Karudi Baba Mmoja (Toleo Jipya)

Ili lilikua linanitoa machozi,,dah

Mie bado nalia..marehemu baba yangu wakati huo alikuwa kijana..akawa anapenda sana kutumbusha ujumbe wa shairi lile!

Du! Enzi za mwalimu tulilelewa, kila somo ni kujenga jamii yenye akili tu!
 
Daaaah vitu vingi vinanipitia kichwani sijui wanetu wa sasa Kama wanafaidi kama ilivyokuwa kwetu
 
yaaaya yaya! nalikumbuka enz hizo anatafutwa mja anaye jua kusoma vzuri afu anasomea nyie mnamfuatiliza kwa nyuma dah afu shair zuri kwel na ujumbe wake pia unamana
 
Hili shairi umenikumbusha mbali sana,tulipigwa ndani ya wiki kila mtu alikuwa anachana mistari kama hana akili nzuri.Chezea kipigo weye!



Mkuu pole sana kwa vichapo,mimi shairi hili nililikariri nikiwa darasa la pili wakati huo dada yangu yupo darasa la nne na kila akirudi nyumbani yeye ni kuimba tu na mimi ndipo nikamsumbua mama yangu mpaka akanifundisha.Adhabu yangu ilikuwa ni kusubiri mpaka nifike darasa la nne ili na mimi nikamuimbie mwalimu na siku zilikuwa haziendi....
 
hahahaaaaaaa, umenkumbusha mbali, nakumbuka nlivyokuwa namuimbisha mama angu baada ya mie kujua kuliimba ye akawa denti wangu
Big up mama
 
NI mojawapo ya mashairi ambayo wengi waliosoma shule za msingi za umma za Tanzania watakuwa wanalikumbuka; lilianza hivi:

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?

4.
Baba aliye kufani akajibu lile swali
Ninakufa maskini baba yenu sina hali
Neno moja lishikeni kama mnataka mali
Kama mnataka mali mtayapata shambani

5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali

baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,

fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,

mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili.

Wakakata na shauri, baada ya siku mbili.
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali.

Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali.
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.


10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali.

Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali.
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani

11. Wakanunua na ng’ombe, majike kwa mafahali.

Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli.
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.


12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali.

Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali.
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli.
“KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI”.


Mtunzi... x,y






 
Na leo watakwambia kilimo kwanza, matrekta kibaaao yanaoza pale dodoma mtanzania wa kawaida ataweza wapi,pesa zinaishia mwa mawakala wa pembejeo, elimu ilikuwa wakati ule bwana!
 
Back
Top Bottom