Karudi Baba Mmoja (Toleo Jipya)

Umenikumbusha mbali sana. Wakati huo tuliweza kuliimba shairi hili hata kabla ya kuanza shule ni kama hadithi ya Juma na Rose au Tumbo niache nimuachie manenge.
Hadithi ya Juma na Rose niliikariri kabla sijaingia shule siku ya siku Mwalimu kanambia nisome mimi nikatiririka tu. Anistopisha akasema nioneshe maneno "tia chai Rose" hapo ndipo nilipoabika mbele ya darasana maana nilikuwa sijui hata moja.
Niliondoka na bakora nne. Mimi nafuta sana kitabu hiki na kama unastori zake zishushe humu. Jana jioni nilikuwa naongea na wife kuwa nitashuka JF kuomba shairi hili kwa wana JF. Kabla sijaomba nafungua tu nakuta bombii nyumbii. Hizo ndizo nyakati shule iliopkuwa shule au elimu ilipokuwa elimu sio sasa eti mtoto anafaulu darasa la saba akiwa hajui kusoma wala kuandika au wakati huu unapoweza kukutana na waziri anayekwambia Tanzania ni muungano wa visiwa vya Zimbabwe na Tanganyika mwaka 1964.
Kuna nyingine kama Jogoo aliyesema, Kibanga kamapiga mkoloni, Sizitaki mbivu hizi na zile za wagagagigikoko! Vitabu vya enzi hizo vinapatikana wapi? bila kusahau Hekaya za Abunwasi.
Nadhani ungesema wadau wa kizazi chetu cha Analojia sio digitali. Digitali si ndio hawa wanaopanuliwa magoli ili wafunge kwa urahisi? Matokeo yake wanafaulu wakiwa hawajui kusoma na kuandika wakiingia kwenye mitihani wanachora mazombi na kutukana!
 
Duh! We jamaa, hili shairi umekariri au umelikopi toka kwenye kitabu? Maana ulivyotiririka!
Lakini mimi huwa nashindwa kuelewa lipi maarufu zaidi kati ya hili na lile la jingine la
"Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia..."
Hayo yote mkuu naoana ngoma droo. Lakini vitu vya zamani vyote vilikuwa vikali ni vigumu kuamua kipi cha kwanza na cha pili. Sasa hivi hovyo kabisa hata watoto hawana wanachozungumza au kukikariri baada ya shule.
 
Ha ha kweli yaaani nilivyokuwa nafungua huu uzu nilikuwa nalisema hili shairi
 
Asiye jua kusoma ni mjinga kabisa,barua ikija aitembeza kutwa'..hii nyimbo ilinifanya nifanye juhudi zote ili nijue kusoma..darasa la kwanza na la pili,mwalimu wetu alikuwa anatuita mbele mmoja mmoja kusoma kwenye ubao...ukishindwa,wenzako wanakuimbia hiyo nyimbo,halafu wanakuzomea..dah
 
'asiye jua kusoma ni mjinga kabisa,barua ikija aitembeza kutwa'..hii nyimbo ilinifanya nifanye juhudi zote ili nijue kusoma..darasa la kwanza na la pili,mwalimu wetu alikuwa anatuita mbele mmoja mmoja kusoma kwenye ubao...ukishindwa,wenzako wanakuimbia hiyo nyimbo,halafu wanakuzomea..dah

Kweli kabisa mkuu. Nyakati zile pamoja na mazingira magumu walimu walijitahidi sana kuweka vihamasisho vingi sana vya kufanya wanafunzi kuelewa na kulipenda somo lakini bila kusahau mikwaju ya kutosha.
Kwenye hesabu mwalimu akiingia mkisimama kumsalimia cha kwanza ni table. Na alikuwa anaweza kuanza na table yoyote mfano tabe ya 3 ya 5 au ya 9. Kila anayepatia ndiye anakaa na anyekosa ni mikwaju.
Ile ilifanya kila mwanafunzi kufanya mazoezi ya kutosha asije pata mikwaju.Hata daftari tulikuwa tunanunua zenye table kwenye jalada la nyuma.
Vivyo hivyo kwa masomo mengine. Sasa hivi wazazi wanakwenda shuleni kupambana na walimu watoto wao wanapochapwa. Leo hii watoto mbumbu mzungu wa reli ndio wanachaguliwa kwenda sekondari. Wakati ule mtu akichaguliwa kwenda sekondari ilikuwa ni issue ya kijiji kizima au wilaya.
Sasa hivi tunaambiwa wanafaulishwa badala ya kufaulu wenyewe. Sasa hivi tunaambiwa wilaya moja huko Rukwa wanafunzi walioandikishwa kufanya mtihani wa darasa la saba wako 4200 lakini 2200 hawajui kusoma wala kuandika. Sasa hao ndio utasikia wamefaulu kwenda sekondari na msemaji kwa mbwembwe utamsikia akisema, "...wilaya yangu imefaulisha zaidi ya asilimia 95 hivyo kuvuka lengo" Nchi kiellimu ni kwishney. Elimu ilikuwa wakati wa Nyerere tu.
Unakumbuka wakati ule somo kama Sayansi kimu tulikuwa tunajifunza halafu baadaye tunafanya kwa vitendo mfano kufua, kushona, kupika chakula shuleni kadiri mwalimiu alivyofundisha aina za vyakula na vitamini na kupiga pasi. Leo watoto hawajui hata kushona kifungo cha shati sembuse kupiga pasi? Ukikumbuka sana unaweza kulia!
 
nakumbuka nishaimbaga huo ubeti wa kwanza mbele ya mtu mzima ile kutamka neno mapaja tu nilipokea kwenzi la kichwa nikaishia hapohapo eti kwanini niseme mapaja,?????
 
Wow asante sana! Nimesika baadhi ya beti nikawa nina hamu kupata zliizobaki!
 
Duh! We jamaa, hili shairi umekariri au umelikopi toka kwenye kitabu? Maana ulivyotiririka!
Lakini mimi huwa nashindwa kuelewa lipi maarufu zaidi kati ya hili na lile la jingine la
"Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia..."
Aisee hata mi nimeshindwa kutoa jibu ni lipi lilikuwa maarufu.
 
Yaani hili shairi nalijua kuliko wimbo wa taifa au ule wa Tanzania...natamani nimjue mtunzi wake maana alitumia akili sana
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom