Kwanza kuna kanuni moja hivi huwa napemda kuitumia kwamba ukiwa na vitu ukiwa na machaguo mawili na chaguo moja likawa si sahihi inamaana kuna uwezekano mkubwa wa lile lililobaki kuwa sahihi.
Tuje sasa
Tunafundishwa kuwa mungu ni mkuu, anajua yote hadi yajayo. Kwa mantiki hiyo tunaweza kusema kwamba katika kipindi fulani huko nyuma kabla mungu hajaumba dunia alijua kuwa angeumbwa dunia, angewaumba watu, na hao watu wangekuja kumuasi na wangine wasingemuasi. Alijua kuwa ambao wangemuasi angewachoma moto na wale wengine wangeenda peponi. Sasa shida inakuja, sasa kama mungu mwenyewe tangu hajaumba ulimwengu alikuwa anajua fulani atakuja kuchomwa, ina maana binadamu hatuko huru, tunaishi kutokana na misingi iliyowekwa katika kipindi kisichopimika huko nyuma, kitu ambacho kinanifanya mimi nimtazame mungu kama asiye na haki. Au sasa labda tuseme kuwa mungu hajui yajayo ila anategemea utendaji wetu ili kuiamua kesho iweje, kutoka dunia ameiumba amekuwa akiona kuwa ni haiwezekani kabisa kwa binadamu kuishi bila kumkosea yeye kwa sababu hata malaika aliowaumba mwenyewe na kukaa nao mbinguni wakimtumikia yeye walimuasi, anasubiri nini kubadilisha mfumo wa utendaji kwa wanadamu na malaika? Kwa sababu mfumo wa kitu fulani ukishindwa kufanya kazi tatizo si hicho kitu, bali ni mfumk na kama mfumo ni mbovu anayewajibika na aliyeutengeneza huo mfumo. Kwa misingi hiyo miwili mimi huwa naona kuwa mungu hayuko aidha katika msingi wa kwanza au wa pili. Huwa naamini kuwa aliumba katika sanaa yake tu. Kwa nini, iko hivi
Kwanza, Kitu A kikitaka kutengeneza/kukimiki kitu kisichofanana na chenyewe (labda tuseme B) ni A ndicho kitakachojua ni kwa nini kimetengeneza/nimekimiliki B na kwa ajili ya kazi gani. Kwa misingi hiyo kitu B hakiwezi kujua ni kwa nini kimetengenezwa/kimemilikiwa. Hivyo malengo halisi ya kutengenezwa kwa kitu anayajua mtengenezaji na si kile kilichotengenezwa. Kwa mfano wewe umepata dili la kupeleka karanga katika kiwanda cba diamond karanga hivyo ukaamua kulima karanga. Ile mimea ya karanga haiwezi kujua ni kwa nini ipo pale na itaelekea wapi, itakachokifanya ni kukua kutokana na kanuni zinazoiongoza jamii yake, ila wewe uliyezipanda ndo utakuwa unajua kuwa sasa zimetoa maua, zimekomaa, nizing'oe nk. Kwa msingi huo sisi binadamu ni vigumu sana kujua ni kwa nini tupo hapa na tutakwenda wapi baada ya hapa na tunachokifanya ni kuishi tu kutokana na mazingira tuliyoyakuta. Anayejua ni kwa nini sisi tuko hapa ni mungu mwenyewe tu.
Lakini pia unapokitenheneza kitu, kitu hicho kitakuwa kinaonvozwa na kanuni zile zile miaka na miaka. Kwa hiyo wewe ukienda tofauti na kanuni au chenyewe kikaenda tofauti na kanuni lazima kuna tokeo jingine litatokea kulingana na kitendo hicho. Kwa hiyo mimi naamini mungu aliuumba ulimwengu kwa sababu zake binafsi ambazo sisi hutuzijui na akaweka kanuni ambazo ndizo zinauongoza ulimwengu katila kila nyanja kata zile ambazo tu adhani ni za kawaida sana.
Lakini pia duniani kuna vitu vingi vinatokea am avyo tunamhusisha mungu moja kwa moja bila kuchunguz zaidi. Tunapozungumzia ulimwengu tunamaanisha eneo kubwa sana ambalo halina kikomo (au kikkmo hake hakijulikani), na huko pia kuna viumbe ambao nao wameumbwa na mungu na wanaishi kwa kufuata kanuni fulani fulani zilizowekwa na mungu. Lakini kwa hali ya kawaida huenda kuna vitu wanavifanya huko na kuleta matokeo fulani duniani (matokeo mabaya au mazuri) na sisi tunamhusisha mungu moja kwa moja. Wazo hili lilinijia wakati tukifanya mazoezi ya sanaa ya maigizo. Wakati tunawasubiri watu waje ili tuanze mazoezi kuna dada mmoja alikuja na chakula (wali) tukaanza kula, wakati tukila kuna baadhi ya vipande vilidondoka chini na sisimizi wakaanza kuvibeba. Baada ya kumaliza kula na watu kufika ilibidi tufagie pale ili tuanze mazoezi na katika kufagia sisimizi na vyakula vyao waziparuliwa na kutupwa huko. Sasa wakati hayo yakiendelea nikaamua kujiweka katika nafasi ya sisimizi na binadamu kwa wakati mmoja.
1. Mimi sisimizi niko ndani nimesikia harufu ya chakula huko juu, aisee mungu mkubwa bwana ameleta chakula. Je, ni kweli chakula hicho kililetwa na mungu kwa ajili ya sisimizi? Tulimuwa tunakula kikadondoka kwa bahati nbaya.
2. Mimi sisimizi, wakati nabeba chakula kuna likitu nisillolifahamu limekuja na kunisukuma mbali, wenzangu wengi wamekufa na kujeruhiwa. Wazo no 1: atakuwa ni shetani, mungu naomba unisaidie, shetani ashindwe. Wazo no 2: huenda nimefanya kosa mungu ananiadhibu, mungu naomba unisamehe. Je, ni kweli kitendo cha kufagiwa kwa sisimizi kumeletwa na mungu? Sisk tulikuwa tunafagia ili tufanye mazoezi.
Kwa hiyo hata mambo mengi hapa duniani yanatokea na tunamhusisha.mungu moja kwa moja lakini kumbe ni matokeo ya muingiliano katika jamii zilizo nje ya ulimwengu.