Karudi Baba Mmoja (Toleo Jipya)

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Karudi baba fulani, toka safari ya nje
Kavimba yote maini, na kucheua punje
Wanae wakaleta ubani, ili kuepua njenje
Wakataka na madini, yawafae nje nje

Akatamka mtumbua, nimevimbiwa kwelikweli
Hata mkinitumbua, sitatapika nje nje mali
Roho yaniumbua, uhai waniacha dhalili
Kama mnataka vitumbua, mjiunge na serikali

Wakazidi kumdodosa, baba alopoteza imani
Baba yetu mwanasiasa, mbona unatupa deni
Akili zetu za kudesa, hazijajua yaliyo sirini
Kama tunataka pesa, tutapataje chamani?

======

NB: Vina na Mizani vitapangwa baadaye...


Ahsante kwa madongo!, na kwao kuwafikia!
Umewapinga vigongo, na sisi twashangilia
Wanatuvunja migongo, na wao wajinonea
Mfano wao vibwengo, na damu watunyonyea!

Wanajiita vigogo, ugogo wa kudokoa
Wanatugea vichogo, wakati wajishibia
Wala kidogo kidogo, na buyu wamalizia
Mfano wao vibwengo, jasho letu washibia

Watavifunga virago, na hilo naashiria
Watuwachia mihogo, maharage na bamia
Wajifanya kama mbogo, kwa wao uharamia
Mfano wao vibwengo, watoto watuulia!

 
Hii ni proper kabisa
ni safari, per diem, tungi, misosi, mafolder, excess luggage na nothing added when coming back to work except pending issues
 


Ahsante kwa madongo!, na kwao kuwafikia!
Umewapinga vigongo, na sisi twashangilia
Wanatuvunja migongo, na wao wajinonea
Mfano wao vibwengo, na damu watunyonyea!

Wanajiita vigogo, ugogo wa kudokoa
Wanatugea vichogo, wakati wajishibia
Wala kidogo kidogo, na buyu wamalizia
Mfano wao vibwengo, jasho letu washibia

Watavifunga virago, na hilo naashiria
Watuwachia mihogo, maharage na bamia
Wajifanya kama mbogo, kwa wao uharamia
Mfano wao vibwengo, watoto watuulia!
 
That's really, hii kweli inatuonesha jinsi hata wazee wetu zamani kama walikuwa wanakwenda mbali bado walikuwa wanatuachia wosia wa Wapi mali tutapata. Maana baba kwenye hadithi hii baada ya kuzunguka nchi zote au sehemu zote lakn alikiri kuwa mali inapatikana shambani tu!

Ujumbe kwetu:
Marekani, Uingereza, Uturuki, China, Kenya n.k. Sio suluhisho la matatizo yetu! Suluhisho letu ni kulima kahawa, pamba, pareto, mpunga, mahindi, ulezi n.k. na kuyachakata/processing mazao hayo hapa nchini na kuuza nje ziada! Vingenevyo ni kufukuza upepo
 
Karudi Baba Mmoja (Toleo Asilia) hili hapa:

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?

Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.

Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.

Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
wote wakashangilia, usemi wakakubali,

"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".
 
karudi baba mmoja (toleo asilia) hili hapa:

karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?

Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.

Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.

Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
wote wakashangilia, usemi wakakubali,
"kama mnataka mali mtayapata shambani".

chanzo: http://issamichuzi.blogspot.com/2008/11/salamu-toka-dodoma.html

kilimo kwanza
 
Hilo shairi la karudi baba mmoja wengine linatuklumbusha mbali, enzi ile kulipokuwa na malenga mashuhuri sana, au gurus walioumia vichwa kutoa ujumbe.

Nlaifananisha na sizitaki mmbichi hizi.
 
Karudi baba fulani, toka safari ya nje
Kavimba yote maini, na kucheua punje
Wanae wakaleta ubani, ili kuepua njenje
Wakataka na madini, yawafae nje nje

Akatamka mtumbua, nimevimbiwa kwelikweli
Hata mkinitumbua, sitatapika nje nje mali
Roho yaniumbua, uhai waniacha dhalili
Kama mnataka vitumbua, mjiunge na serikali

Wakazidi kumdodosa, baba alopoteza imani
Baba yetu mwanasiasa, mbona unatupa deni
Akili zetu za kudesa, hazijajua yaliyo sirini
Kama tunataka pesa, tutapataje chamani?
-----------------------------------------------------

Vina na Mizani vitapangwa baadaye....

Endelazea hapa.

Kwanza sambaratikeni, nawapa huo wosia
Mali jilimbikizieni, siri msiwaambie
wakilalama washitini, Na msije wasikia,
kuleni vyenu sirini, na wanenu limbikizia

Chukua Chako Mapema, ndiyo sera za CCM
Muwaonapo wahema, kuomba kura CCM
Wakipata ni neema, mtaji wao CCM
Tujipangeni mapema, mpeje kura CCM

Misingi wameivunja, kwa wao ubinafsi
Urahisi kujiwekea, mali kuzibinafsi
Ni wapi tutaanzia, imarisha zetu nafsi
Nchi inateketea, kwa msingi binafsi

Zamani tulijifunza, kuwa cheo ni dhamana
Madili tulijifunza, tuweze shika dhamana
Tumebakia mafunza, yasiyojua dhamana
Nani aje kutufunza, tuirudishe dhamana




 
Endelazea hapa.

Kwanza sambaratikeni, nawapa huo wosia
Mali jilimbikizieni, siri msiwaambie
wakilalama washitini, Na msije wasikia,
kuleni vyenu sirini, na wanenu limbikizia
Natamani baada ya mstari wa kwanza ungefuata mstari huu
"zugeni mu ugomvini, wasijue mu wamoja,
 
Natamani baada ya mstari wa kwanza ungefuata mstari huu
"zugeni mu ugomvini, wasijue mu wamoja,

Umesomeka FM, Inaleta akili hii

Kwanza sambaratikeni, nawapa huo wosia
"zugeni mu ugomvini, wasijue mu wamoja,

Mali jilimbikizieni, siri msije wambia
wakilalama washitini,
na wanenu limbikizia,

Chukua Chako Mapema, ndiyo sera za CCM
Muwaonapo wahema, kuomba kura CCM
Wakipata ni neema, mtaji wao CCM
Tujipangeni mapema, mpeje kura CCM

Misingi wameivunja, kwa wao ubinafsi
Urahisi kujiwekea, mali kuzibinafsi
Ni wapi tutaanzia, imarisha zetu nafsi
Nchi inateketea, kwa msingi binafsi

Zamani tulijifunza, kuwa cheo ni dhamana
Madili tulijifunza, tuweze shika dhamana
Tumebakia mafunza, yasiyojua dhamana
Nani aje kutufunza, tuirudishe dhamana
 
UBETI WA 4 WA TOLEO JIPYA

Kwanza kaukasini, nawapa hilo dili
Kutaneni kule mjengoni, kisha mjilipe bili
Haya sasa kwaherini, mauti yanikabili
Kama mwataka kuwini, kiukeni maadili
 
Harudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Harudi hata kiroja, bali kifo cha ambari
Harudi mbaba soja, na si sababu ya mali
Tanzania ya bazazi, arudi kufanya nini?

Baba alivyoondoka, katu hakutaka rudi
Alivyokwishachomoka, kurudi katu kwa budi
Nasema si kuropoka, kurudi hata kwa udi
Ufisadi wazi wazi, arudi kufanza kipi?

Kwanza kutokake zengwe, hata pasi kuipata
Vichaa ka wa Mirembe, wajaliwa uambata
Waruka wabemba bembe, bila senti katakata
Nyumbani hakuna kazi, arudi kufanza kipi?

