Karume day ifutwe huku Tanganyika

Karume day ifutwe huku Tanganyika

Hapana! Hii haiko sawa i think, mie ni mfuasi mkubwa sana wa utumbuaji wa sikukuu za umma zisizo na tija ila hii naona bora ibaki tu kwa heshima ya Mama Tanzania.

Karume ni founding father wa TANZANIA kama alivyokuwa Nyerere, hakutakuwa na maana kuifuta Karume day alafu tuendelee kuwa Tanzania.

And the last thing, naona kuna hii tabia ya ubaguzi ambayo inazidi kuota mizizi kadri siku zinavyosonga! Ni kwanini tubaguane kwa utanganyika wetu na uzanzibari wetu?! Nyerere tunayemheshimu alikemea hilo kwa nguvu zake zote, kwann tusimuenzi kwa kuliishi hilo?!

Tukianza kuwabagua wazanzibar kwa uzanzibati wao na tukafanikiwa katika hilo basi tujue hatutoishia hapo, tutakuja kwabagua wahindi, wazungu, wachina na watu wa mataifa mengine, tukimaliza hapo tutaingia hadi kwenye makabila, rangi ya ngozi, urefu na ufupi, utajiri na umaskini and it will never end.

Dhambi ya ubaguzi huwa haina mwisho!

Wishing you all happy public holiday.
You are the great thinker!
ubaguzi si mzuri. kuna mtanzania mmoja yupo nje akasema yeye.siyo mtanzania eti Mzanzibari. mwalimu wake alikuwa na passport yake,.akampa ramani,.na kumwambia tafuta nchi yako. badaye akamwambia soma wewe achana na ujinga.
ndiyo haya. sisitupo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. hapo unazungumzia Karume na Nyerere. tunaweza kubadili nna ya kusherehekea ila kuwakumbuka ni muhim
 
Rais Magufuli yupo nchini Rwanda akihudhulia maazimisho ya kumbukumbu zoa mauaji ya Kimbali yaliyotokea 1994. Ni kitu kizuri kinachoenesha mshikamano na jirani zetu kuonesha jinsi gani tumeguswa na maafa hayo makubwa.

Ikumbukwe pia leo ni maazimisho ya kumbukumbu ya kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa hili hayatiMzee wetu mwanamapinduzi Abeid Aman Karume.

Swali kwa Watanzania ni kwamba event ipi ni muhimu Kitaifa kati ya hizo mbili? Je haikuwa muhimu sana kwa Rais kuwa Zanzibar na kushirikiana na Wanzanzibari kuazimisha kifo cha Karume?

Je, ingekuwa kifo cha Nyerere, Magufuli angekwenda Kigali?

Mimi binafsi, msimamo wangu ni kuwa Rais amekengeuka. Natoa hoja.
 
Toa fikila za kibaguzi, bado muunguno ni hazina kwa tanzania wazungu wamejaribu kuua huu muungano lakini weshindwa. Yule mzee alikuwa na akiri sana.
Ingekuwa vizuri ungezitaja faida maana kuna wengine hawazijui
 
Magufuli hapendi sherehe, yupo Rwanda anafanya connection zenye tija kiuchumi....ndio rais tunayemtaka....
kuhudhuria hiyo Rwandan genocide ni kama sehemu ya ku establish goodwill na Wanyarwanda ambao wana tija zaidi kwetu kiuchumi kuliko Zanzibar.
Zanzibar ni liability kwetu.

Zanzibar wangekubali kuwa mkoa ndani ya Tanzania basi, mambo yangekuwa simple sana
 
Haiwezi kufutwa kwanza mnakumbuka haikuwepo! Wazanzibari wakalalamika baada kuanzishwa Nyerere day kuwa mapumziko! Nao wanamuenzi Rais wao wa kwanza na Mwenyekiti wa Balaza la Mapinduzi! Ndani ya Muungano siku hiyo haiwezi kufutwa labda zifutwe zote 2.........(Nyerere day)


Kama vipi huko baharini wasi adhimishe Nyerere hatuwezi adhimisha sisi siku ya mvuvi(karume)
 
Kwani hakutoa hata tamko lolote kwenye ule ubao wenu almaalufu "sauti ya kisonge?" Nafikiri alishatimiza wajibu wake wa kumuenzi mzee Karume kwa vitendo kwa kuhakikisha Mapinduzi yanadumishwa kwa ccm kung'ang'ania madarakani,au kuna jema zaidi ya hilo?

Alishamuenzi Karume kwa kuhakikisha ccm inaendelea kutawala Zanzibar.
 
Leo ni Karume day ambapo huwa sielewagi umuhimu wake kwa huku Tanganyika hadi kuifanya iwe mapumziko. Naona Rais pia kaamua kwenda kuhudhuria kumbukumbu ya mauaji ya halaiki huko Rwanda, nadhani ipo haja ya kuifuta hii siku kwa huku Tanganyika kwani inaongeza tu utitiri wa siku za mapumziko.

Swali la kujiuliza ni kuwa hivi huyo Karume hadi tumkumbuke alitufanyia nini hasa Watanganyika?
Futa Muungano kwanza nayo itaondoka bila kupigizana kelele, venginevyo, ni budi kuivumilia tu hii siku.
 
hata mimi hushangaa WAZANZIBARI wanaposherehekea NYERERE day !
for what ?
mawazo ya aina hii huwa sielewi yanatoka wakati gani. mtu akiwa na akili zake au akiwa kapiga kiroba. kama ivo acheni vipigwe marufuku!
watu waache kujifikiria wao tu. huo ni moyo wa ubinafsi! bara kuna wapemba na wazanzibari kibao kama ilivyo huko,.wana enjoy uhuru wa kwenda na kurudi sababu ya wazee hao. wewe nani hata usijue umhimu wao! comment reserved!
 
Aache kwenda kujenga mahusiano ya kiuchumi achome mafuta ya ndege na misafara kwenda kuweka Maua kwenye kaburi? Watanzania watu maalum sana kwa kweli.
 
Kwani Zbar wanafanya nn cha ziada zaidi kwenda kwenye kaburi na kusoma dua? Amewakilishwa na Makamu w Rais wa JMT
 
Back
Top Bottom