TPP
JF-Expert Member
- Mar 18, 2023
- 650
- 782
Thread hii ni maalumu katika kuelezea na kutambua mchango wa wanafalsafa mbalimbali wa kiuchumi au kisiasa katika dunia hii ya usasa.
Ruksa member yoyote mwenye uelewa na ufahamu kuhusu mwanafalsafa wa kiuchumi au kisiasa anaye mfahamu kumuelezea humu.
Binafsi yangu nitaanza na hawa wawili maarufu, Karl Marx na Adam Smith
Karl Marx
Huyu ni mwanafalsafa maarufu katika masuala ya uchumi na siasa mchango wake mkubwa binafsi nautambua zaidi katika mageuzi ya kisiasa katika mataifa mbalimbali duniani
Sehemu kubwa alipo fanikiwa zaidi Marx mpaka sasa ni kwenye mageuzi ya kisiasa
Vitabu vyake maarufu duniani ni Das Kapital na The communist manifesto.
Maarufu zaidi ni "The communist manifesto" kilicho andikwa kwa ushirikiano na mwanafalsafa mwenza wa kijerumani Frederick Engels hiki ndicho kitabu kilicho leta mageuzi makubwa sana katika mataifa mbalimbali
Adam Smith
Bwana Smith yeye alikuwa mwanafalsafa na mtaalamu wa masuala ya uchumi, asili yake ni uskotishi.
Bwana Smith mchango wake unatambulika zaidi duniani kupitia mawazo yake kuhusu dhana nzima ya uchumi bora ndani ya kitabu chake maarufu zaidi cha " The Wealth of Nations"
miongoni mwa vitabu vyake maarufu ni pamoja na The Wealth of Nations na The theory of moral sentiments.
Mchango wa Smith katika dunia ya sasa ndani ya mataifa mbalimbali umejikita katika masuala ya uchumi au mageuzi ya kiuchumi katika mataifa mbalimbali duniani.
Smith ni mshindi wa mageuzi ya kiuchumi wakati Marx yeye ni mshindi katika mageuzi ya kisiasa/tawala katika dunia ya usasa.
N.b Taja au muelezee mwanafalsafa yoyote mtaalamu wa masuala ya uchumi au siasa unaye mfahamu sio lazima Marx na Smith.
Ruksa pia kuweka picha, documents, Quotes, machapisho, vitabu n.k kumuhusu huyo mwanafalsafa.