Karibuni mjiunge na chama cha kijamii

HOTUBA YA UTAMBULISHO WA CHAMA KIPYA CHA SIASA NCHINI CHA CCK


CCK ni Conservatives? Kweli, kuna desturi na maadili mengi sana yamemomonyoka, lakini hamuoni kwamba kila mtanzania anakimbilia modernity? ambayo ipo ndani ya demokrasia na maendeleo?


Kuna makala ya mchambuzi alitueleza kwamba soko lipo tu chini ya mfumo wowote na kwamba Soko lilikuwepo enziii, hata kabla ya ubepari kuingia duniani. Chini ya ubepari, soko limebadilika tu na kuwa soko huria.


Mwalimu Nyerere na Ubapari tena? Mchambuzi pia alitukumbusha lengo kuu la Ujamaa ni kuleta mapinduzi ya kumwangamiza bwanyenye, sasa vipi tena hapo Nyerere na Ubepari? Mapinduzi ya CCM yalikuwa kumtupilia mbali Bwanyenye. Lakini tofauti na zamani, hivi sasa, Bila ya Mabwanyenye, CCM haiwezekani. Na hawa ndio wamekamata Chama, na wanalisha sumu wale wanaotaka kuendeleza flfasa ya MAPINDUZI katika CCM. Jifunzeni kwa Nape.

Kwa kweli ni chama mbadala hasa wa CCM na kinataka kuwarudishia wananchi wa Tanzania fahari yao. Tunataka kurudisha ule moyo wa uzalendo, kuipenda Tanzania na kuona fahari kuwa sisi ni Watanzania.

Kuna kilicho mbadala wa CCM zaidi ya Chadema? CDM tunachukua nchi 2015. Prove me Wrong!!!
 
Naomba anwani ya tovuti nikasome katiba na itikadi ya Chama.
 

miongoni mwa taratibu za kupata walau usajili wa muda ni pamoja na kuwa na katiba,sasa kwa chama kilichopata usajili wa kudumu ni wazi hilo si swali,

kuhusu uchaguzi, ni kuwa hakuna chama kisichokuwa na uongozi wa kukianzisha na sie ni miongoni mwao,tunataraji kufanya uchaguzi kuanzia ngazi ya matawi,kata,wilaya,mkoa na taifa muda si mrefu,karibu ujiunge na upate nafasi ya kugombea

sifa za kupata usajili wa kudumu ni angalau kuwa na wanachama 200 kwa mikoa kumi,kati ya hiyo miwili itoke zanzibar

kuhusu ofisi zetu,zipo za muda sinza maeneo ya legho

pesa zetu zinatoka kwa wanachama wanaokichangia fedha na rasilimali mbalimbali wakijua hiki ndio chama chao cha kuleta ukombozi wa kweli.

swala la muungano ni hoja pana ambayo kupitia mchakato wa katiba mpya,kila mtanzania atapata nafasi pana ya kutoa mawazo na mtazamo wake katika hilo
 


hapo kwenye red: hii inaonyesha namna watanzania tulivyo wavivu wa kufikiri,haiingii akilini kudhani ya kuwa ukiwa mwanachama wa magwanda basi wewe ndo mpinzani,NAAMINI kabisa kuwa chama ni itikadi,itikadi ni imani,kama itikadi yao hao CCK haifanani na chama cha magwanda ni sahihi kabisa kuwa na chama cha itikadi wanayoiona inafaa,itakumbuklwa hata CUF waliwahi kusema chadema wametumwa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005,ni kama vile walitaka kuungwa mkono wao tu na si wengine kusimama kivyao,hii ni changamoto na ni lazima tuikubali
 
CCJ= Chukua Chako Jiondoe (ISSUE IMEKAA KI RUZUKU RUZUKU)

soma hapa tafadhali,maana inaonekana watu hamsomi na mnakurupuka kujibu


Mfumo wa siasa hapa nchini Mojawapo ya matatizo makubwa ambayo yanatusumbua sasa hivi nchini na ambayo athari zake zinatoka kizazi kimoja kwenda kingine ni mfumo wetu wa kisiasa nchini. CCK inaamini kuwa mfumo huu wa kisiasa umepitwa na wakati na hauendani kabisa na matamanio ya kujenga taifa la kidemokrasia. Baadhi ya vitu ambavyo tunaamini vimepitwa na wakati na ambavyo vinahitaji kuondolewa mapema zaidi ni suala la ruzuku kwa vyama vya siasa.

