feki maana wanajulikana. Ni sawa na kumkamata mwanamke anayejiuza huku mkiwaacha wanunuzi wakitamba mitaani.
 


Lowassa amcharukia Mkurugenzi Mkuu Nida




By Muhibu Said



31st May 2012



Email




Print




Comments





Edward Lowassa


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo Nje, Ulinzi na Usalama imeitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kutoa maelezo kuhusu taarifa yake kwamba, kuna askari 700 wa Jeshi la Polisi na 248 wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliobainika kila mmoja kutumia cheti kimoja cha elimu na mtu mwingine.

Taarifa hiyo ya Nida ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wake, Dickson Maimu, alipokutana na wahariri na waandishi wa habari, jijini Dara es Salaam, Mei 14, mwaka huu, kueleza sababu za kuchelewa kutoa vitambulisho vya taifa vilivyotarajiwa kuanza kutolewa mwanzoni mwa mwezi huu.

Kauli ya kuitaka Nida kutoa maelezo hayo, ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Edward Lowassa, wakati kamati yake ilipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.

Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alisema licha ya mkurugenzi mkuu wa Nida kukanusha taarifa hiyo baadaye, maneno aliyotumia wakati anakanusha, hayafanani na yale aliyotumia wakati anatoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari.

“Jambo la tatu linahusu maneno yaliyotolewa na vyombo vya habari kuhusu polisi na JWTZ. Ulikanusha lakini maneno (uliyotumia kukanusha) hayafanani na ya kwanza,” alisema Lowassa.

Siku chache baada ya kutoa taarifa hiyo na kutangazwa na vyombo vya habari, Nida ilitoa taarifa ikikanusha madai ya kubaini vyeti feki katika JWTZ na Polisi.

Katika tamko hilo, Nida ilisisitiza kuwa wao hawana uwezo wala mamlaka ya kubaini vyeti feki na kwamba, taarifa zilizotelewa na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari zilikuwa ni upotoshaji.

Hata hivyo, Lowassa alimpa Mkurugenzi Mkuu huyo wa Nida uhuru wa kuchagua kutoa maelezo hayo ama kwa kamati yake au mbele ya waandishi wa habari pia.

Akijibu hoja hiyo, Maimu alisema taarifa kuhusu suala hilo tayari alikwishaieleza kwa waandishi wa habari, hivyo akaomba kwa sasa aitoe kwa kamati hiyo.

Awali, akichangia mjadala kuhusu mradi huo, Mbunge wa Uzini (CCM), Muhammed Seif Khatib, alipongeza kwa kufanikiwa kutekelezwa hivi sasa tofauti na huko nyuma.

Alisema licha ya kuwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na pia baadhi ya mawaziri wengine waliowahi kuongoza wizara hiyo kabla na baada yake, walishindwa kufanikisha mradi huo kutekelezwa kutokana na kuwapo fitina nyingi.

Kauli hiyo ya Khatib iliungwa mkono na Mbunge wa Manyoni Mashariki (CCM), John Chiligati, ambaye naye alikiri kipindi alichoongoza wizara hiyo hakikuwezesha mradi huo kutekelezwa.

Chiligati alisema sababu kubwa ni kuwa mradi huo unahusisha fedha nyingi, hivyo kila aliyekuwa akitaka kupata zabuni ya kuutekeleza, alipoikosa, alianzisha fitina, ikiwamo kukimbilia mahakamani na kuukwamisha.

Hata hivyo, alisema vipindi hivyo vya fitina vimepita na kusema kinachotakiwa kwa sasa ni kufanya kazi ili kufanikisha mradi huo.

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji wa Vitambulisho, Joseph Makani, aliieleza kamati hiyo kuwa usajili wa watu mkoani Dar es Salaam litaanza rasmi mwezi ujao, baada ya mafunzo ya jinsi ya kuendesha zoezi hilo kwa watendaji wote wa mkoa huo na halmashauri zake zote.
 

tumpongeze IGP MANGU NI MTU makini hana doa ya rushwa ila tumwombee Mungu maadui wanaomchukia kazini ni wengi na mpaka amalize mda wake kila mtanzania atasifia jeshi la polisi.

Mangu ameruhusu askari wengi kujiendeleza kimasomo pia jeshi kwa sasa inaajiri vijana wenye taaluma

UTII WA SHERIA BILA SHURUTI
 

Good move ila isiwe nguvu ya soda.
 

Kagame alishngaa sana hiyo akajiuliza mwiziunampa muda arudishe??? Akaomba wiki.mbili akipewa tz anasafisha wizara zote nakurudikwao
 
askari wasio waadilifu wengi wametimuliwa kimyakimya sa hivi kupangiwa traffick watu wanaogopa sana maana mistake kidogo huna kazi

I hope pia kuna mipango mizuri ya kutumia teknologia kuongeza ufanisi. Pia kuwapa motisha askari waadalifu.
We are eagerly waiting to see.
 
Maadamu walishapata Mafunzo ya Uaskari na kufuzu na ukizingatia uhaba wa maaskari na sungura mdogo ambaye hataruhusu kuwezesha kurecruty wapya na kukwepa kutengeneza majambazi yenye utaalamu. Nashauri badala ya kuwafukuza wapewe fursa ya kujiendeleza pale walipokomea kihalali.
 
Rais ajaye ilianza kupanga safu ya wachapa kazi si wapiga siasa. Mangu ni chaguo mojawapo la Rais ajaye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…