Miaka yake yapita, nadhiri bado akiri
Ughaibu kajikita, kama hanazo akili
Bi Mkubwa amuita, imani yamuajiri
Tanzania ya makadhi, arudi kufanya nini?

Tanzania ya makadhi, ustaadhi wenye mahadhi
Ya milioni makazi, kimarekani si nazi
Sembuse tuso jahazi, wala mtumbwi wa Chazi
Tanzania ya maPazi, arudi kufanya nini?
 
Mwankijiji uko wapi aisee......naona wakuu hapa wameshakuchokoza.......ngoja nami nikajifue kidogo.....later
 
UBETI WA 5 WA TOLEO JIPYA

Alipokwisha watonya, misingi hii ya kifisadi
Pesa zikashindwa mponya, akageuka samadi
Na warithi wakampokonya, malize kwa ukaidi
Kama mwataka jichanganya, kuweni mahasidi
 
Wadau hebu tukumbushane enzi zile za mashairi ya primary (nadhani ni darasa la nne):

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishani.

Kwa wenye kumbukumbu nzuri hebu ongezeeni beti zinazofuata. Samahani hii ni kwa wale waliosoma St. Government. Kwa mliosoma Intaneshino skuli sidhani kama mlikutana na kitu hii
 
Wadau hebu tukumbushane enzi zile za mashairi ya primary (nadhani ni darasa la nne):

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishani.

Kwa wenye kumbukumbu nzuri hebu ongezeeni beti zinazofuata. Samahani hii ni kwa wale waliosoma St. Government. Kwa mliosoma Intaneshino skuli sidhani kama mlikutana na kitu hii

baba alie kufani, akajibu lile swali
ninakufa masikini, baba yenu sina hali
neno moja lishikeni, kama mnataka mali
kama mnataka mali, mtayapata shambani

wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,


jamani ni siku nyingi bwana, akili imejaa mambo mengi sana nitarudi later kumalizia
 
baba alie kufani, akajibu lile swali
ninakufa masikini, baba yenu sina hali
neno moja lishikeni, kama mnataka mali
kama mnataka mali, mtayapata shambani

wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,


jamani ni siku nyingi bwana, akili imejaa mambo mengi sana nitarudi later kumalizia

Mimi nakumbuka mistari hii michache;

akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli
hatakama nikichanjwa, haitoki homa kali
roho naona yachinjwa, kifo kimenikabiri
kama mnataka mali, mtayapata shambani

Zamani sana mkuu, si rahisi kukumbuka mambo haya
 
the good ol' days... nakumbuka ya Sungura...

Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja leo ninakuletea
alitoka siku moja njaa alipo sikia
njaa aliposikia sungura nakwambia

Siku ile akaenda porini kutembelea
akayaona matunda mtini yameenea
sungura akayapenda mtini akasogea
mtini akasogea sungura nakwambia

zilikuwa kama beti sita hivi, nimesahau nafikiri inaendelea hivi au kuna beti nimeziruka...

karuka tena karuka matnda hakufikia
mwisho wake akachoka kachoka hata mkia
penye mti akatoka pembeni akasogea
pembeni akasoge sungura nakwambia

sizitaki mbichi hizi sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
matunda akalilia sungura nakwambia
 
anayeijua ile story ya sadiki aliyekimbilia mjini kutafuta kazi aiweke hapa wajameni....maisha yalivyomshinda town karudi na viraka vya nguo.
 
sikumbuki hiyo ya Sadiki lakini nakumbuka hii nyimbo...

Mkulima mwenye shamba alipanda viazi
akachimba chimba chimba akaona almasi
lo lo lo bahati ya mtu mwenye shamba
akatupa jembe upande akaenda mjini
kununua motokaa sasa ni tajiri
lo lo lo bahati ya mtu mwenye shamba!
 
Back
Top Bottom