Karibuni nyumbani!

Karibuni nyumbani!

Siji kwako kwa maana nikiangali chini kizunguzungu labda roho niache home
 
Mchezo wa chupa hebu fafanua unakuwaje?

Kichupa ni mchezo wa kutoa uoga!
Unasimama na unaelingana nae kimo/urefu, mnapeana migongo,
mnafungana mikono kwa kutumia visigino/vipepsi ><
alafu unainama chini mwenzako anakua juu ya mgongo wako, kila ukiinama chini unamuinua juu kinyume nyume, alafu unamrudisha na anakuinua yeye huku mnaimba: m1 anaimba "kichupa" mwengine anaitikia "cha mafuta mazuri" ivo ivo mpaka mnachoka na kuanza mchezo maalum!
 
Siji kwako kwa maana nikiangali chini kizunguzungu labda roho niache home

Hahahahahahaaaaa! Usijali ICHANA kama ukiangalia chini unahisi kizunguzungu, nitakufunga kitambaa cha macho usione chini!
Karibu nyumbani ICHANA!
 
Hahahahahaaa!
Bulldog kuja kwenu haina shida yoyote wala usijali! But King majuto alisema "mtu huondoa mwiba wa makalioni kwanza ili akae kitako na kuutoa mwiba wa mguuni!"

Kwani na kwenu kuna njia mbaya Bulldog?

Kwetu mbali, usawa wa urefu wa great wall of china
 
Khaa! Usiwe mchoyo kiasi hicho Dina! Au wewe ni anti social?
Karibu tujumuike pamoja, tule bata hadi kuku waone wivu! Nitakua mwenyeji wako!

Potelea mbali....kama kuwa social ni kuning'iniza roho yangu kwenye hizo kamba acha niwe anti-social for good.
 
Hahahahahaaaa! Mamba wa kwetu wanatembea kimisi, hawana spidi, fullu pozi!
...
Gwijimimi mambo vipi?
Umepotea sana kiongozi!!!

Nipo ndugu
Umeniua sana Leo
Lazima nikutimbie maghetoni mwanangu mwenyewe hahaha
 
Hahahahahahaaaa! Usiogope kashesho! Kama wewe sio kibonge sana nitakubeba mgongoni kukupeleka na kukurudisha! Istooshe, nitakuambia ufumbe macho!
Karibu kwangu kashesho!

mmh !! mie kibonge hutaweza kunibeba...asante kwa kunikaribisha
 
grafani11 acha kumbwera, njoo tule banta!
Blu3a.jpg
 
Last edited by a moderator:
Potelea mbali....kama kuwa social ni kuning'iniza roho yangu kwenye hizo kamba acha niwe anti-social for good.

Dina, Dina, Dinaaa!
Nitakuhakikishia usalama wa maisha na viungo vyako kwa asimia mia moja!
Hapo hautovuka mwenyewe! Nitakubeba mgongoni!
Karibu nyumbani Dina!
 
Nipo ndugu
Umeniua sana Leo
Lazima nikutimbie maghetoni mwanangu mwenyewe hahaha

Hahahahahahaaaa!
Karibu sana Gwijimimi, afadhali utanisaidia kubeba warembo na kuwavusha hapo!
M/me yeyote atakae shindwa kuvuka hapo ni heri aogelee!
Lakini hatutombeba! Hahaaaaaa!
 
Kichupa ni mchezo wa kutoa uoga!
Unasimama na unaelingana nae kimo/urefu, mnapeana migongo,
mnafungana mikono kwa kutumia visigino/vipepsi ><
alafu unainama chini mwenzako anakua juu ya mgongo wako, kila ukiinama chini unamuinua juu kinyume nyume, alafu unamrudisha na anakuinua yeye huku mnaimba: m1 anaimba "kichupa" mwengine anaitikia "cha mafuta mazuri" ivo ivo mpaka mnachoka na kuanza mchezo maalum!
Nishaufahamu ila sisi hatukuwa tunaimba tunaenda kimya kimya, halafu nakuongezea mchezo mwingine sijui wewe ushawahi ucheza mnatafuta tairi(uswazi tunaita pila) ambalo halina rim mmoja anaingia kati wengine nje wanalisukuma. Mchezo mwingine sarakasi za kudunda na pila, kutembea na mikono(kichwa chini miguu juu), kujibinjua kwa nyuma mikono hadi inashika sakafu, mara beki daa hadi raha. Watoto wa siku hizi michezo yao Playstation tofauti na sisi michezo yetu lazima uwe fiti damu inachemka huwezi lia dushelele haliinuki mara nini sijui.

Mpira wa miguu ndio usiseme mnakipiga huku nje watu wanaimba Santiagoooo santiagooo Chileeee, mipira hiyo sio mchezo - nyavu za kamba, miguu chini(bila ya njuna)

Tuliocheza mipira hii tunajuana pande kama Mwananyamala, Mtambani, Makurumla, Tandika aisee listi ni ndefu sana nitajaza ukurasa. Labda nimalizie uwanja wa bora Barcelona na kina Gonga wakimaliza zamu ya mitoto mitundu hiyo tunakamata ulingo hadi usiku unaingia.
 
Back
Top Bottom