Karudi Baba Mmoja (Toleo Jipya)

Sikiri mimi masikini, uvivu wangu nyumbani
Ukiwa huu njiani, nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba, chakula kingi kwa baba
..............................................................malizieni mnaojua

Mambo yalikuwa mazuri enzi hizo chini ya nidhamu ya ujamaa na kujitegemea wa Mwl na timu yake!!
 
Je, na hivi vitabu vinaweza patikana wapi? Hakuna anayeweza kuscan vitabu hivi?

Hebu jaribu kwenye duka la vitabu pale ilipokuwa shule ya upili ya forodhanikuna duka la kanisa katoliki nasikia vinapatikana hapo
 
Ngoja nikuimbie kidogo

1.Sungura afahamikaa ujanja kujijazia
Wenzake wanamcheka sungura huwazomea
Ila siku ikafika ya sungura kuumia
Ya sungura kuumia sungura nakuambia!

2.Siku hiyo akaenda shambani kutembelea
Akayaona matunda mgombani yamejaa
Sungura aliyapenda mgombani kasogea
Mgombani kasogea sungura nakuambia

3.Sungura karukaruka lakini hakufikia
Matunda hakuyashika mkononi kuyatia
Hakika alisumbuka nguvuze zikapungua
Nguvuze zikapungua sungura nakuambia

4.Yakamtoka machozi matunda akalilia
Matunda akalilia sungura nakuambia
Sizitaki mbichi hizi sungura kajisemea
Naona nafanya kazi bila faida kujua!

hivyo yani Kama nimekosea nirekebisheni

nimecheka mpaka machozi yamenitoka ubeti wa kwanza na wa pili
 
Ngoja nikuimbie kidogo

1.Sungura afahamikaa ujanja kujijazia
Wenzake wanamcheka sungura huwazomea
Ila siku ikafika ya sungura kuumia
Ya sungura kuumia sungura nakuambia!

Hiyo itakua tolea la pili...

Yetu ilianza hivi
1. Hadithi inayokuja, ni Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, sasa ninakuletea,
Alitoka siku moja njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia.

2. Siku hiyo akaenda, porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia
 
NI mojawapo ya mashairi ambayo wengi waliosoma shule za msingi za umma za Tanzania watakuwa wanalikumbuka; lilianza hivi:

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?

4.
Baba aliye kufani akajibu lile swali
Ninakufa maskini baba yenu sina hali
Neno moja lishikeni kama mnataka mali
Kama mnataka mali mtayapata shambani

5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali

baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,

fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,

mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili.

Wakakata na shauri, baada ya siku mbili.
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali.

Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali.
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali.

Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali.
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani

11. Wakanunua na ng’ombe, majike kwa mafahali.

Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli.
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali.

Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali.
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli.
“KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI”.

Mtunzi... x,y

gosh!you made me remember when we used to scramble for one book at my old school
 
NI mojawapo ya mashairi ambayo wengi waliosoma shule za msingi za umma za Tanzania watakuwa wanalikumbuka; lilianza hivi:

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?

4.Baba aliye kufani akajibu lile swali

Itakua vizuri sana ukiweka na lyrics za ile shairi la "majira yetu haya yangekuaje sasa,utumwa wa nchi..."

1. Tazama ramani utaona nchi nzuri,
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania.

Majira yetu haya yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi Nyerere Ameukomesha.

2. Chemchemi ya furaha ama nipe tumaini,
Kila mara kwako niwe nikiburudika,
Nakupenda hasa hata nikakufasiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.

Majira yetu haya Yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha.

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde nami nikulinde hata kufa.

Majira yetu haya yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi Karume ameukomesha.

Kama nimekosea mahali wadau mnisaidie kurekebisha.

Wimbo huo unapatikana katika kitabu cha darasa la tano (cha zamani) Kiitwacho "TUJIFUNZE LUGHA YETU" KITABU CHA 7, Sura (Chapter) ya 29 iitwayo "REDIO TANZANIA, DAR ES SALAAM". Nilikisoma mwaka 1989.
 
NI mojawapo ya mashairi ambayo wengi waliosoma shule za msingi za umma za Tanzania watakuwa wanalikumbuka; lilianza hivi:

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?

4.
Baba aliye kufani akajibu lile swali
Ninakufa maskini baba yenu sina hali
Neno moja lishikeni kama mnataka mali
Kama mnataka mali mtayapata shambani

5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali

baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,

fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,

mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili.

Wakakata na shauri, baada ya siku mbili.
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali.

Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali.
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali.

Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali.
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani

11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali.

Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli.
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali.

Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali.
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli.
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".

Mtunzi... x,y

By the way, hivi kipindi kile kulikuwa na shuke za msingi zisizokuwa za umma? nahisi wote waliosoma enzi hizo lazima walizipiga hizo verse.
 
Duh!enzi za brown ashika tama au chilunda apambana na chui achilia mbali lindu amuokoa kapilima.hizo siku nzuri za zamani tunanyolewa kipara ngoto
 
1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani? (P.T)

4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli,
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".
 
Back
Top Bottom