Mfumo wa ruzuku uliingizwa kwenye siasa zetu na CCM kwa ajili ya kutafuta njia rahisi ya kupora raslimali zetu na kujinufaisha kwa migongo ya Watanzania. Hakuna sababu wala ulazima wa chama cha siasa kupewa fedha za umma kwa sababu tu ina watu waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali – huu ni wizi wa wazi! Sisi kama CCK tunataka na tutapigania hatimaye kuondolewa kwa mfumo huu wa ruzuku kwa vyama vya siasa kwani vinazawadia uzembe na ubadhirifu.

Iweje chama ambacho kimeshindwa kusimamia serikali yake na ufisadi umeshamiri chini yake bado kinapewa kila mwezi mabilioni ya fedha ambayo hayajafungwa na utendaji kazi wa chama hicho?

Yaani, haijalishi CCM inatawalaje lakini bado inalipwa kila mwezi na Watanzania! Hivyo, kinyume na vyama ambavyo vinaweza kudaiwa kuwa vimeundwa kwa ajili ya ruzuku CCK imeundwa huku ikiwa inatambua kuwa mfumo wa ruzuku ni wa hatari kwenye siasa zetu na kwa kweli ndio umechangia sana kuchelewesha kung’olewa kwa CCM madarakani!

Hivyo, katika mjadala wa Katiba Mpya sisi kama chama tutapigania na kuhakikisha kuwa ruzuku kwa vyama vya siasa zinafutwa ili kila chama kitegemee wanachama wake na akili zake kujiendesha. Kwani TANU ilipewa ruzuku na serikali ya Mkoloni ili ifanye siasa? Si ilitegemea wanachama wake? Kwanini kama wakati huo iliwezekana leo ishindikane?
 
Mie mkinilipa ntawafanyia kazi zenu. Bure hamnipati.
Asante sana, sasa hapa umeteguwa kitendawili kwahiyo tunafahamu vyema sasa kwamba upo hapa JF kwa malipo maalum!! ila sidhani kama kuna chama kinachoweza kukulipa ujila wako zaidi ya CCM.
 

Maandishi ni jambo lingine na utekelezaji ni jambo lingine, CCM kina sera nzuri sana lakini je zinatekelezwa? kadi ya mwana CCM nyuma imeandikwa hivi:
Rushwa ni adui wa haki, sitotoa wala kupokea rushwa, nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko.
Kwahiyo hizo ngonjera mlizojaza hapo kuwalaghai Watanzania hazina mashiko.
 
hongereni kwa kuona umuhimu wa jf kuwafikia watz!

lakini labda mtueleza ni madhaifu gani mliyoyaona kwenye vyama vilivyopo kiasi kwamba mshindwe kuyatatua na muamue kuunda chama kipya!?

Kila la kheri maana safari hii ni ngumu
 
Kwa sasa hivi silipwi, umenoa, jaribu tena baadae! Tena nilishawahi kumtumia Nape PM kuwa waanze kunilipa maana mashambulizi nnayopata hapa JF yakiambatana na matusi si kazi ndogo. Kanchunia.

Vipi, Mbowe analipa?
Mimi ni mfadhili wa Demokrasia natumia resource zangu kuchangia mabadiliko wala bila kuwa na nia ya uongozi wa kisiasa, na mara nyingi tu nimewafadhili wanaCCM mtaani kwangu kwa shughuli zao za kichama ikiwemo hata kutoa gari yangu kuwasaidia misafara yao.
Nina mahusiano mazuri tu na wanaCCM mtaani kwangu na bado sijamuuwa kuwa mwanachama wa Chadema, nazifahamu siasa za Tanzania vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…