Mkuu Mkeshaji, kwa vile unaamini Dr. aliibiwa kura, hivyo kila ambaye sio Chadema basi ndio mwizi wenu?!.
Wanatakiwa waache ubaguzi, wanaJF tushikamane kama walivyoshikimana viongozi wao katika msiba japo sijajua kama jamaa leo alitoa mkono. Hata hivyo hojatete akishapumzika kidogo atatujuza tu najua alikuwa na kazi nzito pale Karimjee.
Jibu langu lili-reflect statement yako...
Ilionesha mambo manne ama zaidi ndani yake:
1. JF ni ya chadema (membaz wa chadema). Hili uongozi wa jf ulishalikanusha tangu katibu mwenezi wa chama chenu alipotoa tuhuma kama hizo.
2. Memba wa jf huwa wanahudhuria kwenye misiba ya membaz wenzao tu (hata kama ni kweli sioni tatizo hapo)
3. Msiba ukiwa ni wa mwanachadema basi wanachadema lazima wahudhurie (hili pia sioni tatizo lake)
4. Ukiona watu maelfu kwa maelfu wamehudhuria msibani basi ujue kuwa aliyekufa ni mwanachadema.
Hiyo ya nne ndo iliyonifanya niamini kuwa kweli Dr. Slaa aliibiwa kura. Kama wanachadema wanaweza kujitokeza kwa wingi namna ile kwenye msiba ni wazi kuwa kwenye uchaguzi ni vivyo hivyo kwani nchi yetu sasa hivi ni kama ipo msibani, na kama umati huo wote una mapenzi na chadema ni aglabu watu hao wataichagua chadema. na kama wameichagua chadema halafu eti haikushinda...kura zimeenda wapi?
Na kwa kuwa nimeona mara nyingi ukiikejeli chadema na ukijiweka karibu na magamba, nakuchukulia kuwa wewe ni mmoja wao.
Kama wewe ni dereva wa taxi, majambazi watatu wakakukodi mkafanye uhalifu, askari wakiwatia mbaloni watasema tumekamata majambazi wanne.
Mkuu Molemo,
Upo! wachangiaji wamejaa kule kwenye thread ya kuchukuwa jimbo la Sumari ya wana Chadema
Kumbukeni kuwa leo ni jumamosi na kwa wafanyakazi wengi leo ni siku ya mapumziko.
Siku ya kumuaga marehemu Regia ilikuwa ni siku ya kazi hivyo watu wengi walichangia kupitia makazini.
Watu wengi huwa wana-access internet huko makazini kwao na hawana access hiyo majumbani.
Usitarajie kupata wachangiaji wengi katika hali kama hiyo.
Pasco,
Kwenye msiba hatuna CCM,CHADEMA,CUF,NCCR-Mageuzi,UDP n.k......Kwenye msiba tunakuwa wamoja.....
Kwenye msiba tunaweka tofauti zetu pembeni na kuwa wamoja kama watanzania....
Mkuu Ritz Usinchekeshe!
Mkuu Molemo,
kuna thread "Pendekezo: Slaa amrithi SUMARI Arumeru"
Hakuna cha msiba tena, msiba ulikuwa wa Regia Mtema tu.
Ebu tueleze wengine huwa tunasikia tu... Hivi kura huwa zinaibiwaje?
Mkeshaji nimenusa pointi yako hapa
Mkuu Molemo,
kuna thread "Pendekezo: Slaa amrithi SUMARI Arumeru"
Hakuna cha msiba tena, msiba ulikuwa wa Regia Mtema tu.
Hojatete usikimbie tuletee picha humu