Karume akacha kikao cha Baraza la Mawaziri

Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,330
195
Kiti chake kikiwa kitupu hapa

4559d1242370398-jmt-karume_mtoro.jpg
 
Karume huwa anakacha maana anakuwa kama anadhalilika....anakuwa mjumbe wa baraza la mawaziri...sawa na waziri yeyote yule....
 
Hivi huyu jamaa tunamhitaji kwa shughuli gani hasa? maana anaudhuru katika kila shughuli ya kimuungano.
 
Mdau,


Swali la kizushi: Kwanini, Mkuu ambaye siti yake ipo wazi hapo pembeni huwa haudhurii kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati nafasi yake ipo na Mafaili, Microphone, Kikombe cha Chai/Kahawa na Maji plus Kibao cha jina katengewa kabisa?

attachment.php
 

Attachments

  • Karume_Mtoro.jpg
    Karume_Mtoro.jpg
    61.9 KB · Views: 369
Mdau,


Swali la kizushi: Kwanini, Mkuu ambaye siti yake ipo wazi hapo pembeni huwa haudhurii kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati nafasi yake ipo na Mafaili, Microphone, Kikombe cha Chai/Kahawa na Maji plus Kibao cha jina katengewa kabisa?

Kaazi kwelikweli Tanzania... Kila kukicha na chemshabongo mpya!!
 
Very interesting topic. Alafu utasikia ooh muungano UMEIMARIKA hauna shida yeyote wanoujadili ni wavunjaji muungano. Kaazi kweli kweli.
 
Sio Karume tu, Hata kama ingekuwa wewe binafsi Umebaini washirika wenzio wanakutumilia kwa maslahi yao na kutumiajina la Ukoo wako kwa kukamilisha malengo yao nadahni usinge endelea na ushirikiano wa aina hiyo, hayupo tayari kuwa fulishi tena na kupakwa mafuta kwa nyuma ya chupa kama wanavyo tumia msemo huo hapa zanzibar
 
...sasa huu ni utovu wa nidhamu. Hali ya hewa inachafuka siku ya Muungano, na siku ya vikao tu? :mad:
 
hamjambo waungwana na JF, nianze kwanza picha nimeipenda na yenyewe tu ni habari tosha. watizame mawaziri walivyokaa, wasome nyuso zao, utabaini wale wanaojiamini na waoga, tuliache hilo. la karume, huu ni mwendelezo Salmin hakuwahi kukalia kiti chake kwenye baraza la mawaziri, na huyu wa sasa. Kiti wazi nalo ni tamko, 'kwamba hatukubaliani na utaratibu wa kumwengua rais wa Zanzibar katika muundo wa muungano'. Kabla ya mabadiriko haya rais wa zanzibar alikuwa makamu wa rais wa muungano, kwa utaratibu wa sasa hadhi yake imeshushwa, na ikumbukwe wazanzibari wakati huo pendekezo la kufanya mabadiriko haya ta sasa walipinga, bila kujali chama. lakini kisichojulikana mpaka leo ni ilikuwaje watawala wa zanzibar chini ya salmin wakaridhia badiriko ambalo hawakubaliani nalo. Huwezi kujua, huenda katika kiti hicho huketi ryhani!
 
Wakurya wana utaratibu wa kukaa kwa matabaka,wakati wa majadiliano. Wenye mke mmoja hukaa tofauti na wale wenye wake wawili. Wenye wake watatu nao hukaa tofauti na wenye wake wanne nk. Karume kwa hadhi yake ni sawa na mtu mwenye wake wengi. Kwanini akae na watu wasio na hadhi kama yake?
 
Back
Top Bottom