The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,906
- 2,885
Leo ni Karume day ambapo huwa sielewagi umuhimu wake kwa huku Tanganyika hadi kuifanya iwe mapumziko. Naona Rais pia kaamua kwenda kuhudhuria kumbukumbu ya mauaji ya halaiki huko Rwanda, nadhani ipo haja ya kuifuta hii siku kwa huku Tanganyika kwani inaongeza tu utitiri wa siku za mapumziko.
Swali la kujiuliza ni kuwa hivi huyo Karume hadi tumkumbuke alitufanyia nini hasa Watanganyika?
Swali la kujiuliza ni kuwa hivi huyo Karume hadi tumkumbuke alitufanyia nini hasa Watanganyika?
Rais Magufuli yupo nchini Rwanda akihudhulia maazimisho ya kumbukumbu zoa mauaji ya Kimbali yaliyotokea 1994. Ni kitu kizuri kinachoenesha mshikamano na jirani zetu kuonesha jinsi gani tumeguswa na maafa hayo makubwa.
Ikumbukwe pia leo ni maazimisho ya kumbukumbu ya kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa hili hayatiMzee wetu mwanamapinduzi Abeid Aman Karume.
Swali kwa Watanzania ni kwamba event ipi ni muhimu Kitaifa kati ya hizo mbili? Je haikuwa muhimu sana kwa Rais kuwa Zanzibar na kushirikiana na Wanzanzibari kuazimisha kifo cha Karume?
Je, ingekuwa kifo cha Nyerere, Magufuli angekwenda Kigali?
Mimi binafsi, msimamo wangu ni kuwa Rais amekengeuka. Natoa hoja.