MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 12,822
- 28,787
Habari JF,
Leo katika gazeti la Raia mwema kuna hii habari inayomhusu Askofu mstaafu Erasto Kweka wa KKKT anaegombea eneo la ekari 12 na binti wa ndugu yake bi. Mary Kweka. Kwa mijibu wa habari ni kuwa baba mzazi wa binti wakati wa uhai wake alimpa askofu shamba awe akilishia mifugo yake ila Askofu akajimilikisha mojakwamoja na mara baada ya kifo cha Baba Mary huyo askofu akaja na madai kuwa alishauziwa. Askofu alipoulizwa na mwandishi kuhusu hizo tuhuma alijibu sio kweli na huyo Mary sio mtu wa ukoo wao.
Binafsi nimepatwa na wasiwasi mkubwa kwenye uadilifu wa Askofu huyu aliyejipatia heshima kubwa. Ninaamini JF ina watu wengi wanaoweza kutuweka sawa katika hili.
Karibuni.