Ni mtazamo wangu, Sita hakustaili kugombea kupitia chama cha CCM kwa heshima aliyonayo kwa sasa katika nchi hii,si heshima ya kulazimisha bali inatokana na uwezo na umakini alionao katika kupambanua mambo pia ana uzalendo na nchi yake, chama kinachomfaa ni CHADEMA
Mimi nilijua walivyoanza kumunyoshea vidole wale mafisadi angesoma alama za nyakati kwa kukipiga chini CCM na kugombea kupitia chama makini, lakini nafasi bado anayo anaweza akapiga chini ubunge kitakachofuata ni kutangazwa kwa uchaguzi upya na yeye nina uhakika atalichukua lile jimbo kupitia CHADEMA tuongeze idadi ya wapiganaji , yule mama najua atapumua kwa taabu kwaza leo tu kachemsha