Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,101
- 25,973
Askofu Mkuu Mstaafu Erasto Ngatara kweka ameingia mgogoro mkubwa wa kugombea mali kati yake na binti yake.
Kulingana na gazeti la Raia Mwema(pg5 Machi 23 ,2016), Askofu Kweka anagombania shamba la eka 12 lenye thamani ya Tsh 220 milioni ambalo lilikuwa la marehemu ndugu yake Alexander Itaeli Kweka.
Mtoto wa marehemu Alexander Kweka(marehemu), anayeitwa Mary amedai,
"Ni kweli kwamba tuna mgogoro na Askofu Kweka kuhusu ene la shamba la familia kiasi cha ekari 12 ambazo amejimilikisha kinyum na sharia"
Mary katika hili anagombania moja kwa moja eneo hilo ambalo amesema ,Askofu Kweka alipewa(kwa kuazimwa) shamba hilo na marehemu baba yake, Alexander, kwa ajili ya mifugo mwaka 1991.
Anaendelea kudai, pamoja na Askofu Kweka kuwa kiongozi mstaafu wa KKKT ambalo yeye ni muumini wake, lakini pia Kweka ni sawa sawa na baba yake mzazi kutokana na msingi kuwa ni ndugu wa karibu wa baba yake mzazi.
Mtoto huyo ameenda mbali Zaidi na kudai Askofu Kweka ametoa hati za makubaliano za kuchukua shamba hilo ambazo hazina saini ya baba yao mzazi marehemu Alexander.
Na gazeti la Raia Mwema lilipo mwuliza Askofu Kweka juu ya tuhuma hizo, yeye alisema bint huyo ni "mwongo" na si sehemu ya familia ya Kweka.
Alipoulizwa juu ya tuhuma za kunga'nga'ania seheu ya shamba hlo Askofu kweka hakuwa tayari kueleza uhalali wa umiliki wake wala makubaliano na marehemu Alexander.
Sasa hiv suala hilo lipo kwenye hatua za kimahakama na sharia.
MY TAKE
Kweli Askofu kuukumbatia utajiri kutamfanya aukose ufalme wa kule Juu, pamoja na kulitumikia kanisa kwa miaka mingi.
Mbaya Zaidi inaelekea alichohubiri sicho anachokitenda.
Kweli itakuwa rahisi ngamia kupitia tundu la sindano kuliko mwenye mali tajiri anayependa mali zake kuingia mbinguni
UPDATE
Nawiwa kuomba radhi kutokana na habarii ambayo Askofu mwenyewe amejitokeza na jusema si ya kweli.
Amesema vilebvile yote yamefajywa jwa ridhaa ya familia yao na ukoo(magazetiji leo Daily News)