hamjambo waungwana na JF, nianze kwanza picha nimeipenda na yenyewe tu ni habari tosha. watizame mawaziri walivyokaa, wasome nyuso zao, utabaini wale wanaojiamini na waoga, tuliache hilo. la karume, huu ni mwendelezo Salmin hakuwahi kukalia kiti chake kwenye baraza la mawaziri, na huyu wa sasa. Kiti wazi nalo ni tamko, 'kwamba hatukubaliani na utaratibu wa kumwengua rais wa Zanzibar katika muundo wa muungano'. Kabla ya mabadiriko haya rais wa zanzibar alikuwa makamu wa rais wa muungano, kwa utaratibu wa sasa hadhi yake imeshushwa, na ikumbukwe wazanzibari wakati huo pendekezo la kufanya mabadiriko haya ta sasa walipinga, bila kujali chama. lakini kisichojulikana mpaka leo ni ilikuwaje watawala wa zanzibar chini ya salmin wakaridhia badiriko ambalo hawakubaliani nalo. Huwezi kujua, huenda katika kiti hicho huketi ryhani!