Karibuni tujifunze: Question tags

Sheillah Sheillah

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
583
1,478
Question tags, ni maswali mafupi mwisho wa sentensi. Tunatumia question tags pale ambapo tunategemea msikilizaji au msomaji kukubaliana na maelezo yetu. Mfano isn't it?, can you? wasn't it? Have they? Nakuendelea

Ili kuweza kutengeneza hizi question tags inabidi ujue kama sentensi ni "positive au negative statement". Kama statement ni positive tunatumia question tag ya negative na kinyume chake ni sahihi.

Mfano, She is a teacher, isn't she?
"She is a teacher" ni positive statement hivyo question tag yake lazima iwe negative "isn't she"?

She isn't a teacher, is she?
She isn't a teacher ni negative statement, na "is she" ni positive tag

Kuna wengine wanajiuliza watajuaje kama wanatakiwa watumie Isn't she, didn't she, wasn't it? Njia ni rahisi.

Unaangalia kama kuna auxiliary verb katika hiyo sentence mfano (be, have, do, is, etc), au model verb kama (could, can, should, etc.).

Mfano
She is a teacher. Is ni auxiliary verb . Kwahiyo ili kukanusha unatumia hiyo "is"= isn't she?
He wasn't relaxed, was he?
We must go, mustn't we?

Au pia sentence unaweza ikawa ina verb tu. Verb ni kitendo. Hapa tutatumia (don't kwa wakati uliopo, doesn't kwa wakati uliopo ila kwa " he ,she, na it" na didn't kwa wakati uliopita).

Utaangalia hiyo verb ipo kwenye wakati gani.

Kwa mfano,
You speak English . Hapo speak ni verb na ipo katika wakati uliopo. Hivo utatumia " don't you"?
Kama verb ingekuwa wakati uliopita tungetumia "didn't you"?

I said that already, didn't I? " said" ni verb ya wakati uliopita ndio maana tunatumia didn't.
Juma eats food, doesn't he? Tunatumia doesn't kwa sababu Juma ni sawa na "he" ambayo ni "nafsi ya tatu umoja" na pia statement ipo katika wakati uliopo

Lakini kuna question tags zisizofuata kanuni zilizokwisha andikwa hapo juu.

Kwa mfano,
1.Question Tag ya I am ni "aren't I". Eg, I am a teacher, aren't I? So ukishaona tu I am ujue negative tag yake ni " aren't I"
2.Let’s go to the beach, shall we?
3.Wait a minute, can you?
4.There is a mosque in that street, isn’t there?

Kwa Leo naishia hapa, naomba atakayekuwa ameelewa ajibu haya. Ambaye hajaelewa nakaribisha maswali.

I don't need to finish this today.
James is working on that.
Your parents have retired.
The phone didn't ring.
It was raining that day.
Your mum hadn't met him before.

Note, Ni kwa wasiojua tu, kwa wanaojua mnakaribishwa kuongezea au kunikosoa nilipokosea.
 
I don't need to finish this today...Do i?
James is working on that...... Isn't he?
Your parents have retired.....haven't they?
The phone didn't ring....... did it?
It was raining that day... wasn't it?
Your mum hadn't met him before.....had she?
 
I don't need to finish this today...Do i?
James is working on that...... Isn't he?
Your parents have retired.....haven't they?
The phone didn't ring....... did it?
It was raining that day... wasn't it?
Your mum hadn't met him before.....had she?
Safi sana.

The bus stop's over there.
She's Italian.
They live in London.
We're working tomorrow.
It was cold yesterday.
He went to the party last night.
We were waiting at the station,
None of those customers were happy.
They could hear me.
You won't tell anyone.
 
Asante sana uu ugonjwa was watu wengi, watu wengig sana hawajui kutengeneza question tags wengi sana tena wengine wasomi kabisa uwa nasikia napotezea.
 
Mkuu sayansi haipo kwa ajili ya wanaume tu, angalia vipanga wa NECTA nani wanaongoza? kujifunza hii lugha haimaniishi watu hawajui hizo sayansi, umekariri mtu kufahamu kingereza lazima asome arts.
Najua vikisu vya NECTA tu ,siwajui hao vipanga unawasemea,sijakariri unavyosema wala sipendi kuwa mtumwa wa lugha unavyofikiria.
 
Oooh yes yes the things of speaking england. We all is know I is the most best of talking england, I is minus my contribution of questin tags.

You human is must know to use @ when is you want to question tag e.g I is tall, @ I?

When you is become now the very expert you use cc e.g I is tall, cc I?

In shortest you is do it like in FB or JF

Thank is you
 
Question tags, ni maswali mafupi mwisho wa sentensi. Tunatumia question tags pale ambapo tunategemea msikilizaji au msomaji kukubaliana na maelezo yetu. Mfano isn't it?, can you?wasn't it? Have they? Nakuendelea.

Ili kuweza kutengeneza hizi question tags inabidi ujue kama sentensi ni "positive au negative statement". Kama statement ni positive tunatumia question tag ya negative na kinyume chake ni sahihi...
Hii mitongoo ungeiandika kwa Kiswahili ungetusaidia sana sisi tusio jua hata maana ya hayo maswali mafupi mafupi ya Kiingereza.

"400kV Tapped"
 
Hii mitongoo ungeiandika kwa Kiswahili ungetusaidia sana sisi tusio jua hata maana ya hayo maswali mafupi mafupi ya Kiingereza.

"400kV Tapped"
Hii ni kwa ajili ya wanaojua kingereza lakina wanashindwa kutengeneza hizo question tags.
 
Sawa, nikajua mpaka sisi ambao hatujui lakini tunapenda kujua hili somo tunahusika.

Ahsante, tuko pamoja, ukiweka somo ambalo mpaka sisi tusio jua ila tunapenda kujua unistue au mtukumbuke kumbuke na sisi tusio jua.

"400kV Tapped"
Sawa nikiweka nitakuita.
 
Back
Top Bottom